STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, August 12, 2013

Sheikh Ponda chini ya Ulinzi mkali wa Polisi, MOI

Kiongozi wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania Sheikh Ponda Issa Ponda akiwa amelazwa kwenye chumba maalumu katika taasisi ya mifupa Muhimbili (MOI), muda mfupi baada ya kufikishwa hospitalini hapojana. Picha na Venance Nestory.


KATIBU wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda yupo chini ya ulinzi huku akitibiwa majeraha katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Sheikh Ponda alisafirishwa usiku wa manane kutoka Morogoro baada ya juzi kupigwa na kitu kinachodaiwa kuwa ni mtutu wa bomu saa 12:25 jioni alipokuwa akisind
ikizwa na wafuasi wake kwenda katika Msikiti wa Mungu Mmoja Dini Moja mara baada ya kumaliza kutoa mhadhara katika kongamano mjini hapo.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kongamano hilo, Sheikh Idd Mussa Msema, alidai kuwa Sheikh Ponda alipigwa risasi tatu begani.
Taarifa kutoka ndani ya familia ya Ponda zilisema kwamba baada ya kupata taarifa za kupigwa risasi, baadhi ya masheikh walifunga safari kwenda Morogoro na kumrejesha Dar es Salaam usiku huo huo. Kabla ya kurudishwa Dar es Salaam, imeelezwa kuwa Sheikh Ponda alipelekwa katika Zahanati ya Islamic Foundation.
Mmoja wa wanafamilia alidokeza kwamba Sheikh Ponda alifichwa na alikuwa chini ya ulinzi mkali wa wafuasi wake na hakuna aliyeruhusiwa kumsogelea.
Muhimbili
Hata hivyo, habari zilizopatikana baadaye jana zilisema kuwa alifikishwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
Sheikh Ponda alifikishwa Muhimbili jana saa 7:18 mchana na alipelekwa kwenye chumba cha wagonjwa wa dharura na baadaye alitolewa na kupelekwa kwenye chumba cha x-ray kwa ajili ya vipimo. Baadaye alipelekwa chumba cha upasuaji.
Eneo kubwa la hospitali hiyo lilikuwa na idadi kubwa ya askari na mmoja wa askari waliokuwa doria hospitalini hapo alisema walitawanywa kwenye hospitali mbalimbali za Dar es Salaam baada ya kupata taarifa kuwa angeletwa kwa matibabu.
“Nakuambia tuko hapa tangu saa kumi na moja asubuhi, tumetawanywa hospitali mbalimbali baada ya kupata taarifa kuwa analetwa Dar. Bahati nzuri kaletwa hapa Muhimbili... tunasubiri apate matibabu na tutamtia mbaroni,” alisema askari huyo.
Taarifa ya polisi
Msemaji wa Polisi, Advera Senso alisema jana katika taarifa yake kuwa Sheikh Ponda yuko Hospitali ya Muhimbili akitibiwa baada ya kupata majeraha yaliyotokana na purukushani na polisi wakati wafuasi wake walipokuwa wanataka kumtorosha. 
 
MWANANCHI.

Njemba yafia gesti ikifanya mapenzi na demu wake


MFANYABIASHARA wa sokoni Kariakoo jijini Dar ambaye pia ni mkazi wa Kigogo Flesh, Hamad Kiponda (46), amefia nyumba ya kulala wageni akiwa na mpenzi wake Latifa Saidi (25).
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi alisema tukio hilo lilitokea juzi saa saba mchana katika nyumba hiyo iitwayo Sansiro iliyoko Kiwalani kwa Gude.

Alisema kuwa kutokana na tukio hilo, Latifa alitoa taarifa polisi kwamba mpenzi wake aliishiwa na nguvu ghafla na kuanza kutokwa povu mdomoni wakati wakifanya mapenzi.

Minangi alieleza kuwa mtoa taarifa huyo aliomba msaada kwa wahudumu wa gesti hiyo, lakini Kiponda alifariki papo hapo kabla ya kupelekwa hospitali.

Chanzo cha kifo chake bado hakijafahamika, wakati mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi huku Latifa akishikiliwa kwa kuhojiwa.

Wakati huo huo, moto umezuka ghafla katika nyumba ya Matiku Nestori (43) mkazi wa Tuamoyo Kigamboni, yenye vyumba sita na kuteketeza vyumba vinne pamoja na mali zote zilizokuwemo ndani ambazo bado thamani yake haijajulikana.
Kwa mujibu wa Kamanda Minangi tukio hilo lilitokea juzi saa nane mchana na chanzo cha moto huo inasadikiwa ni hitilafu ya umeme iliyosababisha moto kuanzia kwenye nguzo.

Tanzania One 

Papii Catalogue sasa aamua kuwatetea wanawake

Catalogue akizungumza kueleza
RAPA mahiri wa bendi ya Extra Bongo, Pappy Catalogue ameibuka na wimbo mpya unawaotetea wanawake dhidi ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji kutoka kwa wanaume uliotarajiwa kutambulishwa rasmi kwa mashabiki wakati wa Idd.
Catalogue aliutaja wimbo huo ni  'Mwanamke Hapigwi' ambao una mashairi unaohimiza wanaume kuacha kutumia ubabe kwa wanawake kama kuwapiga, kuwanyanyasa na kuwaona hawana maana kwa sababu wanawake wanahitaji kutunzwa na kubembelezwa na kama kupigwa basi hupigwa kwa upande wa khanga.
Rapa na muimbaji huyo alisema wimbo huo ameutunga maalum katika kuwapigania wanawake katika zama hizi za matukio ya unyanyasaji dhidi yao hasa majumbani na katika mapenzi.
Catalogue alisema wanaume wamekuwa na desturi ya kuwapiga na kuwanyanyasa wanawake na wapenzi wao na ikitokea wanawake hao wakachoka na kuamua kuwakimbia kwa wanaume wengine wanaojua kuibembeleza wanaume wa awali huona kama wameonewa na kuanzisha songombingo.
"Huu ni wimbo maalum kwa ajili ya kutetea wanawake ni utatambulishwa sambamba na rapu mpya iitwayo 'Utaishije mjini bila ya kazi'," alisema.
Katika hatua nyingine dansa kiongozi wa bendi hiyo, Hassain Mussa 'Super Nyamwela' ametamba kuwa ujio wa wanenguaji wawili wapya kutoka Kongo, Jolie Kindu 'Mrisho Ngassa' na Grace Kamba 'John Bocco' kutazidi kuipaisha bendi yao huku akiwapiga vijembe wapinzani wao kuwa wataishia 'kukopi na kupesti'.
Nyamwela alisema ukali walionao madansa hao wa kike utaiweka kileleni Extra Bongo na kuthibitisha kuwa wao siku zote ni wa kwanza katika safu ya unenguaji kwa sababu wapo chini ya mwalimu asiyechuja (yaani yeye Nyamwela).

Kocha Liver amuwakia Suarez, amtaka aombe radhi

Kocha wa Liverpool

KOCHA wa Liverpool, Brendan Rodgers amemweleza mshambuliaji Luis Suarez kwamba ni lazima aombe radhi kwa kutaka kulazimisha kuihama klabu hiyo.
Suarez (26) amekuwa akifanya mazoezi peke yake baada ya kutaka kulazimisha kuhama Anfield katika kipindi hiki cha usajili.
"Kwanza anapaswa kuomba radhi kwa wachezaji wenzake na klabu," alisema Rodgers alipoulizwa kwamba nini kinachofuata anachopaswa kufanya mshambuliaji huyo.
Ofa mbili za Arsenal zikimekataliwa na Liverpool kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa Uruguay.
"Nimemuona kwa muda. Najua huyu si Luis Suarez tunayemfahamu na ni kazi yangu kuwalinda mashabiki na wachezaji kwa sababu wanastahili zaidi ya hilo," aliongeza Rodgers.
Kocha huyo wa Liverpool alikuwa akizungumza baada ya timu yake kula kipigo, bila ya Suarez, cha goli 1-0 dhidi ya Celtic katika mechi yao ya mwisho ya ya kirafiki ya kujiandaa na msimu juzi.
"Amekuwa kwa siku kadhaa akifanya mazoezi peke yake," alisema Rodgers, ambaye atamkosa Suarez wiki hii kwa vile anasafiri na timu yake ya taifa ya Uruguay kwenda kucheza mechi ya kirafiki nchini Japan wiki hii.
"Atakaporejea kutoka katika mechi ya kimataifa tunamuangalia kuanzia hapo."
Pigo la karibuni zaidi katika matumaini ya Suarez' ya kuondoka Anfield lilikuja siku moja tu baada ya Rodgers kumtaka akubali kwamba hatauzwa, pale mmiliki wa Liverpool, John Henry aliposema kwamba nyota huyo hatauzwa kwa pesa yoyote kwa klabu yoyote hata nje ya Uingereza.
Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger, ameendelea kusema kwamba bado wanamhitaji mchezaji huyo huku ripoti zikisema kwamba klabu hiyo ya London inapanga kumfanya Suarez kuwa ndiye mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi klabuni hapo kwa kumpa mshahara wa paundi 160,000 kwa wiki endapo atajiunga nao.
(Sunday Mirror)