STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, July 3, 2013

Kesi dhidi ya maafisa wa Chadema yatupiliwa mbali

Mwita Waitara

KWA mara nyingine Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Singida, ilitupilia mbali kesi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) iliyokuwa ikiwakabili, Mwita Waitara, Afisa sera na utafiti Makao Makuu na Mshauri wa Chama hicho Dk Kitila Mkumbo,

Kesi hiyo ilitupiliwa mbali baada ya Mashahidi wa Serikali kushindwa kuthibitisha aina ya matusi yaliyodaiwa kutolewa na washitakiwa, waliyomtukana Naibu Katibu Mkuu, Mwigulu Mchemba, yaliyodaiwa kutolewa na Washitakiwa.

Sababu nyingine ya kutupilia mbali kesi hiyo ilielezwa kuwa ni upande wa serikali walishindwa kumleta shahidi muhimu katika kesi hiyo Nchemba, aliyedaiwa kutukanwa ili athibitishe kwamba yeye ndiye aliyetukanwa na namna ambavyo matusi hayo yalimuathiri.

“Washatakiwa hawana kesi ya kujibu kwa kuwa mashahidi wa serikali wameshindwa kuthibitisha aina ya matusi yaliyodaiwa kutolewa na washtakiwa”.alisema Masham Hakimu wa Mahakama hiyo.

“Upande wa serikali walishindwa kumleta shahidi muhimu katika kesi hiyo Mwigulu Nchemba aliyedaiwa kutukanwa ili athibitishe kwamba yeye ndiye aliyetukanwa na namna ambavyo matusi hayo yamemuathiri”.alisema Hakimu.

Alisema, Kushindwa kwa Nchemba kufika mahakamani ni kuonyesha kwamba ama hajui kwamba alitukanwa au hakuona kosa lolote alilotendewa na hivyo Mahakama haiwezi kutoa uamuzi kwa mambo ya kuhisiwa, alisema hakimu huyo.

Awali Washtakiwa hao, walidaiwa kutenda kosa hilo Julai 14, mwaka jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Ndago wilayani Iramba, ambapo Chadema kilikuwa na mkutano wa hadhara.

Wakati ikisomwa hukumu hiyo, alikuwepo Wakili wa Washitakiwa, Tundu Lisu, ambapo Hakimu Masham alisema washatakiwa hawana kesi ya kujibu kwa kuwa mashahidi wa serikali walishindwa kuthibitisha aina ya matusi yaliyodaiwa kutolewa na washitakiwa.

Kesi hiyo ambayo imekuwa ikisuasua mara nyingi kwa upande wa serikali kushindwa kuleta mashahidi mahakamani na kusababisha kesi hiyo kuahirishwa mara kwa mara, iliibua minong’ono jambo ambalo imedaiwa lilikuwa likimkera Hakimu wa kesi hiyo.

Wadau wa mambo ya kisheria wamekuwa wakihoji maswali mengi yasiyokuwa na majibu kwamba, inakuwaje baadhi ya viongozi wa Chama tawala wanawashaiwishi watu kufungua kesi zenye maslahi yao binfasi halafu siku ya kesi hawafiki? Je ni njia ya kuwasumbua watu au ni kuwapuuza Mahakimu?

Wengi wao wamekuwa wakiwatafsiri kuwa wanafanya hivyo wakijua wao ni chama tawala hivyo wanafanya ili kuwakomoa na kuwapa usumbufu wanaotuhumiwa kwa maana ya kuwafanya wazibe midomo ya kuwatetea wananchi?

Mwananchi ambaye alikuwepo mahakamani hapo na yeye akiwa na kesi alisema, anawashauri mahakimu wakate kudharauliwa na Viongozi wa Sampuli hizo, amabo wanawashikiza watu wafungue kesi kwa kulinda heshima zao, halafu wahusika hawafiki mahakani.

Amedai, kwanza kitendo hicho kinawadharirisha wananchi ambao wanabebwa kama debe tupu likisubiri hewa liwekwe kitu, ambapo wahusika wanaoona kesi zinawaendea kombo wanajificha na hivyo kuwaacha wao kama chama wakiadhrika.

Mama ambaye alikuwa mahakani hapo akiwa na kesi ya Miradhi alisema, tabia inayofanywa na viongozi hao, inachezea muda na fedha ambayo ni kodi ya wananchi, lakini akadai badala ya Mahakimu hao kufanya kazi ya kusikiliza kesi za wananchi zenye msingi wa kuwasaidia, wanapoteza muda kwa mambo yasiyo na maana.

Aidha Mwanaharakati aliyeomba asitajwe alisema, baadhi ya Viongozi na Watanzania wasipofuta mawazo ya kufanywa watumwa Punda au Ng’ombe, baadhi ya wanasisa watawachezea hivyo wasikubali kuwafanya vihongwe, huo wao wakijificha kwenye mapambano mfano kesi hizo.

Kuelekea Usiku wa Matumaini; Wabunge, Wasanii, Mabondia watambiana




Mratibu wa Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013, Abdallah Mrisho 'Abby Cool' (katikati), akiongea na wanahabari leo kuhusu burudani zitakazokuwepo siku hiyo.
Mbunge wa Nzega, Dk Hamis Kigwangala (katikati), akielezea jinsi timu yake ya Simba (wabunge) watakavyoigaragaza Yanga katika mechi yao.
Mbunge wa Igalula, Dkt. Athumani R. Mfutakamba (wa kwanza kushoto), akiwawakilisha wabunge wa Yanga katika mkutano huo.
Mwanamuziki 'Diamond Platnumz' akieleza jinsi atakavyomfunika msanii Prezzo kutoka Kenya.
Afisa Masoko kutoka kampuni ya simu za mkononi Tigo ambao ni mmoja wa wadhamini wa Tamasha hilo, Alex Msigala akiongea na wanahabari jinsi kampuni yake ilivyojipanga kufanikisha Usiku wa Matumaini 2013.
Meneja Uhamasishaji Rasilimali kutoka TEA, Doreen Shekibula (katikati), akipongeza waandaaji wa Tamasha hilo.
Jacob Steven (JB) akionyesha jinsi atakavyomwinua Mhe. Idd Azzan katika mpambano wao wa ndondi.
Msanii Ray Kigosi (katikati) akijinadi kuwa atamvunja taya Mhe. Zitto Kabwe siku hiyo.
Mwakilishi wa Bongo Fleva, H-Baba akielezea jinsi timu yake itakavyotoa kichapo kwa wapinzani wao wa Bongo Muvi.
Jacqueline Wolper (katikati) akimtumia salamu Mhe. Halima Mdee kuhusu kichapo atakachomshushia siku hiyo.
...Akionyesha jinsi alivyojipanga kumchapa Mdee.
Mbunge wa Kinondoni, Idd Azzan akielezea alivyo fiti kumkabili JB.
Bondia Thomas Mashali akitoa tambo zake kuwa atampa kichapo Patrick Amote kutoka Kenya.
Bondia Francis Miyeyusho akiwaeleza wanahabari alivyo tayari kumkabili bondia Shadrack Muchanje kutoka Kenya.
Meneja wa Msondo Ngoma, Said Kibiriti akiongea na wanahabari (hawapo pichani) jinsi bendi yake itakavyowafunika wapinzani wao Sikinde.
Kiongozi wa Bendi ya Sikinde, Habib Abbas 'Jeffa' naye akielezea jinsi bendi yake itakavyofanya makamuzi siku hiyo.
Sehemu ya wanahabari waliohudhuria mkutano huo.
Diamond Platnumz (kushoto) akiwa katika pozi na H-Baba baada ya mkutano huo.
---
Baadhi ya wasanii, wabunge na wanamasumbwi watakaoshiriki katika Tamasha la Usiku wa Matumaini 2013, leo walikusanyika katika mkutano wao na wanahabari uliofanyika katika Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza jijini Dar na kuelezea jinsi walivyojipanga kuelekea katika tamasha hilo kubwa ambalo litafanyika Julai 7, mwaka huu katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika tamasha hilo, wabunge wa Simba na wale wa Yanga watashuka dimbani kucheza soka huku baadhi yao wakishiriki katika mapambano ya ndondi dhidi ya waigizaji. Kwenye eneo la ndondi, Mhe. Halima Mdee atapigana na Jacqueline Wolper, Mhe. Zitto Kabwe na Vincent Kigosi ‘Ray’, Mhe. Ester Bulaya atavaana na Aunt Ezekiel huku balaa zaidi likitarajia kuandikwa na mabondia Patrick Amote (Mkenya) atakayevaana na Thomas Mashali (Mtanzania) huku Mkenya Shadrack Muchanje akipigana na Francis Miyeyusho (Mtanzania). Burudani nyingine zitakazokuwepo siku hiyo ni wakali wa muziki, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Prezzo, ambao watashindana katika jukwaa moja ili kutafuta nani mkali zaidi. Bendi za Msondo Ngoma, Mlimani Park ‘Sikinde’ na Jahazi zitawaburudisha mashabiki wao. Vilevile, burudani nyingine itatoka kwa wakali wa Temeke, Wanaume Family na Halisi, wataokata mapanga Taifa kwa staili zao za kuvutia. Soka la kukata na shoka kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva litahakikisha linawapa raha mashabiki wa wasanii watakaoingia uwanjani siku hiyo.

GPL

Dida aanza mazoezi Yanga, timu kuondoka Ijumaa kwenda Kanda ya Ziwa


 Mlinda Mlango Deogratius Mushi 'Dida' akifanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Yanga, Loyola Sekondari hii leo.
  Na Baraka Kizuguto
KIPA mpya aliyesajiliwa na mabingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yanga SC, Deogratius Munishi 'Dida' pamoja beki wa kati aliyesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro, Rajab Zahir leo wameanza rasmi mazoezi na timu yao Uwanja wa sekondari ya Loyola, Mabibo, Dar es Salaam.
Deogratius Munishi 'Dida' ameungana na wachezaji wengine wawili mshambuliaji Shaban Kondo aliyekua akicheza soka nchini Msumbiji pamoja na Zahir aliyerejea kutoka nchini Afrika Kusini alipokuwa akifanya majaribio katika timu mbili za Ligi Kuu nchini humo.
Mapema jana katika siku ya kwanza ya mazoezi kiungo mshambuliiaji Mrisho Khalfan Ngassa alifanya mazoezi asubuhi chini ya kocha mholanzi Ernest Brandts kabla ya kocha huyo kuwapa nafasi wachezaji wote wa timu ya taifa, Taifa Stars kujiunga na timu hiyo leo kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya Uganda julai 13 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Hadi sasa klabu ya Yanga imefanikiwa kusajili wachezaji watano wapya ambao ni Dida kutoka Azam, Zahir wa Mtibwa, Ngassa wa Simba, Shaban Kondo aliyekuwa Msumbiji na Realitus Lusajo kutoka Machava FC.
Kocha Brandts amefurahia kuongezeka kwa wachezaji hao kwani amesema atapata fursa ya kukaa nao na kucheza michezo ya kirafiki kanda ya ziwa hali itakayopelekea kupata nafasi ya nzuri kukiandaa kikosi na msimu mpya wa 2013/2014.
Yanga itaendelea na mazoezi kesho asubuhi Loyola ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ziara yake Kanda Ziwa inayotazamiwa kuanza mwishoni mwa wiki jijini Mwanza.

Wachezaji wote wameendelea na mazoezi leo asubuhi isipokua wachezaji waliojiunga na kambi ya timu ya Taifa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Uganda.

Hivi ndivyo alivyo Ray C kwa sasa baada ya kupona


 Mwanamuziki staa wa bongo fleva Rehema Chalamila a.k.a Ray C amepotea katika anga ya muziki kwa kipindi kirefu kutokana na matatizo ya matumizi ya madawa ya kulevya na baada ya kupata tiba sasa mambo yanaonekana kurudi katika hali yake ya kawaida.
Pamoja na ukimya wake katika muziki, Ray C a.k.a kiuno bila mfupa sasa anaonekana kuwa active zaidi katika mitandao ya kijamii hususan Instagram. Ray C ameshare baadhi ya picha na fans wake kupitia instagram ambazo kwa namna moja au nyingine zinaongea zenyewe (kwa kusindikizwa na captions) juu ya maisha yake ya sasa. Kwa ufupi ni kuwa Rehema anakula bata tu sasa hivi, thanks kwa shavu alilopewa na Rais Jakaya Kikwete ambaye anamuita ‘Daddy’. Take a look….

Hizi ni baadhi ya picha zinazomwonesha yeye mwenyewe alivyo sasa, amenenepa sana!




Mbongo ajinyonga Russia, kisa...!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEilH2P6Saz_jkUSAK4Ocw6yWBnhyLwpFx7JyVkfjWqI4g1IVtdj6OIcHABAGXK0197EGIMkx_i8us2uETfi7IKWX1WAmq01lYL012uHid172kCA9Dw3sg6gvlrwrRYaojg6CsAxtdi79Oc/s640/20130702-130838.jpg
Marehemu Shaaban Japhar enzi za uhai wake
HABARI kutoka kwa baadhi ya Watanzania waishio Saint Petersburg, Urusi, ni kwamba Mtanzania aliyeweka makazi yake mjini hapo kwa muda mrefu Ndg. Shabani Japhari ameaga dunia kwa kujinyonga.
Akituma ujumbe huo kupitia mtandao wake wa Facebook, Ndg. Moses Mango, ambaye pia ni mkazi wa muda mrefu wa Mji huo, alisema ” I hate bringing bad news. Kama wengi mlivyosikia, ndugu yetu Shabani ametutoka leo asubuhi kwa kujinyonga. Kwa sie wote hapa, huu ni mzigo mzito sana aliotuachia. Ningeomba wote tuwe pamoja katika kukamilisha shughuli zote zinazotokana na msiba huu. RIP mrefu", alimalizia kusema Ndg. Mango.
Shabani alifika Urusi miaka ya 80 kama mwanafunzi, na baada ya kuhitimu masomo yake, alibaki mjini Saint Petersburg na kuendelea kujihusisha na masuala mbalimbali ya biashara. Vijana wengi waliokuwa wakifika Urusi ki masomo walimuheshimu na kumchukulia kama kaka, na wengine kumtaka ushauri katika masuala mbalimbali kutokana na uzoefu wake wa Mji.
Marehemu Shabani, ameacha mke na watoto Kandhaa, na dua zetu tunazielekeza kwa familia hiyo, na familia yake nyingine kubwa, iliyopo Tanzania. Kwa hakika wote tumeshtushwa na msiba huu, ambao bado umetuacha na maswali mengi, bila majibu.
 
Bongo Mirror

Mkurugenzi wa NBC atoa somo Mkutano wa Wake wa Marais wa Afrika

Rais Mstaafu wa Marekani, George Bush (kushoto) akiwa na baadhi ya watoa mada katika Mkutano wa Wake wa Marais Afrika, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa VIA Aviation, Susan Mashibe, jijini Dar es Salaam jana. Mkutano huo wa siku mbili ulimalizika jana.  

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Mizinga Melu (wa pili kushoto) akitoa mada kuhusu maendeleo ya wanawake viongozi wakati wa Mkutano wa  Wake wa Marais wa Afrika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kushoto ni Balozi Mark Green Rais na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Global Development (IGD),  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya  Group Loid Engenharia SGPS, Loide Monteiro na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya VIA Aviation, Suzan Mashibe.

Rais wa zamani wa Marekani, George Bush (wa tatu kushoto) akiwa na baadhi ya watoa mada kuhusu maendeleo ya wanawake viongozi wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Wake wa Marais wa Afrika jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Mwelu na (kushoto kwake) ni Mtendaji Mkuu Kampuni VIA Aviation, Susan Mashibe. Wengine ni maofisa wa NBC, kutoka kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Clara Rubambe na kutoka kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu, Flora Lupembe na Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Mwinda Kiula Mfugale.

Rais Mstaafu wa Marekani, George Bush (kulia) akipozi kwa picha na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania , Mizinga Melu wakati wa  Mkutano wa Wake wa Marais Afrika, jijini Dar es Salaam jana. Mizinga alikuwa mmoja wa watoa mada katika mkutano huo

Misri hali ni tete, jeshi ladaiwa kushika madaraka

Rais Mohammed Mosri
HALI imezidi kuwa tete nchini Misri ikielezwa kuwa Jeshi la nchi hiyo kwa sasa linadhibiti madaraka, baada ya muda wa saa 48 alizopewa Rais Mohammed Mosri kutafuta suluhu ya mgogoro ulioibua maandamano ya wiki kadhaa sasa kupita biloa utekelezaji wake.
Kuna taarifa za kutofautiana kuhusu ikiwa jeshi litatoa taarifa punde baada ya muda huo wa masaa 48 aliopewa rais Morsi kutafuta suluhu ya mgogoro huo kutimia.
Jeshi linasemekana tayari kudhibiti jengo la televisheni ya taifa. Maafisa wakuu wa serikali wako kwenye mkutano wa dharura nchini Misri, saa chache kabla ya muda wa mwisho ambao jeshi na upinzani zilimpa rais wa nchi hiyo Mohammed Morsi kusuluhisha mgogoro wa kisiasa unaokumba taifa hilo. Jeshi limesema kuwa litaingilia mzozo unaokumba nchi kwa kutoa mpango wake maalum wa kutatua mgogoro huo, ikiwa pande zote mbili hazitaafikiana. Wafuasi na wapinzani wa rais Morsi wanaanza kujitokeza barabarani kwa maandamano kwa siku ya nne tangu kuanza mwishoni mwa wiki jana. Kwa upande wake RaisMohammed Morsi amesisitiza kwamba yeye ndiye kiongozi halali wa taifa huku maandamano kati ya wapinzani na wafuasi wake yakisababisha vifo zaidi. Kwenye hotuba aliyotoa kwa taifa usiku wa kuamkia leo, Mosri alipinga makataa ya jeshi kutatua mgogoro wa sasa ifikapo Jumanne. Kiongozi huyo amesema hataamrishwa na yeyote na kuwasihi waandamanaji kuweka utulivu. Hata hivyo watu 16 walikufa katika moja wapo ya maandamano ya wafuasi wa Morsi. Awali jeshi lilitoa mpango wa kurejesha taifa katika uthabiti. Stakabathi iliyopatikana na BBC inasema jeshi linapanga kuvunja katiba, kuweka machakato wa uchaguzi mkuu, na kuvunja bunge. Hapo Jumatatu Jeshi lilisema huenda likaingilia kati ikiwa hali haitabadilika. Morsi na wanasiasa walipewa saa 48 kuafikiana.
BBC

TWIGA BANCORP KUTUMIA MAWAKALA KUTOA HUDUMA ZAKE


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp Limited, Hussein Mbululo, akizungumza na waandishi wa Habari kuhusiana na huduma mbalimbali za kibenki zinazopatikana katika katika Banda la Benki hiyo lililopo katika viwanja vya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere barabara ya Kilwa Dar es Salaam.
 Afisa Mtendaji Mkuu wa Twiga Bancorp, Hussein Mbululo (kulia) akizungumza na Wafanyakazi wa Benki hiyo waliopo Viwanja vya Maonesho sabasaba, Ofisa Masoko, Adebert Archerd  na Katikati ni Ofisa Uendeshaji wa shughuli za Kibeki wa Twiga Bancorp, Upendo Tendewa

Yanga kuwafuata KCC-Uganda Ijumaa kucheza nao mara mbili

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiLtb1aNOAjxilGsAf9g1vE5A7S8zZu6jg6rsqeFduotShwhX5ACAGlfu29pKvjqFjNNO3f_bUCBRqyg5CtG601Dt1fW3Ow0l1wIyH1f4Xh0jQA6RQRi9yzgF95K1EJCyKBbhWzXB0VfP8/s640/Y-1.jpg
MABINGWA wa kandanda nchini Yanga inayoendelea kujifua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuondoka keshokutwa kwenda Kanda ya Ziwa kwa ajili ya michezo kadhaa ya kujipima nguvu.
Ziara hiyo ya Yanga katika kanda hiyo inaenda sambamba na kuuonyesha ubingwa wake iliyotwaa mwaka huu kwa kuwapoka watani zao Simba na kwamba ikiwa huko itacheza mechi kadhaa za kirafiki ikiwemo kuvaana mara mbili na KCC ya Uganda.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto, Yanga itaondoka Ijumaa ikiwa na kikosi kamili tayari kwa mapambano hayo yaliyoratibiwa na kampuni ya Nationwide Entertainment Centre ya jijini Mwanza.
Kizuguto alisema pamoja na kwamba ratiba kamili ya mechi zao wakiwa katika ziara hiyo ni vigumu kwake kuainisha lakini anachofahamu kwamba wanaenda kuchjeza mechi zisizopungua tatu  katika miji ya Mwanza, Shinyanga na Tabora.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Nationwide, Frank Pangani alinukuliwa na kituo kimoja cha redio kwamba Yanga itacheza mechi zaidi ya tatu ambapo Jumamosi itaanza kazi kwa kuvaana na KCC kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kabla ya siku ya Jumapili kushuka dimba la CCM Kambarage-Shinyanga kurudiana na Waganda hao.
Pangani alidokeza kuwa Julai 11 Yanga itushuka tena dimbani kuvaana na Mtibwa Sugar baada ya wenyeji Rhino Rangers kushindwa kupatikana kukipiga na Yanga.
Aliongeza Julai 14 pia kutakuwa na mechi nyingine ya Yanga ingawa hajawa na uhakika ni timu gaini itakayocheza nayo na kwamba wanaangalia taratibu za mabingwa hao kutembea mikoa mingine ya kanda hiyo na Magharibi ili kutoa burudani kwa mashabiki ambao kwa muda mrefu wamezikosa kuziona timu kubwa.
Kampuni hiyo mwaka jana iliwapeleka waliokuwa mabingwa Simba katika kanda hiyo na kucheza mechi kadhaa za kujipima ngumu ikiwamo na timu za Toto African katika miji ya Mwanza na Shinyanga kabla ya kutua Dar kuumana na Express ya Uganda.

Tamasha la Raha za Jana na Leo kufanyika Jumamosi

Mratibu wa Tamasha la Raha za Jana na Leo, Kahabi Ng'wendesha akilitambulisha rasmi Tamasha hilo kwa waandishi wa habari jana jijini Dar katika hoteli ya Chichi iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar. Bw. Kahabi alizungumzia namna kampuni ya Yuneda namna ilivyojiandaa kufanikisha tamasha hilo linalosubiriwa kwa hamu na wakazi wa jiji la Dar jumamosi hii katika viwanja vya posta kijitinyama.
Baadhi ya viongozi wa bendi tofauti wakiwa katika mkutano na waandishi wa habari kuthibitisha ni namna gani wamejiandaa naTamasha  hilo linalokutanisha bendi sita za muziki wa dansi nchini Tanzania.Bendi hizo ni Mashujaa,Bantu group,Twanga pepeta,Msondo,Sikinde na king kikii"wazee sugu".
 Mwanamuziki Bichuka(Sikinde) akifafanua namna watakavyoiburuza Msondo Ngoma jukwaani ikiwa ndiyo waasimu wao wa siku nyingi kwa mara nyingine wanakutana jukwaa moja viwanja vya posta.Pia kutakuwa na silent moment kuwakumbuka wanamuziki wote wa mziki wa dansi waliotangulia mbele ya haki nchini Tanzania.
King Kikii(kushoto) akielezea namna alivyojipanga kuteka mashabiki siku ya jumamosi hii katika viwanja vya posta .kulia ni mwanamuziki mkongwe Hamza Kalala.Milango ya uwanja itakuwa wazi kuanzia saa tano asubuhi hadi usiku mnene,Watoto bureeee mpaka saa kumi na mbili,wakubwa Tsh 8,000/= tu mpaka chwee.Michezo ya watoto,nyama choma na vinywaji vyakutosha vitakuwepo.