STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Monday, August 12, 2013

Papii Catalogue sasa aamua kuwatetea wanawake

Catalogue akizungumza kueleza
RAPA mahiri wa bendi ya Extra Bongo, Pappy Catalogue ameibuka na wimbo mpya unawaotetea wanawake dhidi ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji kutoka kwa wanaume uliotarajiwa kutambulishwa rasmi kwa mashabiki wakati wa Idd.
Catalogue aliutaja wimbo huo ni  'Mwanamke Hapigwi' ambao una mashairi unaohimiza wanaume kuacha kutumia ubabe kwa wanawake kama kuwapiga, kuwanyanyasa na kuwaona hawana maana kwa sababu wanawake wanahitaji kutunzwa na kubembelezwa na kama kupigwa basi hupigwa kwa upande wa khanga.
Rapa na muimbaji huyo alisema wimbo huo ameutunga maalum katika kuwapigania wanawake katika zama hizi za matukio ya unyanyasaji dhidi yao hasa majumbani na katika mapenzi.
Catalogue alisema wanaume wamekuwa na desturi ya kuwapiga na kuwanyanyasa wanawake na wapenzi wao na ikitokea wanawake hao wakachoka na kuamua kuwakimbia kwa wanaume wengine wanaojua kuibembeleza wanaume wa awali huona kama wameonewa na kuanzisha songombingo.
"Huu ni wimbo maalum kwa ajili ya kutetea wanawake ni utatambulishwa sambamba na rapu mpya iitwayo 'Utaishije mjini bila ya kazi'," alisema.
Katika hatua nyingine dansa kiongozi wa bendi hiyo, Hassain Mussa 'Super Nyamwela' ametamba kuwa ujio wa wanenguaji wawili wapya kutoka Kongo, Jolie Kindu 'Mrisho Ngassa' na Grace Kamba 'John Bocco' kutazidi kuipaisha bendi yao huku akiwapiga vijembe wapinzani wao kuwa wataishia 'kukopi na kupesti'.
Nyamwela alisema ukali walionao madansa hao wa kike utaiweka kileleni Extra Bongo na kuthibitisha kuwa wao siku zote ni wa kwanza katika safu ya unenguaji kwa sababu wapo chini ya mwalimu asiyechuja (yaani yeye Nyamwela).

No comments:

Post a Comment