STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, December 31, 2014

Bw' Misosi akifa hataki promo videoni

MSANII Joseph Rushahu 'Bwana Misosi' anajiandaa kurekodi video ya wimbo wake mpya uitwao 'Nikifa Sitaki Promo' ambao ameimba akishirikiana na waimbaji nyota wa muziki wa dansi Ramadhan Masanja 'Banzastone' na Athanas Montanabe wa  bendi ya Wana Extra.
Akizungumza kwa njia ya simu akiwa jijini Tanga alipoenda kwa mapumziko ya Sikukuu ya Mwaka Mpya, Misosi aliyetamba na nyimbo kama 'Nitoke Vipi', 'Mungu Yupo Bize' na 'Watoto wa Kitanga', alisema video ya wimbo huo alioutengenezwa katika studio za Plexity Records chini ya mtayarishaji aitwaye Zest inaanza kurekodiwa wiki ijayo akirejea jijini Dar es Salaam.
Misosi alisema alikwama kuitengeneza mapema video hiyo kutokana na pilikapilika za Krismasi na kuwepo nje ya jiji kwa waimbaji walioshirikiana kuutengeneza wimbo huo.
"Kwa sasa nipo Tanga na ninatarajiwa kurejea mwishoni mwa wiki ili kujipanga kuanza kutengeneza video ya wimbo wangu mpya," alisema.
Msanii huiyo alidokeza kuwa, mara baada ya kukamilika kurekodiwa kwa video hiyo ataiachia pamoja na 'audio' yake na alisema itakuwa ndani ya mwezi huu wa Januari.
"Haiwezi kuvuka mwezi huu kabla ya kazi hiyo mpya kutoka hadharani, nataka kuuanza mwaka nikiwa Misosi mpya," alisema.

No comments:

Post a Comment