STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 5, 2014

Leicester City yarudi Ligi Kuu ya England

http://legacymedia.localworld.co.uk/275788/Article/images/17264623/4288974.jpg
LEICESTER City imekuwa klabu ya kwanza kupanda Ligi Kuu ya England ikiirejea baada ya miaka 10 tangu iicheze kwa mara ya mwisho mwaka 2004.
Leciester ilijihakikisha nafasi hiyo ya kucheza EPL msimu ujao baada ya jana kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sheffield Wednesday na kuwafanya wafikishe pointi 89.
Pointi hizo zimeihakikishia moja ya nafasi mbili za kupanda moja kwa moja na hasa baada ya matokeo ya mechi zilizochezwa leo katika Ligi Daraja la Kwanza ya nchi hiyo.
Vijana hao wa Nigel Pearson wamepata nafuu zaidi baada ya Burnsley kulazimishwa sare ya 0-0 na kufikisha pointi 80, huku QPR ikikumbana na kipigo na kubakia na pointi zao 70 wakibaki nafasi ya tatu.

No comments:

Post a Comment