STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 29, 2014

Samuel Eto'oo afunguka 'Sina bifu na Mourinho'

MSHAMBULIAJI mpya wa Evetrion, Samuel Eto'o ametupilia mbali madai kuwa ana bifu na Jose Mourinho wakati timu yake ikijiandaa kuivaa Chelsea katika mechi ya Ligi Kuu tya England kesho Jumamosi.
Eto’o, Mchezaji wa Kimataifa wa Cameroon, na Meneja wa Chelsea Jose Mourinho walikuwa pamoja huko Inter Milan na kutwaa UEFA CHAMPIONS LIGI pamoja na akaja England Mwaka mmoja uliopita kuungana na Mourinho huko Chelsea.
Lakini uhusiano wa Eto’o na Mourinho ulipata msukosuko pale Mreno huyo aliponaswa kwenye Kamera bila kujijua akidhihaki Umri wa Eto’o na kudai ni Mzee kupita Miaka inayodaiwa anayo.
Mara baada ya tukio hilo Eto’o, mwenye Miaka 33, alifunga Bao akiichezea Chelsea na kwenda kushangilia mithili ya Mzee akishika Kibendera cha Kona kama Mkongojo huku akijishika Kiuno ili kumdhihaki Mourinho.
Akiongea na Wanahabari mara tu baada ya kutambulishwa kama Mchezaji mpya, Eto’o alipuuza madai hayo ya kuwa na bifu na Mourinho na badala yake kusema anamshukuru Mourinho kwa kumleta Ligi Kuu England.

Nae Meneja wa Everton Roberto Martinez amedokeza kuwa huenda Mkongwe huyo wa Cameroon akaivaa Chelsea Jumamosi wakati watakapopambana Goodison Park katika Mechi ya Ligi Kuu England.

Mashali kumvaa Mkenya Novemba 4

 Bondia Thomas Mashali katikati akisaini mkataba wa kucheza na Henry Wandera kutoka Kenya Novemba 4 katika ukumbi wa New Madiba 'Korini' uliopo Tandale Dar es salaam. Wanaoshudia kushoto ni Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za kulipwa nchini TPBO, Yassini Abdallah 'Ustaadh' na promota wa mpambano huo Khamis Ally.
 Rais wa TPBO Yassin Abdallah akirekebisha mkataba wa bondia Thomas Mashali katikati atakayepambana na mkenya Henry Wandera Novemba 4 katika ukumbi wa New Madiba 'Korini' uliopo Tandale Dar es salaam kulia ni  promota wa mpambano huo Khamis Ally 
Bondia Thomas Mashali katikati akiwe Dole Gumba katika mkataba wa kucheza na Henry Wandera kutoka Kenya Novemba 4.
****
BONDIA Thomas Mashali 'Simba Asiyefugika' anatarajia kupanda tena ulingoni Novemba 4 kumvaa Mkenya Henry Wandera katika pambano litakalofanyika katika ukumbi wa New Madiba zamani Korini.
Mashali anapigana akiwa na historia ya kupoteza mpambano wake wa mwisho zaidi ya bondia Mada Maugo ambapo walicheza katika uwanja wa taifa na kupoteza kwa pointi mpambano huo.
Akizungumzia mpambano huo Mashali amesema hatokubali kupoteza tena mchezo huo ukizingatia anachezea nyumbani mahali alipozaliwa na ndipo alipoanzia ngumi maeneo ya Tandale.
"Sintokubali niaibike mbele ya ndugu zangu hivyo nawaambia wapenzi waje kwa wingi kuangalia Mashali anavyofanya kazi yake ya mchezo wa masumbwi.
Naye promota wa mpambano huo Khamis Ally amewahakikishia kuwa sehemu ya kuegeshea magari ni kubwa na ulinzi ni wa kutosha kifupi katika ulinzi tumejipanga vizuri pia siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine mazuri ya utangulizi ambapo mabondia wengi wamejitokeza kucheza siku hiyo.
Siku hiyo pia kutakuwa na uuzwaji wa DVD ambazo zinatoa mwanga kwa mchezaji kujua mchezo na kufahamu zaidi mbinu mpya zitumiwazo na mataifa mbali mbali Duniani.
Wakiwemo mabondia bingwa wa dunia kama Manny Pacquaio, Floyd Maywether, Amir Khan, Muhammed Ali, Mike 'Iron' Tyson na wengine wengi wanaotamba na waliotamba katika mchezo huo wa masumbwi Duniani.
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ametoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza kutoa sapoti ya mchezo wa masumbwi kwani ndio mchezo pekee unaoweza kututoa kimasomaso watanzania tukafurahi.

Kikwazo cha Tanzania kuandaa AFCON 2017 HIKI HAPA!

http://bigeye.ug/wp-content/uploads/2014/08/afcon-trophy.pngSHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeliandikia Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kutaka kipengele cha kutaka kwanza nchi iandae Fainali za Afrika kwa Vijana ndiyo iwe na sifa ya kuandaa Fainali za Afrika (AFCON) kiondolewe.
TFF ilishapeleka barua CAF kutaka kipengele hicho kiondolewe, na kutaka kijadiliwe katika Congress (Mkutano Mkuu) ijayo ya CAF.
Tanzania imeshaiandikia CAF barua kuomba uenyeji wa Fainali za AFCON za 2017 baada ya Libya iliyokuwa imepewe uenyeji huo kujitoa. Uamuzi wa Tanzania kuomba kuandaa fainali hizo ulifanywa na Kamati ya Utendaji ya TFF iliyokutana Agosti 24 mwaka huu.

Malinzi kuzuru Kanda ya Kaskazini, mechi za Electronic kupigwa TA, BK

http://in2eastafrica.net/wp-content/uploads/2013/10/Jamal-Malinzi.jpgTIMU za Mgambo Shooting na African Sports za Tanga zitapambana Jumapili (Agosti 31 mwaka huu) katika mechi ya majaribio ya matumizi ya tiketi za elektroniki itakayochezwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kwa kiingilio cha sh. 1,000 tu.
Mechi nyingine ya tiketi za elektroniki siku hiyo itachezwa Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba kwa kuzikutanisha timu za Kagera Sugar na Geita Gold SC ya mkoani Geita. Geita Gold iko Daraja la Kwanza.
Kabla ya mechi hizo, Ijumaa (Agosti 29 mwaka huu) saa 3 asubuhi kwenye viwanja hivyo kutakuwa na mafunzo ya matumizi ya tiketi za elektroniki pamoja na jinsi mfumo huo unavyofanya kazi.
Washiriki wa mafunzo hayo ni wasimamizi wa vituo vya Tanga na Bukoba, viongozi wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa ya Kagera (KRFA) na Tanga (TRFA), makatibu na maofisa habari wa klabu za Kagera Sugar, Mgambo Shooting, African Sports na Geita Gold, mameneja wa viwanja vya Kaitaba na Mkwakwani na wasaidizi wao, maofisa usalama wa TRFA na KRFA, wachanaji tiketi, wasimamizi wa milangoni, wasaidizi (stewards) na waandishi wa habari.
Wakati huo huo Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atatembelea mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara.
Katika ziara hiyo atakutana na viongozi na kuangalia hali hali ya mpira wa miguu katika mikoa hiyo na mahitaji yake. Pia atazungumzia maono (vision) ya TFF katika mpira wa miguu.
Rais Malinzi atawasili mkoani Manyara, Agosti 29 mwaka huu, na ataanza ziara rasmi katika mkoa huo Agosti 30 mwaka huu. Agosti 31 mwaka huu atakuwa Arusha, na kumalizia Septemba 1 mkoani Kilimanjaro.
Katika ziara hiyo, Rais Malinzi atafuatana na Mkurugenzi Msaidizi (Wanachama) wa TFF, Eliud Mvella. Pia Septemba 8 mwaka huu, Rais Malinzi ataanza ziara ya mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe.

Kenya, Rwanda, Uganda kuandaa pamoja Afcon 2017?

http://www.thepeople.co.ke/wp-content/uploads/2014/04/Screen-Shot-2014-04-12-at-8.13.22-AM.png
Sam Nyamweya
NAIROBI, Kenya
KENYA, Rwanda na Uganda zinajadili uwezekano kupeleka maombi Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuandaa kwa pamoja fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2017.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka nchini Kenya (FKF), Sam Nyamweya Jumatano alithibitisha kuwa mipango iliyopo ni kwa nchi tatu kuungana kuomba kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ya Afrika ili kupunguza gharama.
 "Ni mwenye furaha kwamba Uganda na Rwanda wamepokea kwa mikono miwili wazo la FKF la kuungana kuomba uenyeji wa Mataifa ya Afrika 2017 ambayo ipo wazi kutokana na Libya kujitoa kuwa mwenyeji," alisema Nyamweya.
Libya haitakuwa mwenyeji wa Afcon 2017 kutokana na mapigano ya kisiasa nchini humo ambayo yamesababisha kuchelewa kwa mipango ya ujenzi wa viwanja vitakavyotosha timu 16 zinazoshiriki michuano hiyo.
Nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika ilipanga kujenga viwanja 11 kwa gharama ya Dola za Kimarekani 314 ikiwa ni pamoja na unaochukua watazamaji 60,000 eneo la kambi ya jeshi jijini Tripoli.
CAF imekaribisha maombi kwa nchi zinazohitaji kuandaa michuano hiyo, na milango ipo wazi hadi Septemba 30. Uamuzi wa nchi itakayopewa nafasi hiyo ya Libya utatolewa mwakani.

Waamuzi, makamisaa kutahiniwa Sept 5

http://2.bp.blogspot.com/-i5fCDTwnoak/UI6U-vJJl6I/AAAAAAAAagE/F7NZ-AyBkbg/s1600/DSC_8192.JPG
Waamuzi wanatakiwa kuwa fiti kama hivi wawapo uwanjani
MTIHANI wa utimamu wa mwili (physical fitness test) kwa waamuzi wanaotaka kuchezesha mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu utafanyika katika vituo viwili kuanzia Septemba 5-6 mwaka huu.
Waamuzi watakaoshiriki mtihani huo ni wenye beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) na wale wa class one. Pia kutakuwa na semina wa makamishna wanaotaka kusimamia mechi za VPL na FDL ambayo itafanyika Septemba 7 mwaka huu.
Vituo vya mtihani huo ni Dar es Salaam na Shinyanga. Kituo cha Dar es Salaam ni kwa waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma, Iringa, Kilimanjaro, Lindi, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Njombe, Pwani, Ruvuma na Tanga.
Kituo cha Shinyanga ni kwa waamuzi na makamishna kutoka mikoa ya Arusha, Geita, Kagera, Katavi, Kigoma, Manyara, Mara, Mwanza, Rukwa, Shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora.
Waamuzi wote ambao wamechezesha VPL na FDL msimu wa 2013/2014 na kupata matatizo au kuondolewa kwenye ligi hawahusiki na mtihani huo.
Washiriki wanatakiwa kufika kituoni siku moja kabla.Wasimamizi ni Charles Ndagala, Israel Mujuni, Issarow Chacha, Joan Minja, Pascal Chiganga, Riziki Majala, Said Nassoro, Salum Chama, Soud Abdi, Victor Mwandike na Zahara Mohamed.

KOZI YA UKUFUNZI WA UTAWALA YA FIFA KUFANYIKA DESEMBA

http://3.bp.blogspot.com/-wvfWxpMOFiY/U_-DZP5sXQI/AAAAAAAAfmw/WJ4TokM-bfQ/s1600/mwesigwa.JPG
Katibu Mkuu wa TFF, Celestine Mwesigwa aliyesimama
SHIRIKISHO la Soka Tanzania,TFF kwa kushirikiana na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) wameandaa kozi ya ukufunzi wa utawala itakayofanyika Desemba mwaka huu.
Kozi hiyo itakayoendeshwa na wakufunzi kutoka FIFA itafanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Desemba 1 hadi 5 mwaka huu, ambapo sifa ya chini ya elimu kwa wanaotaka kushiriki ni kidato cha nne.
Kwa wanaotaka kushiriki kozi hiyo wanatakiwa kutuma maombi yao kwa Katibu Mkuu wa TFF. 
Mwisho wa kupokea maombi hayo ni Septemba 5 mwaka huu ambapo wanatakiwa pia kuwasilisha nakala za vyeti vyao vya kitaaluma.

Wenger akiri Giroud kuwa nje, akiwakana Falcao, Song Emirates

http://static.goal.com/310700/310713_heroa.jpg
Arsene Wenger
http://www.footmercato.net/images/a/falcao-cible-potentielle-des-gunners_101362.jpg
Falcao
http://www.standard.co.uk/incoming/article8026635.ece/alternates/w620/alex-song.jpg
Alex Song
MENEJA wa Arsenal , Arsene Wenger amethibitisha kuwa Olivier Giroud anatarajiwa kuwa nje ya uwanja hadi angalau Desemba kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu lakini akasisitiza kuwa hana mpango wa kusaka mshambuliaji mwingine yeyeote akiwakana Radamel Falcao, Alex Song na Danny Welbeck.
Giroud (27), ambaye alikuwa mfungaji bora wa Arsenal msimu uliopita akitupia mabao 22 katika michuano yote, anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa kufikia miezi minne kufuatia kufanyiwa upasuaji wa 'enka' aliyoumia katika mechi ya Jumamosi iliyomalizika kwa sare ya 2-2 ugenini dhidi ya Everton katika Ligi Kuu ya England.
Alipoulizwa kuhusu Falcao, Wenger alisema nyota huyo wa Napoli hayumo katika mipaka ya bei anayoweza kutoa na akabainisha kwamba pia hamhitaji Welbeck. Kuhusu uwezekano wa kumsajili Song, Mfaransa huyo alisema: "Alex Song hatarejea hapa."
Kocha huyo akasema kuhusu nyota wa Chile, aliyefunga goli la ushindi katika mechi ya "kapu" ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Besiktas: "(Alexis anaweza kucheza kama mshambuliaji wa kati) kwa miezi mitatu ama minne? Anaweza kucheza pale maisha yake yote.
"Nilimnunua acheze kama mshambuliaji wa kati, siyo kwenye wingi. Naamini huwezi kununua kila pale mchezaji anapoumia. Kama umepata majeruhi Septemba mosi bado utatakiwa kuishi nalo.
"Nilimnunua Sanchez awe mshambuliaji, Walcott anaweza kuwa mshambuliaji mzuri, (Lukas) Podolski anaweza kucheza pale, (Yaya) Sanogo ni mshambuliaji mzuri sana, (Joel) Campbell ukimuuliza yeye ni nani, atasema ni mshambuliaji. Wote ni wachezaji wa ubora wa juu.
"Kupata wachezaji bora zaidi ya tulionao itakuwa ngumu sana."

BRAD PITT NA ANGELINA JOLIE WAOANA!


Jolie na Pit walichumbiana mwaka 2012
NYOTA wa filamu duniani, Brad Pitt na Angelina Jolie ambao wameishi kwa muda mrefu kama mke na mume, wamefunga ndoa rasmi.
Pitt, mwenye umri wa miaka 50 na Jolie mwenye umri wa miaka 39, walifunga pingu za maisha nchini Ufaransa Jumamosi na kumaliza miaka mingi ya sintofahamu ikiwa watawahi kuoana.
Waigizaji hao inaarifiwa walioana katika sherehe iliyofanywa kimya kimya katika kanisa ndogo eneo la Chateau Miraval Ufaransa.
Sherehe hio ilifanyika kwa faragha na kuhudhuriwa tu na familia za wawili hao pamoja na marafiki zao.
Watoto wao pia walihusishwa katika sherehe hiyo.
Jolie aliambatana na wanawe wakubwa wa kiume, Maddox na Pax, wenye umri wa miaka 13 na 10 mtawalia.
Watoto wao wa kike Zahara na Vivienne, wote waliwarushia mauwa wazazi wao walipokuwa wanatembea kuelekea kanisani. Inaarifiwa sherehe hiyo haikufuata dini yoyote.
Wacheza filamu hao walianza uhusiano wao wa kimapenzi mwaka 2005 walipoigiza katika filamu ya 'Mr and Mrs Smith'. Walichumbiana Aprili mwaka 2012.
Kabla ya ndoa yake kwa Jolie, Pit alikuwa amemuoa muigizaji, Jennifer Aniston, wakati Jolie alikuwa ameolewa na Jonny Lee Miller na Billy Bob Thornton. Ndoa yake kwa wawili hao ilivunjika
BIG