STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, March 14, 2013

TFF SASA YAWATULIZA WADAU WA SOKA



Na Boniface Wambura
RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) amewataka wadau wa mchezo huo kuwa watulivu kwa vile tofauti zilizojitokeza kati ya Shirikisho na Serikali zitamalizwa kwa taratibu za mpira wa miguu.

Amesema nia ya TFF ni kuhakikisha Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) haliifungii Tanzania kwani tayari Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangara alishaahidi kuwepo kikao kati yake na viongozi wa TFF kitakachofanyika Jumanne (Machi 19 mwaka huu).

“Suluhu itapatikana kwa mazungumzo kati ya Wizara na TFF. Naamini suala hili tutalimaliza baada ya kikao cha Machi 19 ambacho kimepangwa na Waziri kutokana na maombi ya TFF,” amesema Rais Tenga na kuongeza kuwa tatizo lilianzia kwenye mchakato wa uchaguzi ambao umesimamishwa na FIFA.

FIFA ilisimamisha Mkutano Mkuu wa uchaguzi baada ya baadhi ya wagombea walioenguliwa kulalamika, na yenyewe kuahidi kutuma ujumbe wa kushughulikia suala hilo.

Rais Tenga amesema lisingetokea tatizo hilo, TFF tayari ilishaitisha Mkutano Mkuu ambao ungefuatiwa na uchaguzi. Lakini kwa vile FIFA ndiyo iliyosimamisha mkutano huo, TFF inalazimika kusubiri hadi FIFA itakaposhughulikia suala hilo na kutoa maelekezo ikiwemo lini mkutano ufanyike.

Amesema kwa kuamini tatizo hilo litamalizwa ndani ndiyo maana TFF hadi sasa haijapeleka FIFA maagizo ya Waziri Dk. Fenella ya kutengua marekebisho ya Katiba ya TFF ya mwaka 2012, kuitisha Mkutano Mkuu wa marekebisho ya Katiba na Mkutano Mkuu wa Uchaguzi, kwani ingefanya hivyo Tanzania ingefungiwa mara moja.

TFF inasisitiza kuwa FIFA ilijua tatizo la Serikali kutoa maagizo kwake kupitia vyombo vya habari, hivyo kumuandikia Rais Tenga na kueleza msimamo wake iwapo itabainika kuwa Serikali imekuwa ikiingilia uendeshaji wa shughuli za mpira wa miguu.

Uhalali wa kuwepo kwa barua ya FIFA kwenda kwa Rais Tenga juu ya suala hilo ulihojiwa pia na mwandishi wa Reuters, Brian Homewood baada ya kusoma kupitia vyombo vya habari nchini kuwa Shirikisho hilo huenda likaifungia Tanzania ikibainika Serikali inaingilia shughuli za TFF. Mawasiliano kati ya FIFA na mwandishi huyo ambapo majibu yake pia TFF ilipewa nakala yameambatanishwa katika taarifa hii.

Viambatisho:
Forwarded Message -----
From: Media Office (FIFA) <media@fifa.org>
To: Brian Homewood <brian.homewood@yahoo.co.uk>
Sent: Tuesday, 12 March 2013, 19:39
Subject: RE: tanzania

Dear Brian,

Thanks for your message.

We can confirm that FIFA Secretary General Jérôme Valcke has sent a letter to the President of the Tanzanian Football Federation, Leodegar Tenga, concerning alleged governmental interference in the internal affairs of the TFF.

FIFA is in contact with the TFF President who is optimistic that the matter can be sorted out within TFF, FIFA and the Tanzanian authorities. Furthermore, we can confirm that FIFA is also planning to send a mission to assess the situation with regard to the electoral process as soon as the current matter of alleged interference has been clarified.

Kind regards

FIFA
Media department
Enquiries: media@fifa.org
Tel.: +41-(0)43-222 7272    www.FIFA.com
Twitter: @fifamedia    YouTube/FIFAtv

-----Original Message-----
From: Brian Homewood [mailto:brian.homewood@yahoo.co.uk]
Sent: Dienstag, 12. März 2013 10:19
To: Media Office (FIFA)
Subject: tanzania



Good morning

Are you able to comment on reports (below) that FIFA has sent a warning to Tanzania over government interference in the national football federation?

Many thanks

Kind regards

Brian Homewood

Reuters

By Majuto Omary
The Citizen Reporter
Dar es Salaam. Fifa has threatened to suspend Tanzania from all international competitions if the tug-of-war between the Tanzania Football Federation (TFF) and government does not end in a meaningful way. In a letter to the TFF, the world soccer governing body warned yesterday that it would not hesitate to impose a ban on the country if it confirms that the government interferes with the operations of the federation.

Fifa says there have been various reports of accusations by local media that the ministry of Information, Culture and Sports has interfered with the operations of the TFF.

The letter has quoted the minister responsible for sports, Fenella Mukangara, as saying that the government has urged the TFF to use the
2006 constitution in this year's election, while it 'has already been amended.'
"It has been reported that the TFF has been urged to organise the General Assembly and the elections by the date set by the government,"
reads the letter signed by Fifa secretary general Jerome Valcke.

It further reads: "It is also said that government intends to establish an interim committee if the TFF fails to undertake the orders."

Fifa says if the accusations reported by the local media shall be established to be true, it means the government is interfering with the operations of TFF.

"We would like to remind all members of Fifa that they are required to conduct their activities freely without interference by another person as defined in Articles 13 and 17 of the Constitution of Fifa."

"So if these instructions issued by the government will be implemented, this issue will be taken to the top Fifa authorities for further action, including suspension of Tanzania as it becomes when there is a government intervention," says the letter.

A copy of the letter has been sent to the Confederation of African Football (Caf) reiterating some of the penalties that Tanzania will face if it is suspended.

Golden Bush kurudiana na watoto wao Jumamosi

Timu ya vijana ya Golden Bush wakiwa na makocha wao ambao baadhi ya wachezaji wa Golden Bush Veterani

 WAKALI wa soka la wazee jijini Dar, Golden Bush Veterani keshokutwa wanatarajia kushuka dimba la Kinesi kumenyana na vijana wao Golden Bush Fc inayoshiriki Ligi Daraja la Nne Wilaya ya Kinondoni.
Pambano hilo ni la marudiano kwa timu hizo baada ya wiki iliyopita vijana hao kuwagaragaza wazee kwa mabao 2-1 katika mechi iliyokuwa na upinzani mkali.
Mlezi wa klabu hizo 'ndugu', Onesmo Waziri 'Ticotico' aliiambia MICHARAZO kwamba mechi hiyo inatarajiwa kuwa ya aina yake kutokana na veterani kupania kulipa kisasi baa ya kunyukwa mechi ya awali.
"Tunatarajiwa kushuka dimbani siku ya jumamosi dhidi ya vijana wetu, Golden Bush Fc ambao walitunyuka mabao 2-1 katika mechi ya awali. Hilo ni pambano litakalosaidia kutuweka vema kabla ya kuvaana na wapinzani wetu, Wahenga Fc," alisema Ticotico.
Ticotico ambaye ni mmoja wa nyota wa timu ya Veterani, alisema pambano lao na Wahenga litachezwa sikukuu ya Pasaka mwishoni mwa mwezi huu.
Timu hizo zimeshakutana mpaka sasa mara tatu, ambapo kila timu imeshinda mechi moja kwa idadi ya mabao 4 na kutoka sare ya bao 1-1 katika pamoja jingine, hivyo mechi ijayo ni ya kukata mzizi wa fitina kuona nani zaidi kati yao.

Irene Paul amtoa Kalunde wake hadharani

Micharazomitupu
Msanii Irene Paul 'Brown Eyes' akiwa katika pozi

MSANII anayezidi kukimbiza katika fani ya filamu nchini, Irene Paul amekamilisha filamu yake mpya iitwayo 'Kalunde'.
Akizungumza na MICHARAZO,  Irene alisema filamu hiyo aliyoigiza na wasanii kadhaa nyota aliitarajia kuiachia mtaani kesho Ijumaa baada ya kuikabidhi kwa wasambazaji wake.
Irene alisema hiyo ni kazi yake ya kwanza tangu atumbukie kwenye fani hiyo miaka mitatu iliyopita akiachana na fani ya utangazaji aliyokuwa akiifanya katika vituo viwili kwa nyakati tofauti.
"Nimekamilisha filamu yangu ya kwanza iitwayo 'Kalunde' na ninatarajia kuiachia kwa mashabiki Machi 15," alisema Irene.
Mwanadada huyo aliyecheza filamu kadhaa kama 'Unpredictable', 'Handsome wa Kijiji', I Hate My Birthday, The Shell, Triple L, Fikra Zangu na Shujaa, alisema wakati 'Kalunde' ikiingia mtaani tayari yupo katika maandalizi ya kufyatua filamu nyingine binafsi, ambayo hata hivyo hakupenda kuitaja jina kwa sasa.
"Yaani kwa sasa ni bandika bandua, baada ya Kalunde mashabiki wangu wakae tayari kupata kitu kingine kipya muda si mrefu," alisema Irene.

Shaa sasa awageukia wenye nyumba

Msanii Sarah Kais 'Shaa' katika pozi
WAKATI ngoma yake iitwayo 'Promise' ikiendelea kutamba kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga, msanii mkali wa kike nchini, Sarah Kais 'Shaa' amefyatua wimbo mpya uitwao 'Baba Kodi'.
Wimbo huo mpya wa Shaa, nyota wa zamani wa kundi washindi wa Coca Cola Pop Star,  Wakilisha, unatarajiwa kuanza kusambazwa rasmi kesho Ijumaa wakati video yake ikifanyiwa mipango.
Mmoja wa wasimamizi wa kazi za msanii huyo, Said Fella, aliiambia MICHARAZO kwamba wimbo huo mpya umerekodiwa katika studio za AM Records chini ya mtaalam Maneke.
Fella alisema ndani ya wimbo huo, Shaa anaelezea visa vya baadhi ya wenye nyumba wakati wa kudai kodi zao bila ustaarabu.
"Ni moja ya nyimbo zitakazobamba sana kwa namna Shaa alivyofanya kazi kubwa na ujumbe uliopo ambao ni simulizi za kweli zinazowapa wapangaji wakati wakidai kodi na wenye nyumba zao ambao hukosa ustaarabu," alisema Fella.
Shaa mwenyewe alisema kutoia kwake wimbo huo ni muendelezo wa ahadi yake ya kuwapa burudani mashabiki wake waliomkosa kwa muda mrefu baada ya kukaa kimya tangu alipoachia wimbo wake mpya mapema mwaka jana.
Wimbo huo ni wa pili kwa msanii huyo aliyewahi kuwania tuzo ya MTV 2009 mbali na wimbo wake kunyakua tuzo ya Kili Music Award, baada ya awali kutoa 'Promise'.

Mashabiki Man U, Real wachapana risasi Dar

Timu za Real Madrid na Manchester zilizoumana hivi karibuni na kupelekea mashabiki wa soka nchini kutwangana  risasi


NI kama hadithi lakini huu ndiyo ukweli; soka limekuwa likiibua hisia kali miongoni mwa wanaolifuatilia kiasi cha baadhi ya mashabiki kufikia hatua ya kujiua ama kusababisha maafa kwa wengine!
Ubishani wa soka baina ya mashabiki wa klabu za Manchester United ya England na Real Madrid ya Hispania umezua balaa la aina yake katika eneo la Sinza Kumekucha jijini Dar es Salaam baada ya mmoja wa mashabiki hao kumtwanga risasi mwenzake wakati wakifuatilia kupitia luninga mechi ya marudiano ya hatua ya 16-bora ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ambapo Real iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Saam jana, Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Charles Kenyela, alisema kuwa shabiki wa soka aliyepigwa risasi na kujeruhiwa mkononi ni David Kweka (32) na anayedaiwa kumpiga risasi ni shabiki mwingine wa soka aitwaye Robert Wambura.
Kamanda Kenyela alisema kuwa tukio hilo lilitokea Jumanne iliyopita wakati wawili hao walipokuwa wakifuatilia mechi kati ya Manchester United na Real Madrid iliyoanza saa 4:45 usiku (kwa saa za Tanzania).
Aliongeza kuwa majeruhi (Kweka) aliumia baada ya kupigwa risasi katika kiganja chake cha mkono wa kulia na Wambura ambaye anamiliki silaha hiyo kihalali, chanzo kikitajwa kuwa ni mabishano makali kati yao kuhusiana na mechi hiyo.
Alisema kuwa jeshi hilo linamshikilia Wambura na silaha iliyotumika na kwamba muda wowote (kuanzia jana) atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomakabili.
“Ni jukumu la Jeshi la Polisi kuhakikisha kwamba tunaweka ulinzi katika maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi, hivyo tumejipanga kukabiliana na matukio kama hayo yanayotokea katika maeneo mbalimbali, hasa katika maeneo wanayoonyesha mpira ili kuondokana na ushabiki unaoleta madhara,” alisema Kenyela.
Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Old Traford, England, wenyeji Manchester United walichapwa 2-1 na magoli ya Real inayoongozwa na kocha Jose Mourinho yalifungwa na Luka Modric na Cristiano Ronaldo huku goli pekee la Man U likitokana na kujifunga kwa beki Sergio Ramos wa Real.
Matokeo hayo yaliipa nafasi Real kutinga robo fainali kwa jumla ya magoli 3-2 kwani katika mechi yao ya kwanza iliyochezwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu nchini Hispania, timu hizo zilitoka sare ya 1-1.


CHANZO: NIPASHE

Arsenal yang'oka Ulaya, Malaga yaisulubu Porto

Mfungaji wa bao la pili la Arsenal, Laurent Koscielny (kulia) akiwa haamini kama wametoka michuano ya UIaya
 LICHA ya kupata ushindi uliotarajiwa wa mabao 2-0 ugenini nchini Ujerumani, Arsenal ya Uingereza imejikuta ikishindwa kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana.
Arsenal ilikuwa nchini humo kukabiliana na wenyeji wao Bayern Munich ikiwa nyuma ya mabao 3-1 iliyonyukwa katika pambano lao la awali lililochezwa mjini Londoni mwishoni mwa mwezi uliopita.
Ushindi huo uliotokana na mabao ya Olivier Giroud aliyefunga dakika ya tatu tu ya kuanza kwa mchezo huo na lile la kipindi cha pili lililotumbukizwa wavuni na Laurent Kocsielny, ulifanya matokeo ya mwisho kuwa sare ya mabao 3-3, lakini vijana hao wa Arsene Wenger kung'oka kwa faida ya bao ya ugenini.
Tofauti na mechi yao ya London, Arsenal jana walionyesha uhai na kuwafunika wenyeji wao na kuwashutukiza kwa bao hilo la mapema la Giroud lililodumu hadi wakati wa mapumziko.
Arsenal ilisubiri hadi dakika nne kabla ya kumalizika kwa pambano hilo kuongeza bao la pili kupitia kwa Laurent Koscielny aliyefunga kwa kichwa ambalo hata hivyo halikusaidia kusonga mbele ili kukaribia ndoto zao za kumaliza ukame wa mataji klabuni hapo.
Michuano hiyo ndiyo iliyokuwa tumaini pekee la Arsenal kumaliza ukame huo wa mataji kwani ilishatolewa kwenye michuano ya Kombe la Ligi, Kombe la FA na ndoto za kutwaa ubingwa wa Ligi ya England ni finyu kutokana na ukweli imeachwa mbali kipointi na vinara wa ligi hiyo, Manchester United.
Katiika mechi nyingine ya usiku wa jana katika michuano hiyo ya Ulaya, Malaga ya Hispania ikiwa nyumbani ililipa kisasi cha kunyukwa na Porto ya Ureno bao 1-0 kwa kuilaza wageni wao hao mabao 2-0 na kutinga robo fainali.
Malaga ilipata mabao yake kila kipindi kupitia kwa nyota wake, Isco aliyefunga la kwanza dakika ya 43 na Roque Santa Cruz kuonyesha la pili katika dakika ya 77 na kuifanya timu hiyo sasa kuungana na timu za Barcelona na Real Madrid kutoka Hispania, Borussia Dotmund na Bayern Munich za Ujerumani, PSG ya Ufaransa na Galatasaray ya Uturuki kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.