KIUNGO Frank Lampard alicheza kwa mara
ya kwanza majira haya ya joto, lakini alishindwa kumzuia Cristiano
Ronaldo kuinyanyasa Chelsea jana.
Kabla ya mechi hiyo na Real Madrid mjini
Miami, kiungo huyo mkongwe alikosa mechi zote za kujiandaa na msimu za
klabu, Stamford Bridge kutokana na kuwa majeruhi.
Lakini Lampard ameimarika na kuanza kazi
tayari kwa mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu dhidi ya Hull City, Agosti 18
baada ya kumaliza dakika 45 za kwanza katika Fainali ya Mabingwa wa
Kimataifa wa Guinness.
Katika mechi hiyo, mabao mawili ya
Ronaldo na moja Marcelo, yalitosha kuitotesha timu ya Jose Mourinho 3-1
dhidi ya timu yake ya zamani ambayo kwa sasa inafundishwa na Carlo
Ancelotii.
Chelsea ilipata bao lake pekee kupitia kwa Ramires.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Arbeloa, Pepe, Ramos, Marcelo, Modric, Khedira, Isco, Ozil, Ronaldo na Benzema.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Terry, Cahill, Cole, Lampard, Van Ginkel, Ramires, Oscar, Hazard na Lukaku.

Kiboko yao: Cristiano Ronaldo amefunga mabao mawili dhidi ya Chelsea jana

Kujiachia: Nyota wa Real Madrid wakisherehekea na taji lao la Mabingwa wa Kimataifa wa Guinness

Kitu hichoo: Ronaldo akifunga kwa mpira wa adhabu

Mapenzi yameisha: Shabiki la Real Madrid likiwa limebeba bango kuonyesha kutojali kuondoka kwa Mourinho katika klabu hiyo

Mazungumzo baada ya tukio: Mourinho na
kocha wa zamani wa Chelsea, ambaye kwa sasa ni kocha wa Madrid, Carlo
Ancelotti wakizungumza baada ya mechi

Mabingwa: Nyota wa Real Madrid
wakisherehekea kuifunga Chelsea katika fainali ya Mabingwa wa Kimataifa
wa Guinness.
BI ZUBEIRY BLOG
No comments:
Post a Comment