STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, August 8, 2013

Javu aendeleza makali, Yanga wakiwagonga Wanigeria Taifa


MSHAMBULIAJI Mpya wa Yanga kutoka Mtibwa Sugar, Husseni Javu ameendelea kuonyesha makali yake baada ya jioni hii kuisaidia Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya 3 Pillars ya Nigeria.
Javu alijiunga hivi karibuni na mabingwa hao wa soka nchini hilo ni bao lake la pili baada ya Jumapili kuisaidia Yanga kuilaza timu yake ya zamani wakati walipoishindilia mabao 3-1 katika mechi ya kimataifa ya kirafiki.
Mechi hiyo iliyochezwa kwenye uwanja waTaifa ilishuhudia karibu nyota wote wa Yanga akiwemo Mrisho Ngassa akishuka dimbani.

Ikiwa tumia washambuliaji wake wapya Hussein Javu na Mrisho Ngassa waliojiunga na kikosi msimu huu, Yanga ilikosa nafasi za wazi za kufungua kupitia kwa washambuliaji hao ambao hawakuonekana kuwa makini makini katika umaliziaji wa mipira iliyokuwa ikiwafikia.

David Luhende alikosa bao dakika ya 34 kufuatia mpira alioupiga kuokelewa na mlinda mlango wa 3Pillars FC na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda, huku awali Said Bahanuzi akikosa nafasi pia kama hiyo dakika ya 17 ya mchezo.

Hussein Javu aliipatia Young Africans bao kwanza dakika ya 40 ya mchezo kwa ustadi akiitumia vizuri nafasi hiyo aliyopewa na kuingo Athuman Idd 'Chuji' aliyewazidi ujanja walinzi wa 3Pillars FC na kumpasia Javu aliyeukwamisha mpira wavuni na kuhesabu bao kwa watoto wa Jangwani.

Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans -0 3Pillars FC.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko ambapo Yanga iliwaingiza Didier Kavumbagu, Kelvin Yondani, Oscar Joshua, na Salum Telela kuchukua nafasi za Nadir Haroub, Jerson Tegete, Juma Abdul na Said Bahanuzi mabadiliko ambayo yaliongeza kasi ya mchezo.

David Luhende ambaye leo alikuwa mwiba kwa timu ya 3Pillars FC nusura aipatie Yanga bao la pili lakini mpira alioupiga ulikokolewa na walinzi wa timu hiyo ya Nigeria na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Yanga iliendelea kulishambulia lango la 3Pillars dakika zote za mchezo lakini kutokua makini kwa mshambuliaji Didier Kavumbagu na Hussein Javu kuliendelea kuufanya ubao wa mabao uendelee kusomeka 1-0.

Mpaka dakika 90 za mwamuzi Oden Mbaga zinamalizika, Young Africans 1-0 3Pillars FC .

Kesho kikosi cha Yanga hakitakua na mazoezi na wachezaji wote watakua na mapumziko kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Eid na waterejea tena mazoezini siku ya jumamosi asubuhi katika uwanja wa Loyola kuendelea kujifua na maandalizi ya Ligi Kuu.

Young Africans: 1.Ally Mustapha 'Barthez', 2.Juma Abdul/Salum Telela, 3.David Luhende, 4.Nadir Haroub 'Cannavaro'/Kelvin Yondani, 5.Rajab Zahir, 6.Athuman Idd 'Chuji/Issa Ngao, 7.Said Bahanuzi/Abdallah Mguhi 'Messi'/Shaban Kondo, 8.Haruna Niyonzima/Bakari Masoud, 9.Jerson Tegete/Didier kavumbagu, 10.Hussein Javu, 11.Mrisho Ngassa

No comments:

Post a Comment