KLABU ya Manchester United ikiwa na furaha ya kufuzu Raundi ya Tano ya Kombe la FA, leo watakuwa dimba la ugenini kupepeta na West Ham Utd katika moja ya michezo minne ya Ligi Kuu ya England.
Vijana wa Luis Van Gaal, wanaifuata Wagonga Nyundo wa London wakitoka kuitoa nishai Cambridge United walionekana kutaka kuwatoa nishai kama vigogo vingine vilivyofanyiwa kwenye michuano hiyo ya FA.
Mashetani Wekundu waliichapa timu hiyo ya Daraja la Pili mabao 3-0 baada ya mechi ya kwanza wiki iliyopita kuisha kwa suluhu ya 0-0, hivyo watatua uwanja wa Boleyn Ground kwa nia ya kuendeleza furaha yao.
Wakiwa na kumbukumbu ya kushinda katika mechi ya kwanza msimu huu dhidi ya wapinzani wao ambao kwa misimu mitatu sasa hajaonja ushindi mbele ya Mashetani Wekundu, Manchester isitarajie mteremko.
West Ham wamekuwa na msimu mzuri safari hii wakishinda mechi 10 kati ya 23 walizocheza wakikamata nafasi ya nane na pointi zao 36, saba pungufu na ilizonazo Man Utd waliopo nafasi ya tatu katika msimamo.
Mbali na mechi hiyo pia katika ligi hiyo leo kutakuwa na michezo mingine miwili wa mapoema ukizikutanisha timu za Burnley dhidi ya West Bromwich kabla ya Newcastle United kukikaribisha Stoke City.
No comments:
Post a Comment