STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Friday, April 4, 2014

Mwalimu achaoa mtoto mboko hadi kumuua

bbcccHii ni taarifa kutoka Kenya ambapo inasemekana Wazazi katika kaunti ya Kirinyaga mkoa wa Kati nchini Kenya wameandamana kwa hasira baada ya mwalimu mmoja kumchapa mtoto mmoja wa shule ya msingi hadi kupoteza maisha.
Mtoto huyo inasemekana alichapwa kichwani na mwalimu na kuzirai na alipokua akipelekwa hospitali alifariki dunia,ambapo wazazi hao wameandamana kwa amani wakitaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.
Polisi nchini Kenya wamemtia mbaroni tayari mwalimu huyo na kwa sasa anashirikiwa na Polisi huku uchunguzi zaidi ukiendelea kufanywa,Mtoto huyo alikuwa katika darasa la saba katika shule ya kibinafsi iitwayo Roka Preparatory.
Wengi wa wazazi wenye watoto wao katika shule hiyo wameahidi kuwahamishia shule nyingine ambapo Nchi ya Kenya iliharamisha kitendo cha kuwachapa wanafunzi wa shule karibu miaka kumi iliyopita na hii ilikuwa baada ya visa vya walimu kuwaadhibu vikali wanafunzi na kuwajeruhi kukithiri.
BBC Swahili

Jaji Warioba aishangaa serikali ya JK

DODOMA
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema waliokuwa wajumbe wa tume hiyo hawajawahi kudai malipo ya pensheni ya Sh200 milioni kama inavyodaiwa.
“Wajumbe wa Tume hawajatoa madai ya kulipwa shilingi milioni mia mbili. Hakuna mjumbe yeyote aliyetoa dai kama hilo na Serikali inajua,” alisema

Jaji Warioba katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, aliyoitoa kupitia Nyalali, Warioba and Mahalu Law Advocates ali ongeza:

“Nimeona taarifa iliyotolewa na Serikali kuhusu Tume ya Mabadiliko, nimeshangazwa na maudhui na lugha iliyotumika,” alisema Warioba akirejea taarifa iliyotolewa na Ikulu juzi ikieleza jinsi tume hiyo ilivyohitimisha kazi zake.

Wiki hii Jaji Warioba alikaririwa akilalamika jinsi yeye na makamishna wake walivyoondolewa ofisini na kunyang’anywa magari kwa haraka bila kusubiri siku waliyopanga kufanya makabidhiano, lakini Ikulu ilimjibu kwamba shughuli za Tume hiyo zilikoma siku ambayo Tume ilivunjwa.

Katika taarifa yake ya jana, Jaji Warioba alisema aliwasilisha Rasimu ya Katiba Machi 18 mwaka huu na Tume ilivunjwa Machi 19 wakati wajumbe wakiwa bado mjini Dodoma.

“Pamoja na lugha ya kejeli inayotumiwa na Serikali kuniita mnafiki, busara ya kawaida ilitakiwa kutumika kufanya maandalizi ya kuwarudisha wajumbe nyumbani na kuandaa makabidhiano,” alisema.

Alisisitiza kuwa Serikali ilikuwa na wajibu wa kuwarejesha makwao wajumbe wa tume hiyo, hata kama muda wa kisheria wa kufanya kazi ulikuwa umepita.

“Niliwasilisha Rasimu Machi 18, 2014. Tume imevunjwa Machi 19, 2014 wakati wajumbe wako Dodoma. Pamoja na lugha ya kejeli iliyotumiwa na Serikali na kuniita mnafiki, busara ya kawaida ingeonyesha umuhimu wa Serikali kujipa muda wa kufanya maandalizi ya kuwarudisha wajumbe nyumbani,” alisema Jaji Warioba na kuongeza:

“Hata kama sheria ilitaja muda wa kuvunja Tume bado ilikuwa ni wajibu Serikali kufanya mipango ya safari ya wajumbe baada ya kumaliza kazi. Sheria haikuizuia Serikali kufanya hilo. 

Huo ni wajibu wa Serikali na utaratibu wa kawaida unaotumiwa na Serikali kwa tume zote inazoziunda. Inaonekana Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliwekewa utaratibu tofauti. Kulikoni?”
MWANANCHI

Barcelona yafungiwa kusajili Ulaya

http://www.smckorea.com/2011/fcbarcelonalaligachamps_580693_92772.jpgKLABU ya Barcelona imefungiwa kusajili wachezaji kwa vipindi viwili vya usajili na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa kukiuka taratibu za kimataifa zinazohusu usajili wa wachezaji chini ya umri wa miaka 18. 
Hatua hiyo imekuja kufuatia uchunguzi wa awali uliofanywa na shirikisho hilo kupitia mfumo wake wa uhamisho-TMS kwa mwaka uliopita. 
Barcelona wamekutwa wamekiuka vifungu kadhaa kuhusiana na uhamisho wa kimataifa sambamba na usajili wa wachezaji walio chini ya umri ambao sio raia wa Hispania. 
Uchunguzi huo ulihusisha wachezaji kadhaa walio chini ya umri huo ambao waliandikishwa na kushiriki mashindano wakiwa na timu hiyo katika kipindi cha mwaka 2009-2013.

Wareno, Juve, Basel zashinda Europa League

http://s2.djyimg.com/n3/eet-content/uploads/2014/04/482339519.jpg
Hekaheka kati ya Juve na Lyon jana Ufaransa
http://s2.djyimg.com/n3/eet-content/uploads/2014/04/482339873.jpg
Porto walipoitoa nishai Sevilla jana kwenye Europa League

http://www.beinsports.tv/di/library/bein_us/84/42/basel-vs-valencia_1qsqz6tdnrifu10v28x9wkvfpa.jpg?t=696372997&w=830&h=466&quality=50&cropTo=top
Basel walipoikongota Valencia 3-0
http://www.uefa.com/MultimediaFiles/Photo/competitions/Comp_Matches/02/08/39/76/2083976_w2.jpg
Tevez akionyechanja mbuga kusaka bao kwa Juventus
BAO lililofungwa na Leonardo Bonucci dakika sita kabla ya pambano kumalizika limeisaidia Juventus kupata ushindi mwembamba ugenini dhidi ya Olympique Lyon ya Ufaransa katika mechi ya robo fainali ya kwanza wa Kombe la Europa League.
Ushindi huo wa ugenini umeifanya Juve kuwa na kazi rahisi kwa mechi yao ya marudiano Alhamis ijayo mjini Turin katika kujihakikisha kutinga nusu fainali ya michuano hiyo.
Katika mechi nyingine za mkondo wa kwanza za robo fainali Basel ya Uswisi iliifumua Valencia ya Hispania mabao 3-0 na kunusa nusu fainali, huku Sevilla ikinyukwa ugenini na Porto ya Ureno na Benfica ikishinda ugenini 1-0 dhidi ya AZ ya Uholanzi.
Mabao ya Basel katika mchezo hio yalifungwa na Matias Delgado aliyefunga mawili dakika ya 34 na 38 na jingine kupitia kwa Valentin Stocker dakika za lala salama.
Timu hizo zitarudiana wiki ijayo kujua timu nne za kucheza nusu fainali ya michuano hiyo ya pili kwa ukubwa kwa ngazi ya klabu barani Ulaya baada ya Ligi ya Mabingwa ambayo nayo ipo hatua ya robo fainali kwa sasa.