Marehemu Shaaban Japhar enzi za uhai wake |
Akituma ujumbe huo kupitia mtandao wake wa Facebook, Ndg. Moses Mango,
ambaye pia ni mkazi wa muda mrefu wa Mji huo, alisema ” I hate bringing
bad news. Kama wengi mlivyosikia, ndugu yetu Shabani ametutoka leo
asubuhi kwa kujinyonga. Kwa sie wote hapa, huu ni mzigo mzito sana
aliotuachia. Ningeomba wote tuwe pamoja katika kukamilisha shughuli zote
zinazotokana na msiba huu. RIP mrefu", alimalizia kusema Ndg. Mango.
Shabani alifika Urusi miaka ya 80 kama mwanafunzi, na baada ya kuhitimu
masomo yake, alibaki mjini Saint Petersburg na kuendelea kujihusisha na
masuala mbalimbali ya biashara. Vijana wengi waliokuwa wakifika Urusi ki
masomo walimuheshimu na kumchukulia kama kaka, na wengine kumtaka
ushauri katika masuala mbalimbali kutokana na uzoefu wake wa Mji.
Marehemu Shabani, ameacha mke na watoto Kandhaa, na dua zetu
tunazielekeza kwa familia hiyo, na familia yake nyingine kubwa, iliyopo
Tanzania. Kwa hakika wote tumeshtushwa na msiba huu, ambao bado
umetuacha na maswali mengi, bila majibu.
Bongo Mirror
No comments:
Post a Comment