STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, December 31, 2014

AC Milan yaitoa nishai Real Madrid Umangani

Ronaldo na El Shaarawy wakichuana
Beki wa Madrid Nacho akimdhiobiti mchezaji wa AC Milan
Karim Benzema akifunga bao la pili la Madrid kwa mkwaju wa penati
MSHAMBULIAJI Stephan El Shaarawy aliiwezesha timu yake ya AC Milan ya Italia kupata ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Mabingwa wa Ulaya, Real Madrid ya Hispania katika pambano la kimataifa la kirafiki lililochezwa mjini Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu.
El Shaarawy alifunga mabao mawili katika kipigo hicho kilichokuwa cha kwanza kwa vijana wa Carlo Ancelotti tangu Septemba na kuhitimisha 'ubabe' wa Madrid ambao walikuwa hawajapoteza mchezo wowote katika mechi 22 katika msimu huu.
Jeremy Menez wa Milan ndiye aliyeanza kufungua milango baada ya kufunga bao la kuongoza katika dakika ya 24 kabla ya El Shaarawy kuongeza goli la pili katika dakika 31 kwa shuti kali.
Dakika nne baadaye Madrid walifanikiwa kuchomoa bao moja kupitia kwa Mwanasoka Bora Duniani, Cristiano Ronaldo kufunga akiwa ndani ya 'boksi' akimtungua kipa  Diego Lopez na kuzifanya timu ziende mapumziko Milan wakiwa mbele kwa mabao 2-1.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kushuhudiwa Milan wakiongeza bao la tatu dakika ya 49 kupitia tena kwa El Shaarawy kabla ya watokea benchi Giampaolo Pazzini na M'Baye Niang kushirikiana vyema na na Pazzini kuukwamisha mpira kimiani katika dakika ya 73 kuaindikia Milan bao la nne.
Real Madrid ilijipatia bao la pili la kujifutia machozi kupitia mshambuliaji wake wa Kifaransa Karim Benzema, aliyefunga bao kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 84.
Kwa ushindi huo AC Milan walikabidhiwa kombe lililopokewa na nahodha wake, Riccardo Montolivo.

KIPUTE CHA MAPINDUZI KUANZA KESHO, RATIBA HII HAPA

Kikosi cha Simba kitakachoanza kibarua cha Mapinduzi Cup dhidi ya Mtibwa Sugar usiku wa kesho
Mtibwa Sugar watakaivaa Simba kesho usiku katika Mapinduzi Cup
Yanga X1
Yanga safari hii imekubali kushiriki kamili gado
MSIMU mpya wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi unatarajiwa kuanza rasmi kesho kwa michezo mitatu 'Mnyama' Simba akitarajiwa kushuka dimbani Usiku kuvaana na Mtibwa Sugar, huku Azam wakitarajiwa kuvaama na KCCA ya Uganda Ijumaa.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa ni kwamba kesho mechi ya kwanza itawakutanisha JKU na Mafunzo majira ya saa 9 alasiri kabla ya Polisi-ZNZ kuvaana na Shaba jioni.
Yanga ambayo imekuwa 'ikisumbua' ushiriki wake katika michuano hiyo safari hii imekubali kikamilifu kushiriki na wenyewe wataanza kibarua Jumamosi kwa kuvaana na Sports Club Villa ya Uganda.
Jumla ya makundi matatu yamegawanywa yakiwa na timu nne kila moja nayo ni;
Kundi A:  SC VILLA,  YANGA, POLISI,  SHABA.
Kundi B: KCCA,  AZAM,  KMKM na MTENDE.
Kundi C: SIMBA, MTIBWA, JKU, na MAFUNZO.
RATIBA KAMILI YA MAPINDUZI CUP IKO HIVI:
Alhamisi 1 Januari 2015:
Saa 9:00  JKU vs MAFUNZO.
Saa.11:00.  POLISI VS SHABA.
Saa 2:15.    SIMBA VS MTIBWA.

Ijumaa 2 Jan 2015 
Jioni saa 10:00  KMKM VS MTENDE              KUNDI        B
Usiku Saa 2:00 KCC VS AZAM.                        KUNDI       B

Jumamosi 3Jan 2015.
Jioni Saa 10:00 JKU VS MTIBWA                  KUNDI       C
Usiku Saa 2:00 YANGA VS SC.VILLA             KUNDI      A

Jumapili  4 Jan 2015                           
Jioni saa 9:00 KCC VS MTENDE                        KUNDI    B
Jioni saa 11:00 KMK VS AZAM.                          KUNDI    B 
Usiku saa 2:15. MAFUNZO VS SIMBA                KUNDI    C 

Jumatatu 5 Jan 2015                     
Jioni saa 10;00 SC VILLA VS SHABA               KUNDI    A
Usiku saa 2:00 YANGA VS POLISI                     KUNDI    A

Jumanne 6 Jan 2015
Jioni saa 9:00 AZAM VS MTENDE                   KUNDI     B
Jioni saa 11: 00  MTIBWA VS MAFUNZO        KUNDI     C 
Usiku saa 2:15. SIMBA VS JKU                           KUNDI    C

Jumatano 7 Jan 2015
Jioni saa 9;00  POLISI VS SC VILLA                KUNDI      A 
Jioni saa 11:00  KCC VS KMKM                         KUNDI     B
Usiku saa 2:15. YANGA VS SHABA                  KUNDI      A

Alhamisin 8 Jan 2015.
Jioni saa 10:00  WINNER B VS RUNNERS  A.
Usiku saa 2:00 WINNER  A VS BEST LOOSER 1

Ijumaa 9 Jan 2015
Jioni saa 11:00 WINNER C VS BEST LOOSER 2
Usiku saa 2;00 RUNNERS  B VS RUNNERS C.

Jumapili 11 Jan 2015.
SEMIFINAL 1 
Jioni saa 10:00. WINNER 1 VS WINNER 2
SEMIFANAL 2
Usiku saa 2:00  WINNER  3 VS WINNER 4
 Tarehe 13/1/2015 itakuwa fainali ya michuano hiyo itakayofanyika usiku katika uwanja wa amaan Zanzibar. kuhitimisha michuano hiyo.

Newz Alert! Mtuhumiwa wa Dawa za Kulevya apigwa risasi akitoroka


MTUHUMIWA wa kesi ya Dawa za Kulevya, anayedaiwa kuwa ni  raia wa Sierra Leone amepigwa risasi na kufariki katika harakati zake za kutaka kutoroka katika Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Inadaiwa mtuhumiwa huyo Abdul Koroma alikuwa akitaka kuwaacha kwenye mataa askari Magereza kwa kuruka uzio kabla ya kuwahiwa kwa kupigwa risasi.
I

Bw' Misosi akifa hataki promo videoni

MSANII Joseph Rushahu 'Bwana Misosi' anajiandaa kurekodi video ya wimbo wake mpya uitwao 'Nikifa Sitaki Promo' ambao ameimba akishirikiana na waimbaji nyota wa muziki wa dansi Ramadhan Masanja 'Banzastone' na Athanas Montanabe wa  bendi ya Wana Extra.
Akizungumza kwa njia ya simu akiwa jijini Tanga alipoenda kwa mapumziko ya Sikukuu ya Mwaka Mpya, Misosi aliyetamba na nyimbo kama 'Nitoke Vipi', 'Mungu Yupo Bize' na 'Watoto wa Kitanga', alisema video ya wimbo huo alioutengenezwa katika studio za Plexity Records chini ya mtayarishaji aitwaye Zest inaanza kurekodiwa wiki ijayo akirejea jijini Dar es Salaam.
Misosi alisema alikwama kuitengeneza mapema video hiyo kutokana na pilikapilika za Krismasi na kuwepo nje ya jiji kwa waimbaji walioshirikiana kuutengeneza wimbo huo.
"Kwa sasa nipo Tanga na ninatarajiwa kurejea mwishoni mwa wiki ili kujipanga kuanza kutengeneza video ya wimbo wangu mpya," alisema.
Msanii huiyo alidokeza kuwa, mara baada ya kukamilika kurekodiwa kwa video hiyo ataiachia pamoja na 'audio' yake na alisema itakuwa ndani ya mwezi huu wa Januari.
"Haiwezi kuvuka mwezi huu kabla ya kazi hiyo mpya kutoka hadharani, nataka kuuanza mwaka nikiwa Misosi mpya," alisema.