STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Saturday, May 18, 2013

Redd's Miss Bagamoyo 2013 kufanyika Mei 24

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiiTkXB_wLHpzsqQ905DvOw1PsYZJNU3Ck8iLgJFN1ZnUWcUQqOMWOIhW8at7WeZnDFjQvkb5NMknVzRipc0RkeX1K4Qgw4_o_DKoNowHCFhbIz1EMhJtfFwNdhQty1eZMVrGlXQv3L2xo/s1600/ROSE+MIS+REDDS.jpg
Rose Lucas, Mshindi wa shindano la Redd's Miss Bagamoyo 2012
JUMLA ya warembo 10 wanatarajiwa kuchuana kwenye shindano la kuwania taji la urembo la mji wa Bagamoyo 'Redd's Miss Bagamoyo 2013' litakalofanyika Mei 24 kwenye ukumbi wa TaSUBA, Bagamoyo.
Mratibu wa shindano hilo ambaye pia ni Mkurugenzi wa kampuni ya Asilia Decoration, Awetu Salim aliiambia MICHARAZO alisema kambi ya mazoezi kwa warembo hao inaendelea mjini humo na kwamba maandalizi kwa ujumla yamekamilika na anatarajiwa fainali za mwaka huu kuwa za aina yake.
Anasema hii inatokana na warembo waliojitokeza safari hii ambao alidai ni vimwana haswa wenye sifa na vigezo vyote na kuwataka mashabiki wa fani hiyo kujitokeza kwa wingi kuhudhuria.
Awetu aliongeza kuwa katika kusindikiza shindano hilo siku hiyo ukumbi kutakuwa na burudani mbalimbali za muziki na ngoma asilia toka kwa wasanii na makundi tofauti akiwamo mwanadada Aisha Ramadhani a.k.a Isha Mashauzi na bendi yake ya Mashauzi classic, muziki wa kizazi kipya kutoka kwa Chuo cha Sanaa(tasuba), ngoma ya kabila la wakwere wenyeji wa Bagamoyo na nyinginezo.

No comments:

Post a Comment