STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, February 22, 2013

TOTTENHAM USO KWA USO NA INTER MILAN

Bale (3) akishangilia moja ya mabao yake katika mechi yao dhidi ya Inter Milan mwaka 2010.
DROO ya kuwania kucheza hatua ya Robo Fainali za Michuano ya Ligi ya UEFA, imetangazwa ambapo wakali wa England Tottenham Hotspur wamejikuta wakipangwa kuchuana na Inter Milan ya Italia waliowahi kukutana katika pambano lililosisimua wengi la Ligi ya Mabingwa msimu wa 2010.
Tottenham inayokamata nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi ya England, ilipata nafasi hiyo baada ya jana kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Olympicque Lyon ya Ufaransa na kushinda jumla ya mabao 3-2 baada ya mechi ya awali ya nyumbani wiki iliyopita kupata ushindi wa mabao 2-1.
Inter wenyewe wamepenya kilaini hatua hiyo baada ya kupata ushindi wa jumla wa mabao 5-0 dhidi ya CFR Cluj na hivyo kukutana na mahasimu wao ambao waliwang;oa kwenye Ligi ya Mabingwa mwaka 2010 kwa jumla ya mabao 6-5.
Katika mechi ya kwanza Tottenham walishinda nyumbani mabao 3-1 kabla ya kunyukwa ugenini 4-3 mabao yote matatu ya Waingereza hao wakifungwa na winga msumbufu, Gareth Bale.
Mechi nyingine za hatua hiyo ya robo fainali itazikutanisha timu za Viktoria Plzeň dhidi ya Fenerbahçe, Benfica itakayoumana na Bordeaux, Anzhi Makachkachla dhidi ya Newcastle United, Stuttgart itavaana na   Lazio, Levante dhidi ya Rubin Kazan, Basel  itakayoumana na Zenit iliyoing;'oa Liverpool licha ya kufungwa jana mabao 3-1, na pambano la mwisho litazikuitanisha waliokuwa Mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Chelsea dhidi ya Steaua Bucurest.
Mechi za mkondo wa kwanza wa hatua hiyo zitachezwa Machi 7 na zile za marudiano zifanyika wiki moja baadaye yaani Machi 14, na zitakazofanya vema zitaingia robo fainali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi za klabu barani Ulaya.

No comments:

Post a Comment