STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 5, 2014

Mashetani Wekundu waitafuna Newcastle 4-0

Juan Mata alivyotisha leo nyumbani kwa Newcastle United
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya England, Manchester United imezidi kutakata katika ligi hiyo baada ya  kuibamiza Newcastle Utd ikiwa kwao kwa mabao 4-0, Juan Mata akihusika na mabao matatu.
Mata alifunga mabao mawili na kusaidia jingine lililofungwa na Adnan Januzaj dakika ya 90.
Kiungo mshambuliaji huyo aliyesajiliwa kutoka Chelsea alifunga mabao yake katika dakika ya 39 na 50 na bao jingine lililifungwa na Javier Hernandez 'Chicharito' katika dakika ya 64 na kumpa nafuu kocha david Moyes baada ya timu yake kuchupa hadi nafasi ya sita.
Mashetani Wekundu wao wamefikisha pointi 57 na kuiengua Tottenham Hotspur itakayoshuka dimbani kesho.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Aston Villa ikiwa uwanja wake wa nyumbani imebamizwa mabao 2-1 na Fulham, Cardiff City nayo ilikufa nyumbani kwa mabao 3-0 toka kwa Crystal Palace na Hull City ikiwa nyumbani iliilaza Swansea City bao 1-0 na West Bromwich iliifumua Norwich City kwao kwa bao 1-0.
Chelsea wapo uwanja kwa sasa kupepetana na Stoke City na matokeo mpaka sasa ikiwa ni dakika ya 26 ni 0-0.

No comments:

Post a Comment