STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 5, 2014

Uongozi Shule ya Joyland wahimiza kuwawekezea ktk watoto elimu

Shughuli ilianza kwa walimu kujitambulisha mbele ya wazazi na waalikwa
Wazazi na waalikwa walikuwa makini kunasa matukio kwenye sherehe hizo zilizofanyika katika shule ya Joyland, iliyipo Tuangoma, Kigamboni.
Wazazi walikuwa makini kufuatulia matukio hatua kwa hatua
Mmoja wa walimu wa Joyland akizungumza na wanafunzi wake ambao walikuwa makini kumsikiliza
Mkurugenzi wa Joyland Pre & Primary Inaternational School, Fredrick Otieno akizungumza na wazazi
Kazi ikaanza kwa wanafunzi kuonyesha umahiri wao katika sanaa ya nyimbo
Eee! Watoto wakiwa kwenye maonyesho ya lugha ya Kiingereza
COW! Watoto wakijipanga na kupata neno Cow na kuwaeleza wazazi kwa sauti ya 'Ng'ombe' moooo
Kitengo cha Sayansi hakikuwa nyuma, kilionyesha namna watu wanavyoweza kupanda mazao yao hata juu ya paa
Mwalimu akifafanua jambo baada ya wanafunzi kuonyesha onyesho la sayansi
Yaani vipaji vya sanaa Joyland zimejaa tele!
Walimu wa Joyland wakionyesha manjonjo yao kwa kuimba mbele ya wazazi
Lalalaaaa! Kumbe hata Mkurigenzi wao, Fredrick Otieno (kulia) naye nouma!
Uhondo wa Ngoma Sharti uingie ucheze, Mkurugenzi wa Joyland akiserebuka pamoja na walimu wake.
Yaani ni full gwamba! Bendi ya Shule ya Joyland wakitoa burudani
Mkurugenzi, Fredrick Otieno akizungumza na wazazi na kuwahimiza kuwekeza katika kuwapa watoto elimu bila kujali gharama kwani elimu ni hazina isiyoibwa
Waliofanya vyema walituzwa zawadi kwa umahiri wao darasani
Wakali waliendelea kutuzwa
Limonga Justine Limonga, mtangazaji maarufu wa michezo nchini (kulia) naye alikuwa mmoja aliyekuwa wakigawa zawadi kwa wanafunzi waliofanya vyema katika masomo yao shuleni Joyland International


WAZAZI nchini wamehimizwa kuhakikisha wanawekezea watoto wao katika kupata elimu kwani hazina hiyo ni ya milele kwa maisha ya mtoto kwa sababu ni urithi pekee usiyoweza kuibwa wala kuharibika.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Shule ya Joyland Pre & Primary International, Fredrick Otieno wakati akizungumza na wazazi kwenye hafla ya ufungwaji wa shule hiyo kwa ajili yua likizo fupi.
Otieno alisema urithi pekee unaomfaa mtu katika maisha yake ya baadaye ni elimu, hivyo wazazi wahakikishe wanajinyima na kufanya kila linawezekana kuwapa watoto wao elimu bora.
Alisema pamoja na kwamba elimu ni haki ya mtoto, lakini pia ni jambo la maana kwa maisha ya ukubwa ya mtoto, hivyo wazazi wasipuuzie suala hilo.
Otieno uongozi wa shule yao yenye jumla ya wanafunzi 200 kwa sasa na iliyoanzisha mwaka mmoja uliopita unawashukuru wazazi kwa jinsi  wanavyowapa ushirikiano na kuwaomba waendelee kufanya hivyo.
Alidokeza kuwa pamoja na mipango mingi ya kuzidi kuiboresha shule hiyo ya kisasa, ikiwapo kuja kuanzisha sekondari na kukuza vipaji vya michezo, lakini alidai linalowatatiza kwa sasa ni ukosefu wa umeme.
"Umeme ndiyo tatizo kubwa kwa shule yetu, japo tunazo jenereta lakini lengo letu ni kuvuta umeme, ni tunatakiwa kugharamia kiasi cha Sh Milioni 56 kufanikisha hilo, hivyo wazazi msituangushe," alisema.
Katika sherehe hizo zilizoendana na maonyesho ya masomo kwa wanafunzi, watoto mbalimbali waliofanya vyema katika mitihani yao na shuleni kwa ujumla walizawadiwa zawadi mbalimbali.

No comments:

Post a Comment