STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, December 22, 2013

Ajali nyingine tena! Sita wafa, 15 wajeruhiwa Tanga

Mabaki ya gari lililopata ajali jijini Mwanza

 
MATUKIO ya ajali zinazoondoa roho za wenzetu zinaendelea baada ya watu sita kufariki papo hapo na wengine zaidi ya 10 kujeruhiwa baada ya gari la abiria (daladala) kugongana uso kwa uso na lori la mizigo eneo la Kange mkoani Tanga.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Tanga, Constantine Massawe, ajali hiyo iliyokea jana katika eneo la karibu na mizani kwa kile kilichoelezwa mwendo kasi na kusababisha vifo vya watu hao waliokuwa ndani ya Toyota Hiace na wengine 13 kujeruhiwa vibaya wanne katika hali mbaya waliokimbizwa hospitali ya mkoa huo wa Tanga.
Ajali hiyo imetokea saa chache baada ya ajali nyingine iliyohusisha mabasi ya Bunda Express na Ally's na daladala kupatwa ajali jijini Mwanza na kusababisha vifo vya watu 10 na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Katika ajali hiyo basi la Ally's lililoganga na daladala na kusababisha vifo vya watu saba papo hapo na wawili kufia wakikimbizwa hospitalini kwa matibabu na basi la Bunda kusababisha kifo cha mtu mmoja.
MICHARAZO inawapa pole wote waliokumbwa na ajali na misiba itokanayo na ajali hizo na kuwakumbusha madereva wawe makini wawapo barabarani ili kuepusha matukio ya ajali hizo zinazosababisha vifo na vilema vya kudumu na kuwaacha yatima na wajane bila sababu.

No comments:

Post a Comment