STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, August 21, 2013

Kimenuka! 3 Pillars ya Nigeria yatelekezwa, kisa deni ya Sh Mil. 17 la hoteli waliyohifadhiwa..yadaiwa walikuja kwa 'dili' nyingine kabisa....!

  •  
  • MFADHILI ALIYEWALETA AWATELEKEZA
  • YADAIWA WALIKUJA KUFANYA BIASHARA HARAMU
  • BAADA YA MIANYA KUZIBWA - MFANYABIASHARA ALIYEWALETA AWATEMA
Imefahamika kwamba klabu ya 3 Pillars ya Nigeria ipo katika hali ngumu sana kimaisha jijini Dar es Salaam baada ya mtu mmoja aliyeleta timu hiyo nchini ambaye ana makazi Tanzania na huko Falme za Kiarabu kutokomea na kuitelekeza timu hiyo. 

 Kwa mujibu wa chanzo cha habari  hii - mtu ambaye amekuwa akihusishwa na kuileta timu hiyo nchini kwa ajili ya mechi za kujipima nguvu - ni kwamba 3 Pillars waliletwa nchini na mfanyabiashara mmoja mwenye asili ya kiarabu kwa madhumuni ya kufanya biashara haramu na ndio maana timu hiyo ilikuwa haichukui hata shilingi katika mechi mbili za kirafiki ilizocheza hapa nchini na Klabu ya Yanga pamoja na Coastal Union kwa kuwa walikuwa wanapewa kila kitu na mfanyabiashara aliyewaleta nchini.

Lakini kutokana na hali ya ulinzi kuimarika nchini kutokana na mfululizo wa watanzania kukamatwa na wakiwa wamebeba baishara haramu - kazi ambayo 3 Pillars walitumwa kuja kuifanya Tanzania na mfadhili wao ikawa imeingia mdudu, hivyo mfanyabaishara huyo ameitelekeza timu hiyo ya Nigeria katika hoteli ya Itumbi iliyopo Magomeni Mwembechai ambapo mpaka kufikia siku wanarudi kucheza mechi dhidi ya Yanga tayari walikuwa na deni la millioni 12. Mpaka hivi sasa timu hiyo inadaiwa zaidi ya millioni 17 wakiwa hawajui namna ya kulipa deni hilo.

Mtandao huu uliwasiliana na meneja ya hoteli ya Itumbi na alithibitisha ni kweli klabu hiyo ya 3 Pillars inadaiwa deni hilo: "Ni kweli kabisa hawa jamaa tunawadai kiasi cha millioni 17, mpaka kufikia jana walikuwa hawajatupa muelekeo wa namna watakavyolipa deni hili. Mmiliki wa Hoteli jana alikuwa na kikao na viongozi wao wametoa ahadi kwamba wanaongea na ubalozi wao ili kuweza kupata msaada wa kulipa deni hilo waweze kuondoka nchini na kurudi kwao. Kwa sasa imebidi tusiwape huduma ya chakula ili kutokuongeza deni, hivyo haifahamiki wanakula au vipi," alisema meneja wa hoteli hiyo.

Wakati huo huo imefahamika kwamba ulifanyika mchezo mchafu katika kuzuia 3 Pillars isicheze michezo ya kujipima nguvu Tanzania na baadhi ya viongozi wa TFF kwa maslahi yao binafsi - yanayohusiana na uchaguzi mkuu wa TFF

...........................itaendelea 
 
SHAFII DAUDA 

Sifa zamtokea puani Diamond...Dk Mwakyembe ataka achunguzse ukaribu wake na 'wauza unga'

Diamond
BAADA ya msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platnum kutajwa kujihusisha na mtandao wa dawa za kulevya waziri wa Uchukuzi Dk Harrison Mwakyembe atoa agizo msanii huyo aanze kuchunguzwa.
Msanii huyo leo ameripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari kujihusisha na dawa za kulevya.
Uchunguzi huo utahusisha kuangalia vyanzo vyake vya mapato kama vinaendana na matumiz yake, wakati inasemekana  akaunti za diamond ambazo zinaonekana kubwa mno kulinganisha na kipato cha kawaida cha wasanii.
Hali hiyo imetokana na vugu vugu la kujaribu kuisafisha tanzania kutokana na kushamiri kwa madawa ya kulevya limefikia hatua nzuri na ya kipekee. Dk Mwakyembe amejitosa haswa kupambana na wauza unga, moja kati ya majina yanayosemekana ya wauza unga yanayodaiwa yapo ktk kitengo internal intelligency lipo jina la msanii Diamond.
Inasemekana Diamond ana urafiki wa karibu na mabosi wa Masogange, ambao wengine wapo nchini Afrika Kusini, kamera za cctv za uwanja wa wa ndege wa kitaifa JNIA zimekuwa zikionesha ukaribu wa Diamond na wale watu waliotajwa na Waziri Mwakyembe kuwa walimsaidia Masogange kupitisha mzigo.
Pia safari za kimuziki sehemu mbalimbali duniani ambazo nyingi hupangwa/kutafutwa na vigogo wa madawa ya kulevya waliopo tanzania na wale waliopo Afrika Kusini .
Wakati pia sasa serikali inajaribu kuchunguza akaunti za diamond ambazo zinaonekana kubwa mno kulinganisha na kipato cha kawaida cha wasanii. 
Uchunguzi bado unaendelea, lakini Diamond amekanusha kuhusika na sembe.
 
Chanzo:Pro24 

Hatimaye Abdi Kassim 'Babi' atua KMKM

Abdi Kassim 'Babi'
KIUNGO mshambuliaji nyota wa zamani wa Yanga na Taifa Stars, aliyekuwa akiichezea Azam katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu uliopita, Abdi Kassim 'Babi' au Ballack wa Ugunja' amemwaga wino wa kuichezea mabingwa wa Zanzibar KMKM.
Babi ambaye alikanusha taarifa za kutemwa na Azam na badala yake kueleza kwamba baada ya mkataba wake kumalizika aliamua kuachana na timu hiyo, ametgoa taarifa kupitia akaunti yake ya FB kwamba kwa sasa yeye ni mali ya KMKM baada ya kumwaga wino na kufurahi kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa mwakani.
Mkali huyo aliyewahi kucheza soka la kulipwa Vietnam alisema kutua kwake KMKM kumempa faraja kutokana na kufanya kazi chini ya kocha mzoefu nchini, Ali Bushiri.
Ujumbe wake kwa mafans wake uliotumwa na mkali huyo mwenye mashuti makali unasomeka kama hivi hapo chini:
"Hi nyote ..Nashukuru Mungu mzima wa afya ..nimesaini mkataba na kmkm mabingwa wa soka zanzibar na timu inayo shiriki mashindano ya kimataifa na mashindano mbali mbal ..ikiongozwa na coach mzoefu na mwenye ujuzi wa hali ya juu..ali bushir .so natowa shukrani dha dhati kwa uwongozi wa kmkm kwa kumaliza soezi la usajil kati yangu.na wao na napenda kuwashukuru wote wapenzi wa kmkm ..kwa kuniunga mkono bamoja na uwongozi wa juu na nafurahi zaid kwa vile nipo nyumbani ..na famly yangu na biashara zangu za hapa na pale..asanten sana..watanzania wote .."
 

Arsenal Wenger asalimu amri, atangaza kuingia sokoni kusaka nyota

http://images.football365.com/12/11/800x600/Manchester-United-v-Arsenal-Arsene-Wenger-pa2_2855230.jpg 
LONDON, England
BAADA ya kuona mambo yanamwendea vibaya na hana njia nyingine ya kunusuru ajira yake Arsena, Kocha Arsene Wenger ametangaza kurejea sokoni kusaka wachezaji akitumia akiba aliyonayo ya Pauni Milioni 65.

Wenger ambaye kipigo cha mabao 3-1 toka kwa Aston Villa kimemweka pabaya mbele ya mashabiki wa klabu hiyo ya Emirates alitangaza uamuzi huo usiku wa kuamkia juzi.
 
Kocha huyo alisema kuwa bado anatafuta ufumbuzi mwingine na kwamba atazitumia fedha hizo kwa ajili ya kusaka nyota wengine kwenye michuano hiyo ya Ligi Kuu ya England.
 
Kwa sasa Gunners imeshatangaza dau la pauni milioni 12 ikimsaka kiungo wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Yohan Cabaye dau ambalo limekataliwa na  Newcastle ambayo inataka dau hilo liongezeke zaidi.

Hata hivyo kwa mujibu wa  Starsport klabu hiyo iliyokumbwa na mgogoro inawawinda nyota wengine watatu ambao huenda wakaigharimu pauni hizo milioni 65.

Wanaotajwa kuwa mawindo ya timu hiyo ni nyota wawili wa timu ya  Swansea, Michu na  Ashley Williams pamoja na nyota wa Manchester City, Micah Richards, ambaye mwenyewe binafsi anataka kujiunga na  Gunners.

Awali kabla ya kutangaza nyota hao, Arsenal  iliwahi kujaribu kurusha karata yake kuwashawishi nyota wengine kama  Luis Suarez, Wayne Rooney na  Gonzalo Higuain,lakini ikashindwa na badala yake kocha  Wenger akajikuta akikaliwa kooni na mashabiki kwa kushindwa kutumia fedha msimu huu.

Mfaransa huyo tayari ameshaomba radhi kwa mashabiki kufuatia kipigo cha  Aston Villa aliwatumia ujumbe wa barua pepe uliosomeka: 

"Tunataka mashabiki wetu wawe na furaha. Unaposhindwa kufikia mafanikio hayo ni lazima ujihisi mnyonge na mwenye kuchanganyikiwa. Watu wanadhani hatutaki kutumia fedha ila tunataka kuzitumia."

Waliochinja na kumnyofoa mtu viungo wanaswa Simiyu

Kamanda Msangi
Na Samwel Mwanga, Simiyu
JESHI la Polisi mkoani Simiyu limefanikiwa kuwatia mbaroni watu wawili wanaotuhumiwa kwa mauaji ya kikatili ya kumchinja mtu mmoja, kunyofoa na kumkata sehemu za siri na nyayo za mguu wake wa kushoto na kutoweka navyo.
Watu hao wanasadikiwa pia kushiriki katika mauaji ya kijana Mabula Hamisi (37) ambaye hapo awali hakufahamika jina, makazi wala umri wake Agosti 23, 2012 majira ya saa 2 usiku katika Kijiji cha Ikinabushu, Kata ya Gilya, Tarafa ya Dutwa, Wilaya ya Bariadi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Kamishina Msaidizi, Salumu Msangi aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Bamba Ndubiga (27), mkazi wa Kijiji cha Ngalamila, Wilaya ya Bariadi, na Marando Shaban (26) mfanyabiashara wa Kijiji cha Isuyu, Tarafa ya Dutwa pia wilayani humo.
Watuhumiwa wote hao walikamatwa juzi baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa ndio walikuwa na Mabula siku ya mwisho wakiwa wamepakizana katika pikipiki moja.


58 WAJITOSA UCHAGUZI TFF, BODI YA LIGI

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi4gRKoRzq365Nfvufupjmf66bFRq2WMCeqE3ufWX2EpKPbkI8uqn-u2DI0HfR82OR1wqctpyq68-QoUi3U-Wk7Z4Jp8gi7t3HJQohnWQ-A0Z_V6U2ENYrFSPHi1tMDtLGa3bnt3O_kcYs/s640/75502_562847213733654_1058456517_n.jpg
Jamal Malinzi kajitosa tena
Na Boniface Wambura
JUMLA ya wanamichezo 58 wamerusha fomu kuomba kuteuliwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na ule wa Bodi ya Ligi Kuu (TPL Board) utakaofanyika Oktoba mwaka huu.

Kwa upande wa TFF waliorejesha fomu kwa upande wa urais ni Athuman Jumanne Nyamlani, Jamal Emil Malinzi, Omari Mussa Nkwarulo na Richard Rukambura. Nafasi ya Makamu wa Rais wamejitokeza Imani Omari Madega, Nasib Ramadhan na Walace Karia.

Walioomba nafasi za ujumbe kuwakilisha kanda mbalimbali ni Abdallah Hussein Mussa, Kaliro Samson, Jumbe Odessa Magati, Mugisha Mujwahuzi Galibona, Vedastus Kalwizira Lufano, Samwel Nyalla, Epaphra Amana Swai, Mbasha Matutu Mong’ateko, Stanslaus Haroon Nyongo, Ally Mtumwa, Elley Simon Mbise na Omari Walii.

Ahmed Msafiri Mgoyi, Yusuf Hamisi Kitumbo, Ayoub Nyaulingo, Blassy Kiondo, Nazarius Kilungeja, Ayoub Shaib Nyenzi, Cyprian Charles Kuyava, David Lugenge, Elias Mwanjala, Eliud Peter Mvela, John Mwachendang’ombe Kiteve, James Patrick Mhagama, Kamwanga Rajabu Tambwe na Stanley William Lugenge.

Athuman Kambi, Francis Kumba Ndulane, Zafarani Damoder, Charles Komba, Hussein Mwamba, Stewart Ernest Masima, Farid Salum Nahdi, Geoffrey Nyange, Riziki Majala, Twahil Twaha Njoki, Davis Elisa Mosha na Khalid Abdallah Mohamed.

Wengine ni Alex Chrispine Kamuzelya, Juma Abbas Pinto, Muhsin Balhabou, Omar Isack Abdulkadir, Shaffih Dauda Kajuna na Wilfred Mzigama Kidao.

Kwa upande wa uchaguzi wa TFF mwombaji ambaye hakurudisha fomu ni Venance Mwamoto pekee.

Kwa upande wa TPL Board waliojitokeza kuwania uongozi wa juu ni wawili tu; Hamad Yahya Juma (Mwenyekiti) na Said Muhamad Said (Makamu Mwenyekiti).

Walioomba nafasi za ujumbe wa TPL Board ni Kazimoto Miraji Muzo, Michael Njunwensi Kaijage, Omari Khatibu Mwindadi, Salum Seif Rupia na Silas Masui Magunguma.
                         

Ramadhani Shauri, Cosmas Cheka kuwania mkanda wa UBO

Bondia Ramadhani Shauri kushoto akisaini mkataba wa kucheza ubingwa wa UBO utakaofanyika tarehe 27 mwezi wa 10 jijini Dar es salaam na mpinzani wake kushoto Cosmas Cheka wa Morogoro wengini ni Promota Kaike Silaju na Makamu Mwenyekiti wa PST Aga Peter nyuma
Bondia Cosmas Cheka wa Morogoro  akisaini mkataba wa kucheza ubingwa wa UBO utakaofanyika tarehe 27 mwezi wa 10 jijini Dar es salaam na mpinzani wake  Ramadhani Shauri kushoto wengini ni Promota Kaike Silaju na Makamu Mwenyekiti wa PST Aga Peter nyuma pamoja na kocha wa Cheka Power Iranda  
Promota wa Mpambano wa Ubingwa wa UBO Kaike Siraju katikati akiwanyoosha mikono juu mabondia Ramadhani Shauri kushoto na Cosmasi Cheka watakaopigana tarehe 27 jijini Dar es salaam
Bondia Ramadhani Shauri akizungumza na waandishi wa habari kushoto ni kocha wake Christopher Mzazi na Promota Kaike Siraju
Bondia Ramadhani Shauri akizungumza na waandishi wa habari
Bondia Cosmas Cheka akiongea na waandishi wa habari

TFF yamlilia Baraka Kitenge, ni baba wa Mtangazaji Maulid Kitenge

Mtangazaji Maulid Kitenge, aliyempoteza baba yake mzazi, Baraka Kitenge nyota wa zamani wa Yanga na Taifa Stars

Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu za Yanga na Taifa Stars, Baraka Kitenge (74) kilichotokea Agosti 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Kitenge akiwa mchezaji, alitoa mchango mkubwa kwa timu mbalimbali alizochezea, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
Kitenge amefia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo alikuwa amelazwa akisumbuliwa na kansa ya uti wa mgongo. Enzi zake katika Yanga na Taifa Stas alicheza na wachezaji kama akina Athuman Kilambo na Abdulrahman Juma.
TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Kitenge, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na klabu ya Yanga na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa Marehemu, Yombo Vituka (Jet) jijini Dar es Salaam. Mungu aiweke roho ya marehemu Kitenge mahali pema peponi. Amina
MICHARAZO inawapa pole wadau wote wa soka na hususan familia ya Baraka Kitenge kwa msiba uliowakumba, Allah SW awape subira na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu tukiwakumbusha kuwa Inna Lillah Waina Illah Rajiuun, kadhalika Washukurul Lillah Wal Kul Hal!