Samuel Eto'oo afunguka 'Sina bifu na Mourinho'
MSHAMBULIAJI mpya wa Evetrion, Samuel
Eto'o ametupilia mbali madai kuwa ana bifu na Jose Mourinho wakati timu
yake ikijiandaa kuivaa Chelsea katika mechi ya Ligi Kuu tya England kesho Jumamosi.
Eto’o, Mchezaji wa Kimataifa wa Cameroon, na Meneja
wa Chelsea Jose Mourinho walikuwa pamoja huko Inter Milan na kutwaa UEFA
CHAMPIONS LIGI pamoja na akaja England Mwaka mmoja uliopita kuungana na
Mourinho huko Chelsea.
Lakini uhusiano wa Eto’o na Mourinho ulipata
msukosuko pale Mreno huyo aliponaswa kwenye Kamera bila kujijua
akidhihaki Umri wa Eto’o na kudai ni Mzee kupita Miaka inayodaiwa anayo.
Mara
baada ya tukio hilo Eto’o, mwenye Miaka 33, alifunga Bao akiichezea
Chelsea na kwenda kushangilia mithili ya Mzee akishika Kibendera cha
Kona kama Mkongojo huku akijishika Kiuno ili kumdhihaki Mourinho.
Akiongea
na Wanahabari mara tu baada ya kutambulishwa kama Mchezaji mpya, Eto’o
alipuuza madai hayo ya kuwa na bifu na Mourinho na badala yake kusema
anamshukuru Mourinho kwa kumleta Ligi Kuu England.
Nae Meneja wa Everton Roberto Martinez
amedokeza kuwa huenda Mkongwe huyo wa Cameroon akaivaa Chelsea Jumamosi
wakati watakapopambana Goodison Park katika Mechi ya Ligi Kuu England.
No comments:
Post a Comment