LONDON, England
BAADA ya kuona mambo yanamwendea vibaya na hana njia nyingine ya kunusuru ajira yake Arsena, Kocha Arsene Wenger ametangaza kurejea sokoni kusaka wachezaji akitumia akiba aliyonayo ya Pauni Milioni 65.
Wenger ambaye kipigo cha mabao 3-1 toka kwa Aston Villa kimemweka pabaya mbele ya mashabiki wa klabu hiyo ya Emirates alitangaza uamuzi huo usiku wa kuamkia juzi.
Kocha huyo alisema kuwa bado anatafuta ufumbuzi mwingine na kwamba atazitumia fedha hizo
kwa ajili ya kusaka nyota wengine kwenye michuano hiyo ya Ligi Kuu ya England.
Kwa sasa Gunners imeshatangaza dau
la pauni milioni 12 ikimsaka kiungo wa timu ya Taifa ya Ufaransa, Yohan Cabaye
dau ambalo limekataliwa na Newcastle
ambayo inataka dau hilo liongezeke zaidi.
Hata hivyo kwa mujibu wa Starsport klabu hiyo iliyokumbwa na mgogoro
inawawinda nyota wengine watatu ambao huenda wakaigharimu pauni hizo milioni
65.
Wanaotajwa kuwa mawindo ya timu hiyo
ni nyota wawili wa timu ya Swansea,
Michu na Ashley Williams pamoja na nyota
wa Manchester City, Micah Richards, ambaye mwenyewe binafsi anataka kujiunga
na Gunners.
Awali kabla ya kutangaza nyota hao,
Arsenal iliwahi kujaribu kurusha karata
yake kuwashawishi nyota wengine kama
Luis Suarez, Wayne Rooney na
Gonzalo Higuain,lakini ikashindwa na badala yake kocha Wenger akajikuta akikaliwa kooni na mashabiki
kwa kushindwa kutumia fedha msimu huu.
Mfaransa huyo tayari ameshaomba radhi kwa mashabiki kufuatia kipigo cha Aston Villa aliwatumia ujumbe wa barua pepe uliosomeka:
"Tunataka mashabiki wetu wawe na furaha. Unaposhindwa kufikia mafanikio hayo ni lazima ujihisi mnyonge na mwenye kuchanganyikiwa. Watu wanadhani hatutaki kutumia fedha ila tunataka kuzitumia."
No comments:
Post a Comment