STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 8, 2013

Javu aendeleza makali, Yanga wakiwagonga Wanigeria Taifa


MSHAMBULIAJI Mpya wa Yanga kutoka Mtibwa Sugar, Husseni Javu ameendelea kuonyesha makali yake baada ya jioni hii kuisaidia Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya 3 Pillars ya Nigeria.
Javu alijiunga hivi karibuni na mabingwa hao wa soka nchini hilo ni bao lake la pili baada ya Jumapili kuisaidia Yanga kuilaza timu yake ya zamani wakati walipoishindilia mabao 3-1 katika mechi ya kimataifa ya kirafiki.
Mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja waTaifa ilishuhudia karibu nyota wote wa Yanga akiwemo Mrisho Ngassa akishuka dimbani.

Ikiwa tumia washambuliaji wake wapya Hussein Javu na Mrisho Ngassa waliojiunga na kikosi msimu huu, Yanga ilikosa nafasi za wazi za kufungua kupitia kwa washambuliaji hao ambao hawakuonekana kuwa makini makini katika umaliziaji wa mipira iliyokuwa ikiwafikia.

David Luhende alikosa bao dakika ya 34 kufuatia mpira alioupiga kuokelewa na mlinda mlango wa 3Pillars FC na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda, huku awali Said Bahanuzi akikosa nafasi pia kama hiyo dakika ya 17 ya mchezo.

Hussein Javu aliipatia Young Africans bao kwanza dakika ya 40 ya mchezo kwa ustadi akiitumia vizuri nafasi hiyo aliyopewa na kuingo Athuman Idd 'Chuji' aliyewazidi ujanja walinzi wa 3Pillars FC na kumpasia Javu aliyeukwamisha mpira wavuni na kuhesabu bao kwa watoto wa Jangwani.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans -0 3Pillars FC.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ambapo Yanga iliwaingiza Didier Kavumbagu, Kelvin Yondani, Oscar Joshua, na Salum Telela kuchukua nafasi za Nadir Haroub, Jerson Tegete, Juma Abdul na Said Bahanuzi mabadiliko ambayo yaliongeza kasi ya mchezo.

David Luhende ambaye leo alikuwa mwiba kwa timu ya 3Pillars FC nusura aipatie Yanga bao la pili lakini mpira alioupiga ulikokolewa na walinzi wa timu hiyo ya Nigeria na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Yanga iliendelea kulishambulia lango la 3Pillars dakika zote za mchezo lakini kutokua makini kwa mshambuliaji Didier Kavumbagu na Hussein Javu kuliendelea kuufanya ubao wa mabao uendelee kusomeka 1-0.

Mpaka dakika 90 za mwamuzi Oden Mbaga zinamalizika, Young Africans 1-0 3Pillars FC .

Kesho kikosi cha Yanga hakitakua na mazoezi na wachezaji wote watakua na mapumziko kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid na waterejea tena mazoezini siku ya jumamosi asubuhi katika uwanja wa Loyola kuendelea kujifua na maandalizi ya Ligi Kuu.

Young Africans: 1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Juma Abdul/Salum Telela, 3.David Luhende, 4.Nadir Haroub 'Cannavaro'/Kelvin Yondani, 5.Rajab Zahir, 6.Athuman Idd 'Chuji/Issa Ngao, 7.Said Bahanuzi/Abdallah Mguhi 'Messi'/Shaban Kondo, 8.Haruna Niyonzima/Bakari Masoud, 9.Jerson Tegete/Didier kavumbagu, 10.Hussein Javu, 11.Mrisho Ngassa

Maskin Mhadhiri huyo wa UDSM auwawa kwa risasi DarPicture: Patrick Rweyongeza

Mhadhiri wa College of Engeneering katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, UDSM, Patrick Rweyongeza, ameuawa jana kwa kupigwa na risasi.

Tukio limetokea jana mchana katika maeneo Magomeni-TANESCO wakati marehemu akielekea mjini ambapo watu waliokuwa wamepakizana kwenye pikipiki walimfuata na kumfyatulia risasi na kisha kutokomea.

Inatisha! Tindikali zahamia kwa wageni

RAIA wawili wa kigeni kutoka katika nchi ya Uingereza ambao wanafanya kazi ya kujitolea katika upande wa ualimu  wamemwagiwa tindi kali mjini Zanzibar jana jioni katika mitaa ya Shangani Mji Mkongwe  visiwani Zanzibar.
Habari kutoka katika chanzo chetu cha habari  kinasema Jeshi la Polisi Zanzibar limeanza msako na kuwatafuta watu waliofanya kitendo hicho dhidi ya walimu hao wa kike waliofika Zanzibar kwa kujitolea kufundisha walitambulika kwa majina ya Kate Gee (18) na Kirsiwer Trup (18) na walikuwa na wiki mbili tu.
Walimu hao waliokutwa na janga hilo walikuwa wanafanya kazi katika shule  moja ya msingi inayojulikana kama Mtakatifu Monika iliyopo chini ya kanisa la Aglicana. habari tulizozipata hivi punde  Raia hao hivi sasa wamehamishiwa katika Hospitali ya Aghakani jijini Dar es salaam kwa matibabu zaid tutazidi kuwaleta habari zaidi.
Tukio hilo limetokea wakati hakuna taarifa zozote za matukio ya nyuma ya kumwagiwa watu tindikali visiwani humo akiwamo Katibu wa Mufti visiwani humo na yale yanayotokea Tanzania Bara maeno ya Dar na Arusha hivi karibuni.

Tanzania yazidi kuporomoka FIFA


VIPIGO vinne mfululizo ilivyopata timu ya taifa 'Taifa Stars' imezidi kuiporomosha Tanzania katika orodha ya viwango vya soka duniani ambapo orodha mpya iliyotolewa inaoonyesha ipo nafasi ya 128 toka 121 kwa mwezi uliopita.
Moja wa timu ilizozikwanyua Tanzania katika mbio za kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia, Ivory Coast yenyewe nayo imeporomoka kwa nafasi tano kutoka namba 13 iliyokuwa katika orodha iliyopita hadi kwenye nafasi ya 18 japo inaendelea kutamba barani Afrika ikishika nafasi ya 1.
 ikifuatiwa na Ghana ambao wamesalia nafasi yao ya 24 duniani.
Nchi za Cape Verde imeendelea kupanda chati safari hii kwa nafasi 13 duniani ikikamata namba 36 toka 49 za mwezi uliopita huku barani Afrika ikishika nafasi ya 6 toka ya nane iliyokamata orodha ya awali, huku Cameroon iliyoonekana kuyumba akwa siku za karibu ikipanda kwa nafasi 20 ikishika nafasi ya 51 toka 71 ya awali na Afrika ikishika nafasi ya 8.
Orodha ya jumla ya dunia kwa nafasi za 12 Bora zimesalia kama zilivyo kwa Hispania kuendelea kuongoza ikifuatiwa na Ujerumani, kisha Colombia, Argentina, Uholanzi,  Italia, Ureno, Croatia, Brazili na Belgium, kisha Ugiriki na kumalizwa na Uruguay, huku Marekani wakirejea tena kwwenye Top 20 ya Dunia safari hii.
Orodha kamili mpya ya FIFA unaweza kuipata katika:FIFA World Ranking

Hivi ndivyo Extra Bongo ilivyowatambulisha wanenguaji wao wapya Leaders

Wanenguaji wapya wa Extra Bongo, Jolie na Grace wakionyesha makeke yao

Tunatomboka namuna hii ...ayaa ayaaa hiiiiii
Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki (mwenye kofia) akiwatambulisha wanenguaji wao wao huku Super Nyamwela akiwa makini kumsikiliza pembeni kulia. Kushoto ni Papii Catalogue
Mi naitwa Jolie Kindu au Muringo Ngassa nimekuya Kutanzanie kwa ajili ya kufunika madancers wote mutaona
Msiniangushe jamani, nimeshawafagilia kwa mapaparazi kuwa nyie ni nouma sawasawaaa?
Ally Choki akitoa ufafanuzi kwa wanahabari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa waneguaji wao wawili kutoka Kongo.
Choki alikuwa na kazi kubwa ya kufafanua baadhi ya mambo juu ya madansa hao wanaojiita Mrisho Ngassa na John Bocco ambao watatambuilishwa rasmi kesho kwenye onyesho la Idd Mosi Meeda Club bna Idd Pili itakuwa zamu wa wakazi wa Mbagala kwani Extra Bongo watakuwa Dar Live

Mwanafunzi wa darasa la kwanza afa kwa kugongwa na gari Mbeya

 [ DIWANI ATHUMANI  - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.


WILAYA YA  KYELA - AJALI YA  GARI KUMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU NA        
                                            KUSABABISHA KIFO.
MNAMO TAREHE 07.08.2013 MAJIRA YA  SAA 08:30 HRS HUKO KATIKA ENEO LA KALUMBULU  WILAYA YA  KYELA  MKOA WA MBEYA. GARI  T.932 BUF AINA YA  T/IPSUM IKIENDESHWA NA KAIMU S/O HENDE, MIAKA 33, MBONDEI, MKULIMA  MKAZI WA KYELA-KATI  ILIMGONGA MTEMBEA KWA MIGUU MTOTO HAWA D/O GIBSON,MIAKA 6,MSAFWA,MWANAFUNZI DARASA LA KWANZA S/MSINGI MBUGANI  MKAZI KALUMBULU NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO.  MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA YA KYELA. CHANZO NI MWENDO KASI, DEREVA AMEKAMATWA. TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI. KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
Signed by:
 [ DIWANI ATHUMANI  - ACP ]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

Huyu ndiye jambazi wa kwenye ATM, lanaswa kilaini Dar baada ya mtego

Mtu anayedaiwa kuwa mwizi wa kwenye ATM rais wa Bulgaria akiwa chini ya ulinzi baada ya kunaswa akiiba jijini Dar es Salaam kutokana na kuwekewa mtego kumnasa


MSAKO wa wezi wa kwenye Mashine za Kutolea Fedha (ATM), umeanza kuzaa matunda baada ya raia wa Bulgaria kukamatwa akiiba kwenye ATM ya Bank of Africa (BOA), Tawi la Afrikana, Kinondoni, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa za benki, mtuhumiwa huyo ambaye
hakutajwa jina lake alikamatwa baada ya kamera maalumu zilizowekwa kwenye ATM za BOA, kumtambua kuwa ni mwizi sugu wa benki hiyo anayetafutwa.

Mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo ambaye hakupenda kutajwa jina kwa kuwa si msemaji, alisema tukio hilo lilitokea jana saa 12 asubuhi baada ya mtuhumiwa huyo kuwekewa mitambo maalumu ya kumnasa.

Alisema benki hiyo ilipelekewa malalamiko na baadhi ya wateja kwamba wakienda kutoa fedha kwenye ATM wanakuta akaunti zao hazina salio wakati wanaamini zilikuwa na fedha.

Chanzo hicho cha habari kilidai kuwa baada ya kupelekewa malalamiko hayo, waliweka mitambo maalumu ya kuwawezesha walinzi wa maeneo ya ATM za BOA kumbaini mtu atakayetoa fedha kwa njia ya wizi.

“Kama Benki tuliweka mtambo maalumu na mtuhumiwa huyo alionekana kwenye mtambo wetu, hivyo tuliwaagiza walinzi wetu watakapomwona mtu huyo wamkamate haraka 
sana,”alisema.
Alisema mtuhumiwa huyo alianza mchezo huo kwa muda mrefu ambapo kwa kutumia kadi za ATM zisizojulikana idadi yake, alikuwa anakwenda kwenye ATM mbalimbali za benki hiyo na kutoa fedha hadi Sh10 milioni.

Kuhusu tukio la jana, mmoja wa walinzi wa BOA aliyejitambulisha kwa jina moja la Frank alisema mtuhumiwa huyo alipofika kwenye ATM hiyo aliingia na kuchukua fedha ambazo alizipeleka kwenye gari lake.
Frank alisema baada ya kupeleka fedha hizo, alirudi kwa mara ya pili ili achukue fedha nyingine ndipo walinzi hao walimkamata na kumfunga pingu.

“Huyu mtuhumiwa mwenye asili ya Kiarabu alifika na gari lake saa 12 asubuhi, aliingia kwenye ATM na kutoa fedha ambazo hazikujulikana ni shilingi ngapi na kuzipeleka kwenye gari lake, baadaye alirejea tena kwa ajili ya kutoa fedha zingine, wakati anaingia ndipo alipokamatwa na mlinzi aliyekuwa analinda hapo,” alisema Frank.

Kamanda wa Polisi Kinondoni, Camilius Wambura alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi hilo huku uchunguzi dhidi yake ukiendelea.

“Ni kweli taarifa nimezipata, mtuhumiwa amekamatwa, bado hatujajua ni kiasi gani ambacho ameiba kwa kutumia mtandao, tunaendelea na uchunguzi,” alisema Wambura.

Tukio kama hili lilishawahi kutokea mkoani Mwanza Februari 19 mwaka huu na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na maofisa ya Benki ya NMB liliwatia mbaroni watu watatu ambao walidaiwa kuiba kiasi cha Sh700 milioni kwa nyakati tofauti.

MWANANCHI

Real Madrid yaichakaza Chelsea 3-1, Mourinho

KIUNGO Frank Lampard alicheza kwa mara ya kwanza majira haya ya joto, lakini alishindwa kumzuia Cristiano Ronaldo kuinyanyasa Chelsea jana.
Kabla ya mechi hiyo na Real Madrid mjini Miami, kiungo huyo mkongwe alikosa mechi zote za kujiandaa na msimu za klabu, Stamford Bridge kutokana na kuwa majeruhi.
Lakini Lampard ameimarika na kuanza kazi tayari kwa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Hull City, Agosti 18 baada ya kumaliza dakika 45 za kwanza katika Fainali ya Mabingwa wa Kimataifa wa Guinness.
Katika mechi hiyo, mabao mawili ya Ronaldo na moja Marcelo, yalitosha kuitotesha timu ya Jose Mourinho 3-1 dhidi ya timu yake ya zamani ambayo kwa sasa inafundishwa na Carlo Ancelotii.
Chelsea ilipata bao lake pekee kupitia kwa Ramires.  
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Arbeloa, Pepe, Ramos, Marcelo, Modric, Khedira, Isco, Ozil, Ronaldo na Benzema.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Terry, Cahill, Cole, Lampard, Van Ginkel, Ramires, Oscar, Hazard na Lukaku.
On target: Cristiano Ronaldo scored a brace as Chelsea went down to the La Liga giants
Kiboko yao: Cristiano Ronaldo amefunga mabao mawili dhidi ya Chelsea jana
Party time: Real Madrid stars celebrate with the International Champions Cup after beating Chelsea
Kujiachia: Nyota wa Real Madrid wakisherehekea na taji lao la Mabingwa wa Kimataifa wa Guinness
Lethal: Ronaldo blasted home a free-kick and later added a header to help Madrid secure the game
Kitu hichoo: Ronaldo akifunga kwa mpira wa adhabu
Unloved: A Real Madrid fan holds up a banner showing he doesn't care that Mourinho left the club
Mapenzi yameisha: Shabiki la Real Madrid likiwa limebeba bango kuonyesha kutojali kuondoka kwa Mourinho katika klabu hiyo
Chinwag: Mourinho and former Chelsea boss, and current Madrid manager, Carlo Ancelotti, have a chat
Mazungumzo baada ya tukio: Mourinho na kocha wa zamani wa Chelsea, ambaye kwa sasa ni kocha wa Madrid, Carlo Ancelotti wakizungumza baada ya mechi
Triumphant: Real Madrid stars celebrate after beating Chelsea in the final of the Champions Cup
Mabingwa: Nyota wa Real Madrid wakisherehekea kuifunga Chelsea katika fainali ya Mabingwa wa Kimataifa wa Guinness.
 BI ZUBEIRY BLOG

Answar Sunnah wala Eid yao leo sawa wa wengine duniani


WAISLAM WA AN-SUNA WAMEJUMUIKA  NA WAISLAM WENZAO DUNIANI KUSHEREHEKEA SIKU  HIYO BAADA YA KUMALIZIKA KWA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANIPICHA WAKIWA KATIKA VIWANJA VYA JANGWANI LEO

WAKISALI KWENYE VIWANJA VYA JANGWANI LEO

Waumini wa Kiislam wakisujudu wakati wa swala ya Eid iliyoswaliwa leo na sehemu kubwa ya waumini duniani wanaofuata kalenda ya Kiislam