STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 5, 2014

Stand United yaizidi ujanja Mwadui, yapanda Ligi Kuu

Wachezaji wakisalimiana kabla ya mchezo kuanza.
Stand United (Orange) walipoumana na JKT Kanembwa (blue)
KLABU ya Stand United ya Shinyanga imepanda Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu ujao baada ya leo kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Toto African na kuizidi maarifa Mwadui Fc ambayo licha ya kuifunga Polisi Dodoma, lakini imejikuta ikiambulia patupu katika kundi C la Ligi Daraja la Kwanza.
Ushindi huo wa Stand timu pendwa mkoani Shinyanga, imeifanya kufikisha pointi 32 baada ya kushinda rufaa yao dhidi ya Kanembwa JKT katika mechi yao ya marudiano iliyochezwa mjini Tabora kwa kosa la kuwachezesha wachezaji walioongezwa kwenye dirisha dogo.
Kabla ya kushinda rufaa hiyo ambayo maamuzi yake yametolewa leo, ingeweza kumaliza nyuma ya Mwadui iliyokuwa na pointi 31 baada ya kuishinda Polisi Dodoma mjini Dodoma.
Stand kwa kufuzu huko Ligi Kuu inaungana na Ndanda na Polisi Moro zilizofuzu kutoka kundi A na B.

No comments:

Post a Comment