TIMU
ya soka ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itacheza mechi ya kirafiki
na Burundi (Intamba Mu Rugamba) Aprili 26 mwaka huu ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari ipo kambini
Tukuyu mkoani Mbeya ikijiandaa kwa ajili ya mechi hiyo ikiwa na
wachezaji waliopatikana katika programu maalumu ya kusaka vipaji.
Mechi hiyo itakayofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam itachezeshwa na waamuzi wanaotambuliwa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kutoka nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment