STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, December 22, 2013

Bayern Munich wabeba taji la Dunia

Bayern Munich players celebrate
Mabingwa wa Dunia ngazi ya klabu Bayern Munich wakishangilia ushindi
 MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Ujerumani na Ulaya, Bayern Munich usiku wa jana ulijiongezea taji jingine kwa mwaka 2013 baada ya kuinyoa Raja Casablanca ya Morocco kwa mabao 2-0 katika mchezo wa Fainali za Kombe la Dunia kwa ngazi za klabu.
Bayern Munich iliyoweka historia nchini Ujerumani kutwaa mataji matatu kwa wakati mmoja mwaka huu likiwamo lile la FA ya Ujerumani, ilipata ushindi huo kupitia mabao ya Denta aliyefunga dakika ya 7 kabla ya Thiago Alcantara kuongeza jingine dakika ya 22 na kutosha kutwaa taji hilo la dunia.
Hilo lilikuwa taji la kwanza kwa kocha anayekinoa kikosi hicho Pep Gardiola aliyetua kwa mabingwa hao msimu huu akitokea Barcelona. Hata hivyo hilo ni taji la tatu kwa Pep kwani alishatwaa mara mbili akiwa mabingwa wa Hispania mwaka 2009 na 2011 na kuweka historia ya aina yake kwa ngazi ya makocha.
Katika mechi ya kusaka mshindi wa tatu timu ya Altetico Mineiro ya Brazili iliyoaibishwa na Raja katika mechi ya nusu fainali ya michuano hio iliyofanyika nchini Morocco, ilipata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya  Guangzhou Evergrande kutoka China, ikishuhudia Ronadinho Gaucho akifunga moja ya mabao hayo.

No comments:

Post a Comment