KLABU ya Barcelona
imefungiwa kusajili wachezaji kwa vipindi viwili vya usajili na
Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa kukiuka taratibu za kimataifa
zinazohusu usajili wa wachezaji chini ya umri wa miaka 18. Hatua hiyo imekuja kufuatia uchunguzi wa awali uliofanywa na shirikisho hilo kupitia mfumo wake wa uhamisho-TMS kwa mwaka uliopita.
Barcelona wamekutwa wamekiuka vifungu kadhaa kuhusiana na uhamisho wa kimataifa sambamba na usajili wa wachezaji walio chini ya umri ambao sio raia wa Hispania.
Uchunguzi huo ulihusisha wachezaji kadhaa walio chini ya umri huo ambao waliandikishwa na kushiriki mashindano wakiwa na timu hiyo katika kipindi cha mwaka 2009-2013.
No comments:
Post a Comment