STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 22, 2013

GOLDEN BUSH USO KWA USO NA CLOUDS FC


Kikosi cha Golden Bush Veterani wakiwa na kocha wao, Madaraka Selemani.

WAKALI wa kutatandaza soka mkoa wa Dar es Salaam, Golden Bush Veterani jioni ya leio inatarajiwa kushuka dimbani kuvaana na kikosi cha kituo maarufu cha redio nchini Cloud's Fm, 'Clouds Fc.
Pambano hilo la kirafiki ambalo linasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka wa jijini kutokana na tambo za pande zote mbili litachezwa kwenye uwanja wa Tanganyika Packers kuanzia saa 10:30 jioni.
Kwa mujibu wa Mlezi wa Golden Bush, Onesmo Waziri 'Ticotico' ni kwamba kikosi chao tangu Jumatatu walikuwa kambini katikati ya jiji wakijiandaa na pambano hilo baada ya kupoteza mechi yao mwishoni mwa wiki dhidi ya Survey ya Chuio Kikuu.
Ticotico alisema katika mechi ya leo wanatarajia kuwashusha dimbani wachezaji wake nyota ili kuhakikisha wanaitoa nishai Clouds, aliodai walikuwa wakiwakwepa mara kwa mara wakiomba nafasi ya kucheza nao.
"Tupo kamili kwa ajili ya kutoa kipigo kwa Clouds, hasa ikizingatiwa wamekuwa wakitukwepa mara nyingi, pia tumetoka kupoteza mechi mwishoni mwa wiki iliyopita, hivyo hatutaki tena tufanye makosa," alisema Ticotico ambaye ametamba atakuwepo dimbani kuwaongioza vijana wake kusaka ushindi.
Baadhi ya nyota wa timu hiyo wanaotarajiwa kushuka dimbani leo ni pamoja na Wisdom Ndhlovu, Herry Morris, Majaliwa, Said Swedi 'Panucci', Shija Katina, Waziri Mahadhi 'Mandieta' na wengineo, huku wapinzani wao wakitarajiwa kuwategemea zaidi akina Shafii Dauda, Mbwiga Mbwiguke, Lwambano, Ally Mayay 'Tembele', Gofrey Lea na wengineo

2 comments:

  1. Nadhani itakuwa bonge la mechi, ila huyo Ticotico anajua kucheza soka au ndiyo mambo ya debe tupu?

    ReplyDelete
  2. Ticotico anajua soka na kuchonga pia ni nouma...nimeshawahi kumuona Chuo Kikuu akisakata kabumbu...ila sijajua kama leo watapona kwa Clouds ya Mbwiga Mbwiguke Mtoto wa Kizaramo kama anaenda...aaah jamaa anazungumza kama kameza kanda...
    Said wa Mwenge

    ReplyDelete