STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, December 22, 2013

Adebayor azidi kumuumbua AVB, Spurs ikiishusha Man Utd

Tottenham celebrate
Adebayor (kulia) akipongezwa baada ya kufunga bao jioni ya leo
MASHAMBULIAJI Emmanuel Adebayor ameendelea kumuumbua aliyekuwa kocha wa Tottenham Hotspur, Andre Villa Boas, baada ya jioni hii kufunga mabao mawili yaliyoipa ushindi  wa mabao 3-2 ugenini timu yake dhidi ya wenyeji Southampton.
Adebayor aliyekuwa hapangwi na AVB licha ya ukame wa mabao katika klabu ya Spurs alifunga bao la kusawazisha kipindi cha kwa kwanza na kuongeza bao jingine la ushindi kwa timu yake ambayo kwa sasa inanolewa na kocha mpya Tim Sherwood.
Wenyeji walitangulia kupata bao dakika ya 13 kupitia kwa Adam Lallana kabla ya Adebayor kusawazisha dakika ya 25 na timu kwenda mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1.
Katika harakati za kuokoa shambulizi lililoelekezwa langoni mwake mchezaji Jos Hooiveld na kuisaidia Spurs kupata bao la pili dakika ya 54 na dakika tano baadaye Rick Lambert aliisawazishia wenyeji bao  kabla ya Adebayor kuongeza la pili dakika ya 64.
Ushindi huo umeifanya Spurs kuiengua Manchester United ambayo jana ilipata ushindi wa mabao 3-2 nyumbanji dhidi ya West Ham United kwa kufikisha pointi 30, mbili zaidi ya mabingwa watetezi hao, huku Southampton ikibaki  na pointi zake 24 katika nafasi ya tisa.
Mechi nyingine ya ligi hiyo inaendelea kwa pambano la Swansea City dhidi ya Everton na kesho Arsena walioporomoshwa hadi nafasi ya tatu itavaana na Chelsea wanaoshika nafasi ya nne katika harakati za kutaka kurejea tena kileleni mwa msimamo unaoongozwa kwa sasa na Liverpool ilipota ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Cardiff City jana.

No comments:

Post a Comment