STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, October 28, 2013

Mwanajeshi mwingine wa Tanzania auwawa DR Congo, ashambuliwa na Waasi wa M23

Mwanajeshi anayedaiwa kuuwawa DR Congo
WATANZANIA wameendelea kupoteza ndugu zao wanaolinda amani katika mataifa ya nje baada ya taarifa za kwenye mtandao kueleza mwanajeshi aliyekuwa akihudumu katika Jeshi la Kulinda Amani MANUSCO huko DR Congo kuuwawa na waasi wa M23.
Taarifa hizo zinamtaja mwanajeshi huyo kuwa ni Rajab Ahmad Mlima aliyeshambuliwa kwa risasi wakati akijaribu kuwalinda wakazi wa mji wa Kiwanja na Ratshruru Kaskazini mwa mji wa Goma dhidi jeshi la  waasi hao wa M23.
Kifo cha mwanajeshi huyo kimekuja wakati watanzania wakiwa bado hawajasahau mashujaa wao waliouwawa Sudan Kusini na DR Congo hivi karibuni katika harakati za kulinda amani katika nchi hizo.
Mwenyezi Mung Ailaze mahali pema Peponi Roho ya mwanajeshi huyo. Ameen

Chelsea, Spurs zang'ara, Sunderland ikiona mwezi EPL

 
UZEMBE uliofanywa na kipa Joe Hart kutoka golini bila kuwasiliana na beki wake, Nastasic aliyekuwa akimrudishia mpira kwa kichwa, uliiwezesha Chelsea kupata bao lililowapa ushindi dakika ya lala salama na kukwea hadi nafasi ya pili katika Ligi Kuu ya England.
Fernando Torres aliuwahi mpira uluioonekana kama unaelekea nje ya lango lililokuwa wazi la Man City na kuipatia timu yake bao muhimu na kushinda 2-1 kartika pambano lililokuwa kali lililochezwa uwanja wa Stamford Bridge.
Awali, Torres alitoa krosi nzuri kwa Schurrle aliyeifungia Chelsea bao la kuongoza katika dakika ya 32 lililodumu haidi mapumziko kabaal ya wageni kulirejesha dakika tatu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kupitia kwa Sergio 'kun' Aguero.
Katika mechi nyingine zilizochezwa jana, Tottenham iliendelea kufukuzia nafasi za juu baada ya kuinyuka 
Hull City kwa bao 1-0 lililofungwa na Roberto Saldado, nao wachovu wa ligi hiyo Sunderland waliwafunga wapinzani wao Newcastle United kwa mabao 2-1 ikiwa ndiyo ushindi wao wa kwanza msimu huu na timu za Swansea City na West Ham wakitoshana nguvu kwa kutoka 0-0.

Maskini Wema Sepetu! Afiwa na baba yake mzazi

STAA wa filamu na aliyewahi kuwa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu amepatwa na msiba mzito baada ya baba yake mzazi Balozi Issac Abraham  Sepetu kufariki dunia asubuhi ya leo katika Hospitali ya TMJ Mikocheni jijini.
Inaelezwa kuwa, Balozi Sepetu alikuwa amelazwa katika hospital ya TMJ akitibiwa ugonjwa wa Kisukari na kiharusi uliokuwa ukimsumbua kwa muda mrefu sasa.
Hadi umauti unamkuta, Balozi Isaac Sepetu alikuwa ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Uwekezaji wa Vitega Uchumi Zanzibar na taarifa zilizopo ni kwamba anatarajiwa kuzikwa visiwani Zanzibar siku ya kesho.
Mtandao huu wa MICHARAZO MITUPU unaungana na Wema waombolezaji wote kumpa pole Wema Sepetu na familia nzima, ndugu na jamaa wa marehemu Balozi Zepetu na kuwaomba kuwa na subira katika kipindi hiki kigumu kwa kukumbuka kuwa 'Sisi ni wa Mungu na kwake tutarejea. Mwenyezi Mungu, Aiweke Roho ya Marehemu Balozi Isaac Abraham Sepetu, Mahala Pema Peponi. Ameen

Vitali Klitschko aitamani Ikulu ya Ukraine

BINGWA wa uzito wa juu wa WBC raia wa Ukraine, Vitali Klitschko anataka kufuata nyayo za bondia mwenzake, Manny Pacquiao wa Ufilipino kwa kujiingiza kwenye siasa, ila yeye anautaka Urais wa nchi hiyo kwenye uchaguzi wa 2015.
 
Manny Pacquiao pamoja na kuwa mbunge lakini pia anajishughulisha siasa ni mbunge wa Bunge la Ufilipino, hali ambayo imemvutia Klitschko ambaye mwezi Agosti alisema lengo kubwa ni kuifanya Ukraine kuwa nchi ya kisasa yenye maisha ya kiulaya.

Anasema ataamua na watu wenye mtazamo mmoja, ndoto zinazofanana na kuingia kwenye siasa na kutokea ndani kufanya mabadiliko.

Bondia huyo mwenye elimu ya udaktari kwa kusomea ambapo ana masta yake  ambayo alichukua baada ya kupata elimu ya juu ua utabibu wa binadamu.

King Class Mawe alivyomnyuka mpinzani wake Dar

Bondia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Hassani Bandani wakati wa mpambano wao usio na ubingwa uliofanyika katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala Dar es salaam King Class Mawe alishina kwa pointi mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi 


Bonia Ibrahimu Class 'King Class Mawe' kulia akimshambulia kwa makonde Hassani Bandani wakati wa mchezo wao usio na ubingwa uliofanyika katika ukumbi wa panandi panandi King Class Mawe alibuka na ushindi wa point mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi
Ibrahimu Class akioneshwa mshindi baada ya mpambano kumalizika mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi 
KING CLASS MAWE AKIWA NA MMOJA YA MASHABIKI WAKE BAADA YA KUSHUKA ULINGONI
KING CLASS MAWE KWENYE POZI
Bondia Chalo Issa kulia akipambana na Amour Mzungu wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa panandi panandi ilala bungoni Mzungu alishinda kwa pointi mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi 
Bondia Shabani Kaoneka kulia akioneshana umairi wa kutupiana makonde na Halid Makwega wakati wa mpambano wao uliofanyika jumamosi katika ukumbi wa panandi panandi Kaoneka alishinda kwa pointi mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi 

Bondia Shabani Kaoneka kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na Halidi Makwega wakati wa mpambano wao Kaoneka alishinda mpambano huo mpambano uho uliofanyika siku ya jumamosi 
REFARII AKIMUONESHA MKONO JUU BONDIA SHABANI KAONEKA BAADA YA KUMDUNDA HALIDI MAKWEGA KWA POINT WAKATI WA MPAMBANO ULIOFANYIKA KATIKA UKUMBI WA PANANDI PANANDI ILALA BUNGONI DAR ES SALAAAM

Jamal Malinzi amrithi Tenga TFF, ambwaga Myamlani

KATIBU Mkuu wa zamani wa Yanga, Jamal Emil Malinzi, usiku wa kuamkia leo ameshinda Urais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akimrithi uongozi Leodger Tenga baada ya kupata kura 72, dhidi ya 52 za mpinzani wake Athumani Jumanne Nyamlani.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa NSSF Water Front, Dar es Salaam, Walace Karia alifanikiwa kushinda nafasi ya Makamu wa Rais kwa kupata kura 67 akiwashinda Nassib Ramadhani kura 52 na Imani Madega sita.
1_3cebe.jpg
Raia anayemaliza muda wake, Leogder Tenga aliwa na Rais Mpya Mteule, Jamal Malinzi
Kwenye kinyang'anyiro hicho upande wa nafasi za Ujumbe; Kanda ya 13 ilienda kwa kiungo wa zamani wa Simba Wilfred Kidau aliyepata kura 60 na kuwashinda Muhsin Said kura 50, Omar Abdulkadir kura 10 na Alex Kabuzelia kura nne.
Kanda 12; Khalid Mohamed Abdallah amepata kura 69 na kumshinda Davis Mosha aliyepata kura 54.

Kanda ya 11 Geoffrey Nyange 'Kaburu' amepata kura 78 na kuwashinda Riziki Majala kura tano, Twahir Njoki kura mbili, Juma Pinto kura 26 na Farid Mbaraka kura 14, Kanda ya 10 ameshinda Hussein Mwamba aliyepata kura 63, huku Charles Komba akipata nne na Stewart Nasima 58.
Kanda ya tisa Othman Kambi aliyepata kura 84 yeye amewashinda Francis Bulame kura 30, wakati James
Mhagama aliyepata 93 amemshinda Zafarani Damoda aliyepata kura 11 na Kanda ya nane, Ngube Kiondo amepata kura 73 amemshinda Ayoub Nyaulingo kura 52.

Kanda ya Tano, Ahmed Iddi Mgoyi aliyepata kura 92 amemshinda Yussuf Kitumbo aliyepata kura 34, wakati Kanda Omar Walii Ali amepata kura 53 dhidi ya 19 za Ally Mtumwa. Eley Mbise amepata kura 51 dhidi ya 53 kura 57 za Lamanda Swai.
Mbasha Matutu aliyepata kura 63, amembwaga Vesastis Ligano aliyepata kura 61, wakati Vedastus Lufano aliyepata kura 51, amewashinda Jumbe Odesa Magati kura 11, Mugisha Galibona kura 24 na Samuel Nyalla kura 39 na Kanda namba moja, Karilo Samson hakuwa na mpizani akapita moja kwa moja.