STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Sunday, February 8, 2015

Yanga kulipa kisasi kwa Mtibwa leo Taifa?!

Wakata Miwa wa Manungu, Mtibwa Sugar
http://3.bp.blogspot.com/-tF7Zk9GPpjs/VKb2tjxT3jI/AAAAAAACVKE/K8Kraov5bvI/s1600/IMG_6036.JPG
Kikosi cha Yanga kitatoka vipi leo Taifa?
BAADA ya ombi lao la kutaka mechi yao dhidi ya Mtibwa Sugar kuahirishwa kugonga mwamba kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Yanga leo watashuka dimba la Taifa kwa nia ya kulipa kisasi cha mabao 2-0 walichopewa na wapinzani wao kwenye mechi ya mkondo wa kwanza.
Yanga ilikumbana na kipigo hicho katika mechi ya ufunguzi wa ligi hiyo kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro na iliiomba TFF iwaahirishie mechi yao ili kutoa nafasi ya kujiandaa vizuri kwa mchezo wao wa Kombe la Shirikisho dhidi ya BDF XI ya Botswana siku ya Jumamosi ijayo.
TFF imewachomolea na kuwataka washuke dimbani leo na kuwa na muda wa wiki moja ya kuvaana na wageni wao watakaowafuata Alhamisi wiki hii kwa ajili ya mchezo huo wa Jumamosi.
Ikiwa imetoka kupata ushindi mwembamba wa bao 1-0 uliovunja mwiko wa kushindwa kushinda katika uwanja wa Mkwakwani kwa karibu misimu miwili sasa, Yanga itawashukia Mtibwa Sugar kama mwewe kutokana na hasira za 'kubaniwa' na TFF.
Hata hivyo Yanga isitarajie mteremko kwani wapinzani wao, kwani msimu huu timu hiyo imeonekana kuimarika zaidi kuliko misimu miwili iliyopita na isingependa kulala tena jijini Dar kama ilivyokuwa katika msimu uliopita walipochapwa mabao 2-0.
Ikiwa chini ya nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Mecky Mexime, Mtibwa ilikaa muda mrefu kileleni kabla ya kuteleza baada ya kuruhusu kipigo chake cha kwanza toka kwa maafande wa Ruvu  Shooting na leo ingependa kupata ushindi ili kujirejesha nafasi za juu.
Mtibwa Sugar imeporomoka toka nafasi ya tatu hadi ya sita ikiwa na pointi 18 wakati watani zao wapo nafasi ya pili baada ya Azam kuwaporomosha kufuatia sare ya mabao 2-2 iliyoapa mjini Morogoro dhidi ya Polisi Moro.
Kocha Mexime waliolazimishwa suluhu ya 0-0 na Coastal Union katika mechi yao ya mwisho, alisisitiza kuwa lengo lao ni kuona wanamaliza katika nafasi mbili za juu na hivyo wamerekebisha makosa yaliyowafanya washindwe kupata ushindi katika mechi  nne zilizopita za ligi hiyo.
Timu hiyo katika mechi hizo iliambulia sare tatu na kipigo kimoja na kuwwafanya waporomoke kileleni waliokoongoza kwa muda mrefu tangu kuanza kwa msimu huu.
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema kikosi chao kipo tayari kwa vita ya leo ili kuweza kuendeleza ubabe wao na kujiweka katika mazingira mazuri ya kuchukua ubingwa baada ya kurejea kileleni.
Muro alisema Yanga itawakosa baadhi ya nyota wake ambao ni majeruhi, lakini bado wachezaji waliosalia wataiongoza timu hiyo kulipa kisasi cha mabao 2-0 ilichopewa mjini Morogoro katika mechi ya mkodno wa kwanza kabla ya kuingia kambini kuwasubiri BDF XI ya Botswana kwenye mchezo wa kimataifa.

No comments:

Post a Comment