STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 5, 2014

Messi aizamisha Real Betis Hispania

Barcelona v Real BetisNYOTA wa Argentina, Lionel Messi ameendelea kutisha kwa mabao baada ya usiku huu kuizamisha Real Betis kwa kufunga mabao mawili yaliyoisaidia Barcelona kushinda 3-1.
Mchezaji huyo,  alianza kufunga bao katika dakika ya 14 kwa mkwaju wa penati kabla ya kuongeza jingine katika kipindi cha pili kwenye dakika ya 86.
Beki wa Betis, Jordi Figueras alijifunga bao na kuipa Barca uongozi wa mabao 2-0 katika dakika ya 67 kabla ya Rubén Castro kufunga bao la kufutia machozi dakika moja baadaye ndipo messi akaja kumalizia udhia na kuifanya Barca kuijongeza Atletico iliyopo kileleni.
Kivumbi cha ligi hiyo yta Hispania inaendelea hivi sasa Real Madrid ikiwa ugenini tayari inaoongoza kwa bao 1-0 dhidi ya Real Sociedad, goli likifungwa na Illarramendi sekundu chache kabla ya mapumziko.

No comments:

Post a Comment