STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, July 3, 2013

Yanga kuwafuata KCC-Uganda Ijumaa kucheza nao mara mbili

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiLtb1aNOAjxilGsAf9g1vE5A7S8zZu6jg6rsqeFduotShwhX5ACAGlfu29pKvjqFjNNO3f_bUCBRqyg5CtG601Dt1fW3Ow0l1wIyH1f4Xh0jQA6RQRi9yzgF95K1EJCyKBbhWzXB0VfP8/s640/Y-1.jpg
MABINGWA wa kandanda nchini Yanga inayoendelea kujifua jijini Dar es Salaam kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kuondoka keshokutwa kwenda Kanda ya Ziwa kwa ajili ya michezo kadhaa ya kujipima nguvu.
Ziara hiyo ya Yanga katika kanda hiyo inaenda sambamba na kuuonyesha ubingwa wake iliyotwaa mwaka huu kwa kuwapoka watani zao Simba na kwamba ikiwa huko itacheza mechi kadhaa za kirafiki ikiwemo kuvaana mara mbili na KCC ya Uganda.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Yanga, Baraka Kizuguto, Yanga itaondoka Ijumaa ikiwa na kikosi kamili tayari kwa mapambano hayo yaliyoratibiwa na kampuni ya Nationwide Entertainment Centre ya jijini Mwanza.
Kizuguto alisema pamoja na kwamba ratiba kamili ya mechi zao wakiwa katika ziara hiyo ni vigumu kwake kuainisha lakini anachofahamu kwamba wanaenda kuchjeza mechi zisizopungua tatu  katika miji ya Mwanza, Shinyanga na Tabora.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Nationwide, Frank Pangani alinukuliwa na kituo kimoja cha redio kwamba Yanga itacheza mechi zaidi ya tatu ambapo Jumamosi itaanza kazi kwa kuvaana na KCC kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza kabla ya siku ya Jumapili kushuka dimba la CCM Kambarage-Shinyanga kurudiana na Waganda hao.
Pangani alidokeza kuwa Julai 11 Yanga itushuka tena dimbani kuvaana na Mtibwa Sugar baada ya wenyeji Rhino Rangers kushindwa kupatikana kukipiga na Yanga.
Aliongeza Julai 14 pia kutakuwa na mechi nyingine ya Yanga ingawa hajawa na uhakika ni timu gaini itakayocheza nayo na kwamba wanaangalia taratibu za mabingwa hao kutembea mikoa mingine ya kanda hiyo na Magharibi ili kutoa burudani kwa mashabiki ambao kwa muda mrefu wamezikosa kuziona timu kubwa.
Kampuni hiyo mwaka jana iliwapeleka waliokuwa mabingwa Simba katika kanda hiyo na kucheza mechi kadhaa za kujipima ngumu ikiwamo na timu za Toto African katika miji ya Mwanza na Shinyanga kabla ya kutua Dar kuumana na Express ya Uganda.

No comments:

Post a Comment