NA MWANDISHI WETU
UMOJA wa Wanafunzi wa Kiislam Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MSAM) kilichopo Kigamboni  Jijini  Dar es Salaam unaomba wadau mbalimbali kujitokeza katika mahafali ya kuwaaga wanafunzi wa kiislam wanaomaliza chuo ambayo yataambatana na harambee ya uchangiaji  wa fedha za ujenzi wa msikiti chuoni hapo.
Ombi hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa MSAM Abdullatif Jafari wakati akizungumza na mwandishi wa habari hivi karibuni Jijini Dar es Salaam.
Jafari alisema chuo kimewapa  ruhusa ya kutafuta mdhamini wa ujenzi wa msikiti kwa kipindi kirefu ila hadi sasa hawajapata mafanikio kwani baadhi ya wahisani wamekuwa wakiaahidi bila mafanikio pamoja na ukweli kwamba MSAM imekuwa ikiteleza maagizo yao kila wanapohitaji.
Alisema matarajio yao ni kuhakikisha kuwa wanapata kiasi cha shilingi milioni mia moja za kuanzia ujenzi hivyo basi wanaaomba watu wenye nia nzuri kwa vijana wa kiislam wanaoishi maeneo ya chuo waweze kufanikisha zoezi hilo mapema.
Katibu huyo alisema wanafunzi wamekuwa wakichanga mara kwa mara ila juhudi zao zimekwama hivyo wanaomba mtu, taasisi yoyote yenye uweze kuwasaidia ujenzi wa msikiti huo ili waweze kumuabudu mungu kwa amani na kwa wakati.
’’Jumamosi ijayo tunawaaga wenzetu wanaomaliza hivyo basi tunataka kutumia fursa hiyo kuweza kuchangisha fedha za ujunzi wa msikiti nadhani nao watakuwa wameacha alama Fulani katika haarakati hizi’’, alisema.
Jafari alisema iwapo tutapata ushirikiano kutoka kwa wadau mabalimbali nchini tunaamini kuwa upo uwezekano mkubwa wa kufanikisha zoezi hilo mapema na dhana ya kufikiria mtu mmoja tutaondokana nayo.
Alisema ni vema jamii ikatambua kuwa kufanikisha ujenzi huo itakuwa imechangia msaada mkubwa katika kujenga imani na maadili ya vijana ambao wanasoma katika chuo hicho cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni.
Aidha Katibu huyo alitoa rai kwa wale wote wenye nia ya kuchangia ujenzi huo wa msikiti na hawataweza kufika wanaweza kutoa michango yaao kwa njia za M Pesa 0766656730, Tigo Pesa 0713774828 au akaunti namba ya jumuiya Muslim Students Association of Mwalimu Nyerere (MSAM) 3300825636 Kenya Commercial Bank Samora Avenue.