STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 5, 2014

Homa ya mechi na Azam, Ruvu Shooting yastopisha watatu

Kikosi cha Ruvu Shooting kitakachovaana na Azam siku ya Jumatano
KATIKA kinachoonekana kama ni 'homa' ya pambano lao dhidi ya Azam litakalochezwa siku ya Jumatano uongozi wa Ruvu Shooting umewapiga 'stop' wachezaji wao watatu kwa madai ya utovu wa nidhamu.
Wachezaji waliosimamishwa kwa mujibu wa Msemaji wa klabu hiyo, Masau Bwire ni Ibrahim Susan 'Chogo', Juma Seif 'Kijiko' na Cosmas Lewis wanaodaiwa walitimka kambini bila ruhusa na uongozi kuingiwa na hofu nao na hivyo kuwasimamisha hadi baada ya mechi hiyo.
Bwire alisema wachezaji hao hawatakuwepo kwenye pambano hilo na watatakiwa kujieleza kwa viongozi sababu ya kufanya utovu huo wa nidhamu.
"Tumewasimamisha kwa kitendo chao cha kuondoka kambini bila ruksa na hivyo watatakiwa kujieleza baada ya mchezo huo wa Jumatanoi,' alisema Bwire.
Ruvu Shooting inatarajiwa kuwa wenyeji wa vinara hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Azam katika pambano litakalochezwa kwenye uwanja wa Mabatini-Mlandizi siku ya Jumatano.
Awali mechji hiyo ilipangwa kuchezwa kesho, lakini Azam iliomba udhuru kutokana na wachezaji wake watano kuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana U20, Ngorongoro Heroes ambayop kesho watashuka dimbani nchini Kenya kuumana na vijana wenzao katika mechi ya kuwania fainali za Afrika kwa timu za vijana.

No comments:

Post a Comment