STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 29, 2014

Mashali kumvaa Mkenya Novemba 4

 Bondia Thomas Mashali katikati akisaini mkataba wa kucheza na Henry Wandera kutoka Kenya Novemba 4 katika ukumbi wa New Madiba 'Korini' uliopo Tandale Dar es salaam. Wanaoshudia kushoto ni Rais wa Oganaizesheni ya Ngumi za kulipwa nchini TPBO, Yassini Abdallah 'Ustaadh' na promota wa mpambano huo Khamis Ally.
 Rais wa TPBO Yassin Abdallah akirekebisha mkataba wa bondia Thomas Mashali katikati atakayepambana na mkenya Henry Wandera Novemba 4 katika ukumbi wa New Madiba 'Korini' uliopo Tandale Dar es salaam kulia ni  promota wa mpambano huo Khamis Ally 
Bondia Thomas Mashali katikati akiwe Dole Gumba katika mkataba wa kucheza na Henry Wandera kutoka Kenya Novemba 4.
****
BONDIA Thomas Mashali 'Simba Asiyefugika' anatarajia kupanda tena ulingoni Novemba 4 kumvaa Mkenya Henry Wandera katika pambano litakalofanyika katika ukumbi wa New Madiba zamani Korini.
Mashali anapigana akiwa na historia ya kupoteza mpambano wake wa mwisho zaidi ya bondia Mada Maugo ambapo walicheza katika uwanja wa taifa na kupoteza kwa pointi mpambano huo.
Akizungumzia mpambano huo Mashali amesema hatokubali kupoteza tena mchezo huo ukizingatia anachezea nyumbani mahali alipozaliwa na ndipo alipoanzia ngumi maeneo ya Tandale.
"Sintokubali niaibike mbele ya ndugu zangu hivyo nawaambia wapenzi waje kwa wingi kuangalia Mashali anavyofanya kazi yake ya mchezo wa masumbwi.
Naye promota wa mpambano huo Khamis Ally amewahakikishia kuwa sehemu ya kuegeshea magari ni kubwa na ulinzi ni wa kutosha kifupi katika ulinzi tumejipanga vizuri pia siku hiyo kutakuwa na mapambano mengine mazuri ya utangulizi ambapo mabondia wengi wamejitokeza kucheza siku hiyo.
Siku hiyo pia kutakuwa na uuzwaji wa DVD ambazo zinatoa mwanga kwa mchezaji kujua mchezo na kufahamu zaidi mbinu mpya zitumiwazo na mataifa mbali mbali Duniani.
Wakiwemo mabondia bingwa wa dunia kama Manny Pacquaio, Floyd Maywether, Amir Khan, Muhammed Ali, Mike 'Iron' Tyson na wengine wengi wanaotamba na waliotamba katika mchezo huo wa masumbwi Duniani.
Kocha wa Kimataifa wa mchezo wa ngumi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ametoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza kutoa sapoti ya mchezo wa masumbwi kwani ndio mchezo pekee unaoweza kututoa kimasomaso watanzania tukafurahi.

No comments:

Post a Comment