STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 29, 2014

Wenger akiri Giroud kuwa nje, akiwakana Falcao, Song Emirates

http://static.goal.com/310700/310713_heroa.jpg
Arsene Wenger
http://www.footmercato.net/images/a/falcao-cible-potentielle-des-gunners_101362.jpg
Falcao
http://www.standard.co.uk/incoming/article8026635.ece/alternates/w620/alex-song.jpg
Alex Song
MENEJA wa Arsenal , Arsene Wenger amethibitisha kuwa Olivier Giroud anatarajiwa kuwa nje ya uwanja hadi angalau Desemba kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu lakini akasisitiza kuwa hana mpango wa kusaka mshambuliaji mwingine yeyeote akiwakana Radamel Falcao, Alex Song na Danny Welbeck.
Giroud (27), ambaye alikuwa mfungaji bora wa Arsenal msimu uliopita akitupia mabao 22 katika michuano yote, anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa kufikia miezi minne kufuatia kufanyiwa upasuaji wa 'enka' aliyoumia katika mechi ya Jumamosi iliyomalizika kwa sare ya 2-2 ugenini dhidi ya Everton katika Ligi Kuu ya England.
Alipoulizwa kuhusu Falcao, Wenger alisema nyota huyo wa Napoli hayumo katika mipaka ya bei anayoweza kutoa na akabainisha kwamba pia hamhitaji Welbeck. Kuhusu uwezekano wa kumsajili Song, Mfaransa huyo alisema: "Alex Song hatarejea hapa."
Kocha huyo akasema kuhusu nyota wa Chile, aliyefunga goli la ushindi katika mechi ya "kapu" ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya dhidi ya Besiktas: "(Alexis anaweza kucheza kama mshambuliaji wa kati) kwa miezi mitatu ama minne? Anaweza kucheza pale maisha yake yote.
"Nilimnunua acheze kama mshambuliaji wa kati, siyo kwenye wingi. Naamini huwezi kununua kila pale mchezaji anapoumia. Kama umepata majeruhi Septemba mosi bado utatakiwa kuishi nalo.
"Nilimnunua Sanchez awe mshambuliaji, Walcott anaweza kuwa mshambuliaji mzuri, (Lukas) Podolski anaweza kucheza pale, (Yaya) Sanogo ni mshambuliaji mzuri sana, (Joel) Campbell ukimuuliza yeye ni nani, atasema ni mshambuliaji. Wote ni wachezaji wa ubora wa juu.
"Kupata wachezaji bora zaidi ya tulionao itakuwa ngumu sana."

No comments:

Post a Comment