STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, April 5, 2014

PSG yaifumua Reims 3-0 yanusa ubingwa Ufaransa

http://i.smimg.net/13/34/300x225/edinson-cavani-psg.jpg
Edinson Cavani
PSG bila Zlatan Ibrahimovic jioni hii imepata ushindi mnono wa mabao 3-0 ikiwa nyumbani dhidi ya Reims na kujiweka katika mazingira mazuri ya kutetea taji la Ligi Kuu ya Ufaransa.
Edinson Cavani alianza kuifungia PSG bao dakika mbili kabla ya mapumziko akimalizia kazi ya van der Wiel.
Dakika tatu baada ya kuanza kwa kipindi cha pili, wageni walijifunga bao kupitia kwa Aissa Mandi kabla ya mchezaji huyo kuijifunga tena katika dakika ya 89 nma kuipa nafasi kubwa PSG kutetea taji lao.
Kwa ushindi huo, PSG inayotarajiwa kuvaana na Chelsea mjini London siku ya Jumanne katika mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ikiwa na hazina ya ushindi wa mabao 3-1 imeifanya ifikishe pointi 79 na kuzidi kuwakimbia wapinzani wao Monaco waliopo nafasi ya pili na poingti 63.

No comments:

Post a Comment