STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, August 21, 2013

TFF yamlilia Baraka Kitenge, ni baba wa Mtangazaji Maulid Kitenge

Mtangazaji Maulid Kitenge, aliyempoteza baba yake mzazi, Baraka Kitenge nyota wa zamani wa Yanga na Taifa Stars

Na Boniface Wambura
SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu za Yanga na Taifa Stars, Baraka Kitenge (74) kilichotokea Agosti 20 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Msiba huo ni mkubwa kwa wadau wa mpira wa miguu kwani kwa nyakati tofauti Kitenge akiwa mchezaji, alitoa mchango mkubwa kwa timu mbalimbali alizochezea, hivyo mchango wake tutaukumbuka daima.
Kitenge amefia Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo alikuwa amelazwa akisumbuliwa na kansa ya uti wa mgongo. Enzi zake katika Yanga na Taifa Stas alicheza na wachezaji kama akina Athuman Kilambo na Abdulrahman Juma.
TFF inatoa pole kwa familia ya marehemu Kitenge, Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na klabu ya Yanga na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.
Mipango ya mazishi inafanywa nyumbani kwa Marehemu, Yombo Vituka (Jet) jijini Dar es Salaam. Mungu aiweke roho ya marehemu Kitenge mahali pema peponi. Amina
MICHARAZO inawapa pole wadau wote wa soka na hususan familia ya Baraka Kitenge kwa msiba uliowakumba, Allah SW awape subira na moyo wa uvumilivu katika kipindi hiki kigumu tukiwakumbusha kuwa Inna Lillah Waina Illah Rajiuun, kadhalika Washukurul Lillah Wal Kul Hal!

No comments:

Post a Comment