STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, August 29, 2014

Kenya, Rwanda, Uganda kuandaa pamoja Afcon 2017?

http://www.thepeople.co.ke/wp-content/uploads/2014/04/Screen-Shot-2014-04-12-at-8.13.22-AM.png
Sam Nyamweya
NAIROBI, Kenya
KENYA, Rwanda na Uganda zinajadili uwezekano kupeleka maombi Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuandaa kwa pamoja fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) 2017.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka nchini Kenya (FKF), Sam Nyamweya Jumatano alithibitisha kuwa mipango iliyopo ni kwa nchi tatu kuungana kuomba kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ya Afrika ili kupunguza gharama.
 "Ni mwenye furaha kwamba Uganda na Rwanda wamepokea kwa mikono miwili wazo la FKF la kuungana kuomba uenyeji wa Mataifa ya Afrika 2017 ambayo ipo wazi kutokana na Libya kujitoa kuwa mwenyeji," alisema Nyamweya.
Libya haitakuwa mwenyeji wa Afcon 2017 kutokana na mapigano ya kisiasa nchini humo ambayo yamesababisha kuchelewa kwa mipango ya ujenzi wa viwanja vitakavyotosha timu 16 zinazoshiriki michuano hiyo.
Nchi hiyo ya Kaskazini mwa Afrika ilipanga kujenga viwanja 11 kwa gharama ya Dola za Kimarekani 314 ikiwa ni pamoja na unaochukua watazamaji 60,000 eneo la kambi ya jeshi jijini Tripoli.
CAF imekaribisha maombi kwa nchi zinazohitaji kuandaa michuano hiyo, na milango ipo wazi hadi Septemba 30. Uamuzi wa nchi itakayopewa nafasi hiyo ya Libya utatolewa mwakani.

No comments:

Post a Comment