Hii
ni taarifa kutoka Kenya ambapo inasemekana Wazazi katika kaunti ya
Kirinyaga mkoa wa Kati nchini Kenya wameandamana kwa hasira baada ya
mwalimu mmoja kumchapa mtoto mmoja wa shule ya msingi hadi kupoteza
maisha.
Mtoto huyo inasemekana alichapwa kichwani na mwalimu na kuzirai na
alipokua akipelekwa hospitali alifariki dunia,ambapo wazazi hao
wameandamana kwa amani wakitaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya mwalimu
huyo.
Polisi nchini Kenya wamemtia mbaroni tayari mwalimu huyo na kwa sasa
anashirikiwa na Polisi huku uchunguzi zaidi ukiendelea kufanywa,Mtoto
huyo alikuwa katika darasa la saba katika shule ya kibinafsi iitwayo
Roka Preparatory.
Wengi wa wazazi wenye watoto wao katika shule hiyo wameahidi
kuwahamishia shule nyingine ambapo Nchi ya Kenya iliharamisha kitendo
cha kuwachapa wanafunzi wa shule karibu miaka kumi iliyopita na hii
ilikuwa baada ya visa vya walimu kuwaadhibu vikali wanafunzi na
kuwajeruhi kukithiri.
BBC Swahili
No comments:
Post a Comment