STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 5, 2014

Chelsea yarejea kileleni ikiibutua Stoke City 3-1

Mohamed Salah
Mohammed Salah akifunga bao la kuongoza la Chelsea dhidi ya Stoke City
KLABU ya Chelsea usiku huu imerejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kuifumua timu ya Stoke City kwa mabao 3-1 katika pambano lililochezwa uwanja wa Stanford Bridge.
Vijana wa Jose Mourinho wenye kibarua kigumu Jumanne ijayo dhidi ya PSG waliowatandika mabao 3-1 mjini Paris katika mechi ya robo fainali ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliandika bao la kwanza dakika ya 32 kupitia Mohamed Salah aliyemalizia kazi ya Nimanja. Matić bao lililodu hadi wakati wa mapumziko.
Kipindi cha vijana vijana wa Darajani walikuja na nguvu mpya na kufanikiwa kuongeza bao la pili lililofungwa na kiungo wake mkongwe, Frank Lampard katika dakika ya 61' kabla ya Willian kuhitimisha karamu ya mabao dakika ya 72 kwa pande la Mohammed Salah.
Kwa ushindi huo Chelsea imefikisha jumla ya pointi 72 na kukalia kiti cha uongozi kwa muda kwa kuing'oa Liverpool ambayo itashuka dimbani kesho kubakabiliana na West Ham Utd katika mechi ya ugenini.
Mechi nyingine kwa mujibu wa ratiba hiyo, Everton itakuwa wenyeji wa Arsenal ya kocha Arsene Wenger.
Jumatatu  Tottenham Hotspur itakuwa ikijaribu kurejea kwenye nafasi yake ya sita baada ya jioni hii kuenguliwa na Manchester Utd itakapokuwa nyumbani kuikaribisha Sunderland.

No comments:

Post a Comment