STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, February 8, 2015

Manchester Utd chupuchupu kufa ugenini

Falcao akijaribu kufunga
Kouyate akishangilia bao lake
Pilikapilika uwanjani
KLABU ya Manchester United imeponea chupu chupu kufa ugenini baada ya kupata sare ya 1-1 mbele yua West Ham United.

Bao la kusawazisha lililofungwa dakika za lala salama na Daley Blind liliwaokoa Mashetani Wekundu kufa katika uwanja wa Boleyn Ground.
Blind alifunga bao hilo katika dakika mbili za nyongeza na kumnusuru kocha Luis Van Gaal kuumbuka kama alivyonusurika kocha wa Manchester City jana dhidi ya Hull City baada ya vijana wake kusawazisha bao dakika za jioni.
Wenyeji walitangulia kupata bao dakika ya 49 kupitia kwa Cheikhou Kouyaté na kulikuwa na kila dalili kwa Mashetani Wekundu kufa ugenini, lakini Blind kuchomoa na kuifanya Manchester United kufikisha pointi 44 na kukomalia nafasi ya nne nyuma ya Southampton waliorejea katika Tatu Bora.
Hata hivyo dakika mbili za nyongeza baada ya Man kupata bao ilijikuta ikimpoteza beki wake, Luke Shaw kwa kupewa kadi nyekundu ilifuatia kutokana na kadi ya pili ya njano kwa kumchezea vibaya Stewart Downing.
Vikosi vilikuwa hivi; 
West Ham: Adrian, Jenkinson, Song, Tomkins, Cresswell, Kouyate, Noble, Downing, Nolan, Valencia, Sakho.
Sub: Jarvis, O'Brien, Amalfitano, Jaaskelainen, Cole, Oxford, Lee
Manchester United: De Gea, Valencia, Jones, Rojo, Shaw, Blind, Rooney, Januzaj, Di Maria, van Persie, Falcao
Sub: Mata, Smalling, Ander Herrera, Fellaini, Valdes, McNair, Wilson

Kocha Redknapp kurejea soka kama mwanahisa

http://talksport.com/sites/default/files/tscouk_old_image/blog/Harry-Redknapp_21.jpg
Kocha Harry Redknapp
MENEJA wa zamani wa klabu ya QPR, Harry Redknapp amebainisha anaweza kurejea katika ulimwengu wa soka akiwa sehemu ya mwanahisa.
Redknapp mwenye umri wa miaka 67 ambaye alijiuzulu kuinoa QPR wiki iliyopita kutokana na matatizo ya mguu anahusishwa na kikundi kinachotaka kununua klabu karibu na nyumbani kwake katka Pwani ya Dorset.
Akihojiwa Redknapp amesema jambo hilo linamvutia hivyo anataka kujihusha nalo, kwani mchezo wa soka bado uko katika damu yake.
Redknapp ambaye amewahi kuipeleka Tottenham Hotspurs katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na pia kuzinoa klabu za Portsmouth na West Ham United aliongeza kuwa wana matumaini ya kupata klabu ya kuinunua.

Jose Mourinho aanza mbwembwe zake England

http://static.guim.co.uk/sys-images/Observer/Columnist/Columnists/2013/6/7/1370621593808/jose-mourinho-010.jpg
Jose Mourinho
KOCHA wa vinara wa Ligi Kuu ya England Chelsea, Jose Mourinho amesema hadhani kama tofauti ya pointi saba walionayo kileleni mwa msimamo wa Ligi hiyo ni faida katika mbio zao za kugombea taji hilo. Chelsea imeitandika Aston Villa kwa mabao 2-1 jana, wakati Manchester City wanaowafuata katika nafasi ya pili wakipotoka sare na Hull City wanaokamata nafasi ya tatu toka mkiani.
Akihojiwa Kocha Mourinho, amesema ingekuwa nchi nyingine angeweza kuanza kushangilia katika kwa Uingereza tofauti ya alama saba sio chochote.
Mourinho aliendelea kudai kuwa bado kuna mechi 14 na alama 42 za kupigania hivyo kila mchezo unakuwa mgumu na chochote kinaweza kutokea.
Kocha huyo pia alisisitiza hakushtushwa kuona City wakitoa sare nyumbani na Hull ambao wako mstari wa kushuka daraja lakini amefurahi kuona matumaini ya kunyakuwa taji yakiwa mikononi mwao.
Ligi hiyo iliendelea tena jioni ya leo kwa timu za Newcastle United wakipata sare ya 1-1 na timu ya Stoke City wakati West Bromwich Albion wakiwa ugenini walipata sare ya 2-2 dhidi ya timu ya Burnley.

Sepp Blatter aponda vyombo vya habari vurugu AFCON

http://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/4/44/Sepp_Blatter_at_signing_of_agreement_creating_FIFA_Ballon_d%E2%80%99Or_in_Johannesburg_2010-07-05_1.jpg
Rais wa FIFA, Sepp Blatter
RAIS wa Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA) Sepp Blatter, ameponda vyombo vya habari kuonyesha vurugu zilizozuka katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Mataifa ya Afrika kati ya wenyeji Guinea ya Ikweta na Ghana.
Mchezo huo uliochezwa Malabo ulisimamishwa kwa dakika 30 baada ya mashabiki kurusha vitu kwa wachezaji na mashabiki wa timu pinzani hali iliyosababisha polisi kutumia helikopta na mabomu ya machozi kuwatawanya mashabiki hao.
Vurugu hizo zilikuwa zikirushwa moja kwa moja duniani kote, lakini Blatter anadhani pamoja na vurugu hizo lakini kuna mazuri mengi ya kusifiwa katika michuano hiyo inayotarajiwa kumalizika leo.
Blatter amesema siku zote habari nzuri huwa sio habari ila habari mbaya ndio habari akimaanisha kuwa siku zote watu wamekuwa wakizungumzia mabaya.
Rais huyo amesema dosari ndogo kama iliyotokea katika mchezo wa nusu fainali haipaswi kupewa nafasi ya kusahau mafanikio yaliyopata katika michuano hiyo ambayo imendaliwa kwa kipindi kifupi kuliko ilivyopangwa.

Asamoah Gyan bado alia na Yattara

http://img.modernghana.com/images/content/bgwi04lyx6_asamoahgyan580.jpg
Asamoah Gyan
NAHODHA wa kikosi cha timu ya taifa ya Ghana, Asamoah Gyan ambay anajiandaa kushuka dimbani kuiongoza timu yake katika mechi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika dhidi ya Ivory Coast, amedai hatomsamehe golikipa wa Guinea Naby Yattara kutokana na faulo aliyomchezea timu zao zilipokutana.
Golikipa huyo alimkanyaga Gyan kwa teke la tumboni katika dakika za mwisho za mchezo wa robo fainali uliokutanisha timu hizo.
Yattara alilimwa kadi nyekundu lakini hajapewa adhabu yeyote nyingine mpaka sasa kiasi cha Gyan katika mahojiano yake alisema bado analitaka Shirikisho la Soka la Afrika(CAF) kumtwanga adhabu Yattara kwa sababu anadhani alidhamiria kufanya tukio lile.
Gyan aliendelea kudai kuwa ilikuwa ni faulo mbaya ambayo ingeweza kumsababisha asicheze tena soka ndio maana hataki kumsamehe kwa hilo.
Hata hivyo kipa huyo alinukuliwa juzi akisema kuwa hawezi kumuomba radhi Gyan kwa sababu hakukusudia kumuumiza na kusisitiza kuwa hilo ni tukio la bahati mbaya katika harakati za mchezo.

YANGA YALIPA KISASI, NGASSA AKIONDOA 'GUNDU'

http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2015/02/NGASSA-MRISHO.jpg
Mrisho Ngassa aliyefunga mabao yote mawili Yanga ikiizamisha Mtibwa uwanja wa Taifa
MABAO mawili ya winga machachari Mrisho Ngassa aliyetokea benchi yameiwezesha Yanga kulipa kisasi kwa Mtibwa Sugar na kurejea kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Yanga ambayo awali ilionekana kuugaya mchezo huo uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa, ulishuhudiwa dakika 45 za kwanza mambo yakiwa magumu kwa klabu zote baada ya kutofungana bao lolote.
Hata hivyo mabadiliko yaliyofanywa na kocha Hans van der Pluijm ya kumtoa Kpah Sherman na kumuingiza Mrisho Ngassa yalizaa matunda baada ya mkali huyo kufunga mabao hayo muda mchache tangu awepo uwanjani na kuifanya Yanga kurudi katika nafasi ya kwanza.
Yanga imefanikiwa kufikisha pointyi 25 baada ya mechi 13 na kuiengua Azam ambao jana walilazimishwa sare ya 2-2 na Polisi Morogoro ikiwa na pointi 22 baada ya kucheza mechi 12.
Azam inatarajiwa kushuka dimbani siku ya Jumatano kwa ajili ya kucheza na Mtibwa Sugar katika mechi ya kiporo itakayochezwa uwanja wa Chamazi.
Magoli hayo mawili yamemwezesha Ngassa kuondoa 'gundu' baada ya kutoweza kufunga bao lolote msimu huu, kitu ambacho hakikuwa cha kawaida kwa mchezaji huypo aliyewahi kuwa Mfungaji Bora.
Wakati Azam wakiingia kambini kujiandaa na pambano lao na Mtibwa, Yanga wanatarajiwa kuelekea visiwani Zanzibar ili kuweka kambi kusubiri  mchezo wao wa Kombe la Shirikisho utajkaocheza Jumamosi.
Yanga itashuka dimbani Jumamosi kuumana na BDF XI ya Botswana katika mechi ya mkondo wa kwanza wa raundi ya kwanza ya michuano hiyo kabla ya kurudiana nao wiki mbil baadaye.
MSIMAMO LIGI KUU TANZANIA BARA 2014-2015
                              P   W   D    L    F    A   GD   Pts
01.  Yanga              13  07  04  02  15   07  08  25
02.  Azam               12  06  04  02  17   10  07   22
03. Polisi Moro         14  04  07  03  12   11  01  19
04. JKT Ruvu           14  05  04  05  14   14  00  19
05. Ruvu Shooting   14  05  04  05   10  11   -1  19
06. Mtibwa Sugar     12  04  06  02   13  09  04  18
07. Coastal Union     14  04  06  04  11   10  01  18
08. Kagera Sugar      14 04  06  04   11   11  00  18
09. Simba                 13  03  08  02  13   11  02  17
10. Mbeya City          13   04  04  05  09  11   -2  16
11. Ndanda Fc           14  04  03   07  13  18   -5  15
12. Mgambo JKT        12  04  02  06   06  11   -5  14
13. Stand Utd            14  02  06   06   09  17   -8  12
14. Prisons                13  01  08   04   10   12   -2  11
 

Wafungaji:
7-
Didier Kavumbagu(Azam)
6- Samuel Kamuntu (JKT Ruvu), Rashida Mandawa (Kagera Sugar)
5-
Ame Ali (Mtibwa), Danny Mrwanda (Yanga)
4-
Rama Salim (Coastal),  Simon Msuva (Yanga),  Emmanuel Okwi (Simba), Nassor Kapama (Ndanda)
3- Ally Shomari (Mtibwa),  Jacob Massawe (Ndanda), Kipre tchetche (Azam)
2-
Shaaban Kisiga, Dan Sserunkuma(Simba),  Salum Kanoni, Atupele Green (Kagera Sugar) Aggrey Morris (Azam),  Najim Magulu, Jabir Aziz (JKT Ruvu), Amissi Tambwe, Jerry Tegete, Mrisho Ngassa (Yanga), Ibrahim Kihaka (Prisons), Mussa Mgosi (Mtibwa), Heri Mohammed, Mussa Said (Stand Utd), Ally Nassor,  Malimi Busungu (Mgambo), Nicolaus Kabipe (Polisi),Yahya Tumbo (Ruvu Shooting)

Yanga kulipa kisasi kwa Mtibwa leo Taifa?!

Wakata Miwa wa Manungu, Mtibwa Sugar
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjD1DkH-KANYfSP-lMJIrFLhkzjqB0KhC2HRInBtLOg-GaupvdQqEA5_bgI-mH-UIyzUAItfzKFQQrOWcqfRRa8UBWoaXdQk1K7ESNnytqX3XOT2wNo7RpSWAvXOYRRhw10rgajuMQIjnnn/s1600/IMG_6036.JPG
Kikosi cha Yanga kitatoka vipi leo Taifa?
BAADA ya ombi lao la kutaka mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar kuahirishwa kugonga mwamba kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Yanga leo watashuka dimba la Taifa kwa nia ya kulipa kisasi cha mabao 2-0 walichopewa na wapinzani wao kwenye mechi ya mkondo wa kwanza.
Yanga ilikumbana na kipigo hicho katika mechi ya ufunguzi wa ligi hiyo kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro na iliiomba TFF iwaahirishie mechi yao ili kutoa nafasi ya kujiandaa vizuri kwa mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya BDF XI ya Botswana siku ya Jumamosi ijayo.
TFF imewachomolea na kuwataka washuke dimbani leo na kuwa na muda wa wiki moja ya kuvaana na wageni wao watakaowafuata Alhamisi wiki hii kwa ajili ya mchezo huo wa Jumamosi.
Ikiwa imetoka kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 uliovunja mwiko wa kushindwa kushinda katika uwanja wa Mkwakwani kwa karibu misimu miwili sasa, Yanga itawashukia Mtibwa Sugar kama mwewe kutokana na hasira za 'kubaniwa' na TFF.
Hata hivyo Yanga isitarajie mteremko kwani wapinzani wao, kwani msimu huu timu hiyo imeonekana kuimarika zaidi kuliko misimu miwili iliyopita na isingependa kulala tena jijini Dar kama ilivyokuwa katika msimu uliopita walipochapwa mabao 2-0.
Ikiwa chini ya nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Mexime, Mtibwa ilikaa muda mrefu kileleni kabla ya kuteleza baada ya kuruhusu kipigo chake cha kwanza toka kwa maafande wa Ruvu  Shooting na leo ingependa kupata ushindi ili kujirejesha nafasi za juu.
Mtibwa Sugar imeporomoka toka nafasi ya tatu hadi ya sita ikiwa na pointi 18 wakati watani zao wapo nafasi ya pili baada ya Azam kuwaporomosha kufuatia sare ya mabao 2-2 iliyoapa mjini Morogoro dhidi ya Polisi Moro.
Kocha Mexime waliolazimishwa suluhu ya 0-0 na Coastal Union katika mechi yao ya mwisho, alisisitiza kuwa lengo lao ni kuona wanamaliza katika nafasi mbili za juu na hivyo wamerekebisha makosa yaliyowafanya washindwe kupata ushindi katika mechi  nne zilizopita za ligi hiyo.
Timu hiyo katika mechi hizo iliambulia sare tatu na kipigo kimoja na kuwwafanya waporomoke kileleni waliokoongoza kwa muda mrefu tangu kuanza kwa msimu huu.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema kikosi chao kipo tayari kwa vita ya leo ili kuweza kuendeleza ubabe wao na kujiweka katika mazingira mazuri ya kuchukua ubingwa baada ya kurejea kileleni.
Muro alisema Yanga itawakosa baadhi ya nyota wake ambao ni majeruhi, lakini bado wachezaji waliosalia wataiongoza timu hiyo kulipa kisasi cha mabao 2-0 ilichopewa mjini Morogoro katika mechi ya mkodno wa kwanza kabla ya kuingia kambini kuwasubiri BDF XI ya Botswana kwenye mchezo wa kimataifa.

Man Utd, West Ham vita kali England

http://www.whufc.com/javaImages/86/a4/0,,~11445382,00.jpg

KLABU ya Manchester United ikiwa na furaha ya kufuzu Raundi ya Tano ya Kombe la FA, leo watakuwa dimba la ugenini kupepeta na West Ham Utd katika moja ya michezo minne ya Ligi Kuu ya England.
Vijana wa Luis Van Gaal, wanaifuata Wagonga Nyundo wa London wakitoka kuitoa nishai Cambridge United walionekana kutaka kuwatoa nishai kama vigogo vingine vilivyofanyiwa kwenye michuano hiyo ya FA.
Mashetani Wekundu waliichapa timu hiyo ya Daraja la Pili mabao 3-0 baada ya mechi ya kwanza wiki iliyopita kuisha kwa suluhu ya 0-0, hivyo watatua uwanja wa Boleyn Ground kwa nia ya kuendeleza furaha yao.
Wakiwa na kumbukumbu ya kushinda katika mechi ya kwanza msimu huu dhidi ya wapinzani wao ambao kwa misimu mitatu sasa hajaonja ushindi mbele ya Mashetani Wekundu, Manchester isitarajie mteremko.
West Ham wamekuwa na msimu mzuri safari hii wakishinda mechi 10 kati ya 23 walizocheza wakikamata nafasi ya nane na pointi zao 36,  saba pungufu na ilizonazo Man Utd waliopo nafasi ya tatu katika msimamo.
Mbali na mechi hiyo pia katika ligi hiyo leo kutakuwa na michezo mingine miwili wa mapoema ukizikutanisha timu za Burnley dhidi ya West Bromwich kabla ya Newcastle United kukikaribisha Stoke City.

NI GHANA AU IVORY COAST LEO

* Zinakutana katika fainali ya kisasi

http://www.ghanatoghana.com/wp-content/uploads/2015/01/Ghana-black-stars-players-group-picture.jpg
Ghana Black Stars
https://nbcprosoccertalk.files.wordpress.com/2013/11/ivory-coast-oct.jpg
Kikosi cha Ivory Coast
MALABO, Guinea ya Ikweta
AFRIKA inatarajiwa kufahamu Bingwa Mpya wa soka wakati Ivory Coast na Ghana zitakapoumana kwenye mchezo wa fainali za michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2015.
Pambano hilo litakalopigwa kwenye uwanja wa Estadio de Bata, linakumbushia fainali za mwaka 1992 wakati Tembo wa Afrika, Ivory Coast na Black Stars ya Ghana zilipokutana nchini Senegal.
Katika fainali hiyo ya aina yake, Ivory Coast waliwazidi kete wapinzani wao hao na kutwaa taji hilo kwa mikwaju ya penati 11-10 baada ya kumaliza dakika 120 milango ya timu zote ikiwa migumu.
Ivory Coast wamefuzu hatua hiyo baada ya kuing'oa timu ya DR Congo kwa kuwachapa mabao 3-1 katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa Jumatano, huku kocha wake Herve Renald 'akizuga; kuwa walipenya kibahati kutokana na timu yake kucheza ovyo.
Wenyewe Ghana walifanikiwa kuwatoa wenyeji Guinea ya Ikweta kwa kuwabangua mabao 3-0 katika mechi iliyojaa vurugu za mashabiki waliokuwa wakishinikiza mwamuzi 'kuwabeba' tena kama ilivyokuwa katika mechi ya robo fainali dhidi ya Tunisia iliyomponza refa wa Mauritius kufungiwa.
Wenyeji hao walitarajiwa jana kuvaana na DR Congo kwa ajili ya kuwania nafasi ya mshindi wa tatu na nne wa fainali hizo za 30 ambazo zilianza kutimua vumbi lake tangu Januari 17.
Mchezo huo wa fainali unasubiriwa kwa hamu kutokana na umahiri wa vikosi vya timu hizo za Afrika Magharibi na washiriki wa Fainali zilizopita za Kombe la Dunia zilizofanyika nchini Brazili.
Tembo wa Afrika wanajivunia kikosi kinachoundwa na nahodha wake Yaya Toure ambaye ndiye Mchezaji Bora wa Afrika, sambamba na mwanasoka ghali wa Afrika, Wilfried Bony na wakali wengine.
Wakati wapinzani wao wanatambia nahodha wake, Asamoah Gyan,  Andre Ayew na nduguye Jordan Ayew, Kwame Appiah na wengine wanaochezaji soka la kulipwa katika klabu mbalimbali za Ulaya.
Kikosi cha Ghana kinachonolewa na kocha wa zamani wa Chelsea,  Avram Grant ambaye atakuwa akitaka kuwapa waajiri wake taji la tano  baada ya kulikosa kwa muda mrefu tangu walipotwaa mara ya mwisho mwaka 1982 na kulikosa kwenye fainali za mwaka 2010 mbele ya Misri.
Ivory Coast wenyewe watakuwa wakisaka taji la pili la michuano hiyo baada ya fainali za mwaka 2012 zilizofanyika nchini Guinea ya Ikweta ikishirikiana na Gabon kulikosa kwa kufungwa na Zambia.
Cha kuvutia ni kwamba kocha aliyewapa taji Zambia mwaka huo, Herve Renald ndiye anayeinoa timu hiyo kwa sasa na kama timu yake itashinda leo ataweka rekodi ya aina yake Afrika ya kuw kocha wa kwanza kuchukua taji hilo akiwa na nchi mbili tofauti.
Je ni Tembo wa Afrika au Nyota Weusi watakaoibuka na ushindi katika mchezo huo wa leo? Tusubiri tuone baada ya kumalizika wa fainali hizo zilizohamishiwa Guinea ya Ikweta baada ya waliokuwa wenyeji wa awali Morocco kuchomoa kwa kisingizio cha hofu ya ugonjwa wa Ebola.
Kitendo hicho kimesababisha nchi hiyo ya Morocco kuadhibiwa kwa kufungiwa fainali mbili za Afrika za 2017 na 2019.

Mchujo wa mabondia wa All African Games kuanza kesho

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgKf3j_9lbtaLQyaz_zQF0flGoPDNwRHy3gQ4ONfElr_vig3q8o4Qz8FPYmcPqZ0gMZDYrQgTaoGCdBXuRzDb3SOhXV60xTZTtAozbghUpubPSY0R6H4oYZPX0-B6AMkqUQhs2jWXY7oUw/s1600/antony.JPG
Mchujo kama huu unatarajiwa kuanza kesho Uwanja wa Ndani wa Taifa
http://www.thisday.co.tz/media/picture/large/BFTsecretary%20genera%20Makore%20Mashaga1.jpg
Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga
MCHUJO wa kusaka mabondia wa kuingia kambini kwa ajili ya ushiriki wa michuano ya Michezo ya Afrika (All African Games) unatarajiwa kuanza kesho jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga alisema mashindano ya mchujo huo utafanyika kwenye Uwanja wa Ndani ya Taifa na utamalizika Siku ya Wapendanao Februari 14.
Mashaga alisema mashindano hayo maalum yatashirikisha walifanya vizuri katika mashindano ya wazi ya taifa yaliyofanyika hivi karibuni katika Uwanja wa Taifa.
"Mashindano maalum kwa ajili ya kusaka mabondia watakaotuwakilisha kwenye michezo ya Afrika yataanza Februari 9-14 Uwanja wa Ndani wa Taifa na utashirikisha waliofanye vema kwenye michuano ya wazi," alisema.
Kwa mujibu wa Mashanga mabondia 39 watachujana ili kupatikana 15 ili kuunda timu ya taifa ya mchezo huo wa ngumi.
Mashindano hao ya Mataifa ya Afrika yanatarajiwa kutimua vumbi lake kati ya Septemba 4-19 mjini Brazzaville, Congo na Tanzania ni miongoni mwa nchi shiriki.