STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 5, 2014

Jahazi ya timu ya Babi lazidi kutota Malaysia

Kikosi cha UiTM inayozidi kutetereka kwenye Ligi Kuu ya Malaysia
HALI siyo shwari kwa timu ya UiTM ya Malaysia anayoichezea kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Abdi Kassim 'Babi' baada ya jana kufumuliwa tena nyumbani kwa mabao 3-1 na timu ya Kedah.
Hicho kilikuwa ni kipigo cha tatu mfululizo kwa timu hiyo na kuifanya izidi kudorora kwa kushika nafasi ya pili toka mkiani miongoni mwa timu 12 zinazoshiriki Ligi Kuu ya Malaysia.
UiTM ambayo inaelezwa ina mgogoro wa chini kwa chini, imesaliwa na pointi saba tu baada ya kushinda mechi mbili tu na kuambulia sare moja na kufungwa mechi saba.
Jumatatu watakuwa na kibarua kigumu kwa kuwakabili vinara wa ligi hiyo PDRM wanaoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 26 baada ya kucheza mechi 10 kama wapinzani wao.

No comments:

Post a Comment