STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 5, 2014

Hatimaye Bayern yafungwa Ujerumani

Crucial strike: Augsburg's Sascha Moelders celebrates his goal against Bayern Munich
Muuaji wa Bayern Munich leo kwenye Bundesliga

MABINGWA wa Bundesliga, Bayern Munich, hatimaye imesimamishwa rekodi yao kutofungwa katika mechi 53 baada ya jioni hii kupigwa kidude na Augsburg.
Bao pekee la dakika ya 31 lililofungwa na Sascha Moelders lilitosha kuwazima vijana wa kocha Pep Gardiola ambacho Jumatano itakuwa na kibarua kigumu kwa Manchester United kwenye mechi ya mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika mechi ya awali timu hizo zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na hivyo kuwafanya Bavarians kuwa na kibarua kigumu kuwasimamisha Mashetani Wekundu ambao wameanza kurejea kwenye fomu.
Kwa kipigo hicho Bayern imeendelea kubakiwa na pointi 78 baada ya mechi 29, huku wakiwa tayari wameshanyakua taji hilo kitambo

No comments:

Post a Comment