STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, August 21, 2013

Waliochinja na kumnyofoa mtu viungo wanaswa Simiyu

Kamanda Msangi
Na Samwel Mwanga, Simiyu
JESHI la Polisi mkoani Simiyu limefanikiwa kuwatia mbaroni watu wawili wanaotuhumiwa kwa mauaji ya kikatili ya kumchinja mtu mmoja, kunyofoa na kumkata sehemu za siri na nyayo za mguu wake wa kushoto na kutoweka navyo.
Watu hao wanasadikiwa pia kushiriki katika mauaji ya kijana Mabula Hamisi (37) ambaye hapo awali hakufahamika jina, makazi wala umri wake Agosti 23, 2012 majira ya saa 2 usiku katika Kijiji cha Ikinabushu, Kata ya Gilya, Tarafa ya Dutwa, Wilaya ya Bariadi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Simiyu, Kamishina Msaidizi, Salumu Msangi aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Bamba Ndubiga (27), mkazi wa Kijiji cha Ngalamila, Wilaya ya Bariadi, na Marando Shaban (26) mfanyabiashara wa Kijiji cha Isuyu, Tarafa ya Dutwa pia wilayani humo.
Watuhumiwa wote hao walikamatwa juzi baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa ndio walikuwa na Mabula siku ya mwisho wakiwa wamepakizana katika pikipiki moja.


No comments:

Post a Comment