STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, December 22, 2013

Mbunge wa Kigamboni katika Jogging

Jua lile literemke mamaaa aiyaa iyaaa iaayyaa mmaaaaamaaa! Ni kama Mbunge wa KIgamboni Faustine Ndugulile akiwaongoza baadhi ya wapiga kura wake na wanamichezo wengine katika Jogging iliyofanika leo Mbagala
Na Moshi Lusonzo
MBUNGE wa jimbo la Kigamboni, jijini Dar es Salaam, Dk. Faustine Ndugulile,amewataka vijana kujikita kwenye michezo michezo mbalimbali kama sehemu ya ajira pamoja na kujenga afya zao.
Akizungumza wakati wa maadhimisho ya mwaka mmoja wa Klabu ya mchezo wa mbio za pole (Jogging) ya Mbagala, Dk. Ndgulile, alisema endapo vijana hao watabadilika kimtazamo, yeye binafsi atajitolea kuwasaidia ili kuinuka kiuchumi.

Alisema wakati vijana kugeuza vikundi hivyo kuwa sehemu ya kufanyia uhuni na vitendo viovu umekwisha, badala yake watumie nafasi hiyo kujielemisha na kuibua mawazo yatayopelekea miradi ya kimaendeleo.

"Nawapongeza wanachama wa Mbagala Jogging kwa kufikisha muda wa mwaka mmoja mpo pamoja, lakini nawasihi kwa muda huu muanze kufikiria ndani ya kikundi mtafanya nini kwa ajili ya maendeleo yenu," Alisema

Dk. Ndugulile, aliahidi kusaidia kikundi hicho jezi kwa ajili ya mazoezi  pamoja na mtaji wa mradi wowote watakaopendekeza.

Akisoma risala, Kiongozi wa kikundi hicho, Time Saidi, alisema Kikundi hicho chenye vijana 116 kimefanikiwa kuwaweka pamoja vijana na kuwaepusha na tabia ya matumizi ya madawa ya kulevya.

 

TFF yapata katibu mkuu wake mpya kumtangaza J4

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF)  limepata Katibu Mkuu Mpya atakayechukua nafasi iliyoachwa wazi na Angetile Osiah aliyemaliza muda wake na kukaimiwa na Afisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura.
Taarifa toka ndani ya TFF zinasema kuwa jina la mmoja kati ya waliotuma maombi ya kuiomba kazi hiyo amepatikana ila atatangazwa rasmi siku ya Jumanne.
Huyo atakuwa katibu mkuu wa kwanza katika uongozi mpya wa Rais Jamal Malinzi aliyechaguliwa Oktoba 27 mwaka huu katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika jijini Dar es Salaam. Je aliyekinyakua ajira hiyo TFF ni nani?" Tusubiri hapa hapa MICHARAZO itawaletea jina mapema kabla ya hiyo Jumanne.

Manji awatuliza wanayanga kipigo cha Simba

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhig58rdwrAIR7WJXYxbZcwgXIL4ceT8XntMecNNVYbBBiOwVTfYFBL_uSL0TxZS6fG7nexCjkLsXj9_-Nk0SnvLEBfMP-Zuxk9JicU281LVRwy4bJmq0qynTL-B_5MchbjXcDh7zp1yf9r/s640/3.jpg
Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji akiwa na makamu wake, Clement Sanga katika moja ya mikutano yake na wanahabari
MWENYEKITI wa Yanga Bw.Yusuf Manji akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu, kushoto ni makamu mwenyekiti Clement Sanga.
Mwenyekiti wa klabu ya Young Africans Bw. Yusuf Manji amewaomba wanachama, wapenzi na washabiki wasivunjike moyo kwa matokeo ya jana ya mchezo wa kirafiki dhidi ya ya Simba SC, mechi iliyochezwa katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya klabu ya Yanga makutano ya mitaa wa Twiga/Jangwani Manji amesema anajua wanachama, na wapenzi wameumia sana hakuna aliyefurahishwa na matokeo ya kufungwa mabao 3-1 lakini isiwakatishe tamaa uongozi unafanyia kazi mapungufu yaliyojitokeza.
“Mechi ya jana ilikuwa ni bonanza, ndio maana hapakuwa na timu iliyopata pointi katika mchezo huo zaidi ya kusherehekea, sisi tumepata zawadi ya milion 98 wakati wenzetu Simba SC wamepata milion 1, hivyo zaidi sisi tumeendelea kuimarika kiuchumi zaidi wenzetu wameishia kusherehekea” alisema Manji.
Aidha amesema wachezaji zaidi ya tisa wa Yanga hawajapata muda wa kupumzika tangu mwezi Novemba baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu kwani walijiungana timu za Taifa na wamekua huko kwa takribani mwezi mzima bila kupumzika tofauti na wenzetu Simba SC ambao hawana wachezaji wengi timu ya Taifa.
Manji pia alisema anawapa hongera timu ya Simba SC kwa kushinda bonanza la jana, amesema mchezo wa jana walicheza vizuri hivyo wanastahili pongezi kwa hilo.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya mapungufu yaliyojitokeza katika mchezo wa jana, amesema kamati husika inayafanyia kazi na kwa kuwa yeye anasafiri leo kwenda nje ya nchi  majukumu yote amemkabidhi makamu mwenyekiti Clement Sanga mpaka yeye atakaporejea.
Credits:Youngafricans.co.tz

Adebayor azidi kumuumbua AVB, Spurs ikiishusha Man Utd

Tottenham celebrate
Adebayor (kulia) akipongezwa baada ya kufunga bao jioni ya leo
MASHAMBULIAJI Emmanuel Adebayor ameendelea kumuumbua aliyekuwa kocha wa Tottenham Hotspur, Andre Villa Boas, baada ya jioni hii kufunga mabao mawili yaliyoipa ushindi  wa mabao 3-2 ugenini timu yake dhidi ya wenyeji Southampton.
Adebayor aliyekuwa hapangwi na AVB licha ya ukame wa mabao katika klabu ya Spurs alifunga bao la kusawazisha kipindi cha kwa kwanza na kuongeza bao jingine la ushindi kwa timu yake ambayo kwa sasa inanolewa na kocha mpya Tim Sherwood.
Wenyeji walitangulia kupata bao dakika ya 13 kupitia kwa Adam Lallana kabla ya Adebayor kusawazisha dakika ya 25 na timu kwenda mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
Katika harakati za kuokoa shambulizi lililoelekezwa langoni mwake mchezaji Jos Hooiveld na kuisaidia Spurs kupata bao la pili dakika ya 54 na dakika tano baadaye Rick Lambert aliisawazishia wenyeji bao  kabla ya Adebayor kuongeza la pili dakika ya 64.
Ushindi huo umeifanya Spurs kuiengua Manchester United ambayo jana ilipata ushindi wa mabao 3-2 nyumbanji dhidi ya West Ham United kwa kufikisha pointi 30, mbili zaidi ya mabingwa watetezi hao, huku Southampton ikibaki  na pointi zake 24 katika nafasi ya tisa.
Mechi nyingine ya ligi hiyo inaendelea kwa pambano la Swansea City dhidi ya Everton na kesho Arsena walioporomoshwa hadi nafasi ya tatu itavaana na Chelsea wanaoshika nafasi ya nne katika harakati za kutaka kurejea tena kileleni mwa msimamo unaoongozwa kwa sasa na Liverpool ilipota ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Cardiff City jana.

Manji kumng'oa Brandts Yanga au kujiuzulu yeye kipigo cha Simba?

http://www.wavuti.com/uploads/3/0/7/6/3076464/7586757.jpg
Mwenyekiti ya Yanga, Yusufu Manji

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi7qvvvWZAl1z_NKlELsRWtApvNeE2NjMtLDAsF4AedtMaZffcfNuHMoiZuBJmhp6UeFvchyIa53C-_gxof0gLVdS4AZLt7To7wOHDVNucEeWpysGdx2OX1vXE5YI4CvCfQ4k0vTasIVS4/s640/DSC05063.JPG
Kocha Brandts
MWENYEKITI wa Yanga, Yusuph Manji ameitisha mkutano na wanahabari akitaka akuzungumzia pambano la jana dhidi ya Simba katika mchezo wa Nani Mtani Jembe huku kukiwa na taarifa kwamba kuna mambo mawili anayoweza kutoa maamuzi katika mkutano huo.
Moja ya linaloelezwa atalitangaza ni kumtimua kocha mkuu wa klabu hiyo Ernie Brandts au kubwaga manyanga kutokana na aibu aliyoipata jana uwanjani wakati Yanga ikilala kwa mabao 3-1 mbele ya Simba.
MICHARAZO tunafuatilia kinachoendelea na kuwafahamisha.

Bayern Munich wabeba taji la Dunia

Bayern Munich players celebrate
Mabingwa wa Dunia ngazi ya klabu Bayern Munich wakishangilia ushindi
 MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Ujerumani na Ulaya, Bayern Munich usiku wa jana ulijiongezea taji jingine kwa mwaka 2013 baada ya kuinyoa Raja Casablanca ya Morocco kwa mabao 2-0 katika mchezo wa Fainali za Kombe la Dunia kwa ngazi za klabu.
Bayern Munich iliyoweka historia nchini Ujerumani kutwaa mataji matatu kwa wakati mmoja mwaka huu likiwamo lile la FA ya Ujerumani, ilipata ushindi huo kupitia mabao ya Denta aliyefunga dakika ya 7 kabla ya Thiago Alcantara kuongeza jingine dakika ya 22 na kutosha kutwaa taji hilo la dunia.
Hilo lilikuwa taji la kwanza kwa kocha anayekinoa kikosi hicho Pep Gardiola aliyetua kwa mabingwa hao msimu huu akitokea Barcelona. Hata hivyo hilo ni taji la tatu kwa Pep kwani alishatwaa mara mbili akiwa mabingwa wa Hispania mwaka 2009 na 2011 na kuweka historia ya aina yake kwa ngazi ya makocha.
Katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu timu ya Altetico Mineiro ya Brazili iliyoaibishwa na Raja katika mechi ya nusu fainali ya michuano hio iliyofanyika nchini Morocco, ilipata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya  Guangzhou Evergrande kutoka China, ikishuhudia Ronadinho Gaucho akifunga moja ya mabao hayo.

Ajali nyingine tena! Sita wafa, 15 wajeruhiwa Tanga

Mabaki ya gari lililopata ajali jijini Mwanza

 
MATUKIO ya ajali zinazoondoa roho za wenzetu zinaendelea baada ya watu sita kufariki papo hapo na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa baada ya gari la abiria (daladala) kugongana uso kwa uso na lori la mizigo eneo la Kange mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Tanga, Constantine Massawe, ajali hiyo iliyokea jana katika eneo la karibu na mizani kwa kile kilichoelezwa mwendo kasi na kusababisha vifo vya watu hao waliokuwa ndani ya Toyota Hiace na wengine 13 kujeruhiwa vibaya wanne katika hali mbaya waliokimbizwa hospitali ya mkoa huo wa Tanga.
Ajali hiyo imetokea saa chache baada ya ajali nyingine iliyohusisha mabasi ya Bunda Express na Ally's na daladala kupatwa ajali jijini Mwanza na kusababisha vifo vya watu 10 na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Katika ajali hiyo basi la Ally's lililoganga na daladala na kusababisha vifo vya watu saba papo hapo na wawili kufia wakikimbizwa hospitalini kwa matibabu na basi la Bunda kusababisha kifo cha mtu mmoja.
MICHARAZO inawapa pole wote waliokumbwa na ajali na misiba itokanayo na ajali hizo na kuwakumbusha madereva wawe makini wawapo barabarani ili kuepusha matukio ya ajali hizo zinazosababisha vifo na vilema vya kudumu na kuwaacha yatima na wajane bila sababu.

Aliyetabiri Mei 21 mwisho wa dunia aanza yeye kufariki

http://images.smh.com.au/2011/05/23/2379088/art-endoftheworld2-420x0.jpg
Mchungaji Hanold Camping enzi za uhai wake

http://www.jewishjournal.com/images/bloggers_auto/blog_judgement_truck_wiki_3912-584.jpg

http://larrydixon.files.wordpress.com/2011/04/judgment-day-may-21.jpg
Bango lililokuwa likisisitiza kuwa ifikapo Mei 21, 2011 mwisho wa dunia

YULE mchungaji, mtunzi na mmiliki wa redio ya Kikristo aliyeleta kizaazaa kwa baadhi ya waumini wake duniani kwa kutangaza kwamba Mei 21, 2011 ingekuwa mwisho wa dunia, Hanold Camping, amefariki wiki iliyopita bila mwenyewe kushuhudia siku hiyo ya mwisho kama alivyowahi kutabiria.
Camping alifariki Desemba 15, 2013 yaani wiki iliyopita tu akiwa na miaka 92 kutokana na kuanguka akiwa nyumbani kwake kabla ya hapo alikuwa akisumbuliwa na kiharusi.
Ingawa kifo chake kimekuwa kimyakimya, lakini ni kwamba Camping anakumbukwa kwa jinsi alivyotabiri KIAMA kutokea Mei 21 na kubandika mabando makubwa katika maeneo mbalimbali duniani ikiwamo Tanzania kupitia kituo chake cha radio cha Family Radio Network.
Baada ya utabiri wake wa Mei kutotokea alisema tukio hilo lingejiri Oktoba 21, 2011 na hakuna kitu kama hicho kilicjotokea mpaka mauti yamemkumba na kuwaacha aliowatabiria wakiendelea kudunda kuthibitisha kuwa hakuna anayejua SIKU wala SAA ila MUNGU Mwenyezi Pekee aliyeumba Mbingu na Ardhi na kila kilichopo ndani yake.