STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Thursday, March 14, 2013

Shaa sasa awageukia wenye nyumba

Msanii Sarah Kais 'Shaa' katika pozi
WAKATI ngoma yake iitwayo 'Promise' ikiendelea kutamba kwenye vituo mbalimbali vya redio na runinga, msanii mkali wa kike nchini, Sarah Kais 'Shaa' amefyatua wimbo mpya uitwao 'Baba Kodi'.
Wimbo huo mpya wa Shaa, nyota wa zamani wa kundi washindi wa Coca Cola Pop Star,  Wakilisha, unatarajiwa kuanza kusambazwa rasmi kesho Ijumaa wakati video yake ikifanyiwa mipango.
Mmoja wa wasimamizi wa kazi za msanii huyo, Said Fella, aliiambia MICHARAZO kwamba wimbo huo mpya umerekodiwa katika studio za AM Records chini ya mtaalam Maneke.
Fella alisema ndani ya wimbo huo, Shaa anaelezea visa vya baadhi ya wenye nyumba wakati wa kudai kodi zao bila ustaarabu.
"Ni moja ya nyimbo zitakazobamba sana kwa namna Shaa alivyofanya kazi kubwa na ujumbe uliopo ambao ni simulizi za kweli zinazowapa wapangaji wakati wakidai kodi na wenye nyumba zao ambao hukosa ustaarabu," alisema Fella.
Shaa mwenyewe alisema kutoia kwake wimbo huo ni muendelezo wa ahadi yake ya kuwapa burudani mashabiki wake waliomkosa kwa muda mrefu baada ya kukaa kimya tangu alipoachia wimbo wake mpya mapema mwaka jana.
Wimbo huo ni wa pili kwa msanii huyo aliyewahi kuwania tuzo ya MTV 2009 mbali na wimbo wake kunyakua tuzo ya Kili Music Award, baada ya awali kutoa 'Promise'.

No comments:

Post a Comment