STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, November 20, 2013

Majeruhi wa risasi wivu wa mapenzi aaga dunia

MAJERUHI Francis Shumira aliyejeruhiwa katika tukio la kushambuliwa kwa risasi Ilala Dar es salaam jana amefariki dunia leo asubuhi Hospitali ya Muhimbili alikolazwa MOI kwa matibabu.
Kufariki kwa Francis kunafanya idadi ya watu waliofariki katika tukio hilo hadi hivi sasa huku ikiacha majeruhi wawili mmoja Christina Alfred Newa Mwanafunzi wa masuala ya Mawasiliano visiwa vya Syprus na mama mzazi wa Christina, Hellen Elieza Newa.
Aidha mipango ya mazishi ya mtumishi wa Benki ya Barclays ya jijini Dar es Salaam, Alfa Alfred Newa inafanyika nyumbani kwao Ilala karibu na Kablu ya wazee huku maziko yakisubiri kutengemaa kwa afya ya mama mzazi.
familia imekiri kuwa Christina na Marehemu Munisi walikuwa na mahusiano lakini ni zamani na walitengana kutokana na vurugu alizowahi mfanyia siku za nyuma. 
IKUMBUKWE Tukio la shambulizi la risasi lililotokea hii Novemba 19, 2013  asubuhi Ilala Amana jirani na Hoteli ya MM na Klabu maarufu ya wazee limesababisha vifo vya watu wawili na kuacha majeruhi watatu wawili kati yao wakiwa taabani.
Taarifa za awali za Polisi zinapasha kuwa, Watu walio poteza maisha katika tukio hilo ambalo lilikuwa ni la mtu aliyetambulika kwa jila la Godfrey Munisi kuwapiga risasi wana familia lilisababisha kifo cha Alfa Alfred na liliwajeruhi Francis Khiranga Shumira , Christina Alfred, Hellen Elieza Newa.
Taarifa hizo zinasema kuwa Mfyatua risasi huyo ambaye baade alijiua nayeye, Godfrey Munisi alikuwa na uhusiano wa karibu na Christina Alfred Newa. 
Katika tukio hilo, ambalo linaelezwa kuto tofautiana sana na lile la Mwanahabari ufoo Saro lililotokea miezi ya hivi karibuni, muuaji alimjeruhi Nshumila kifuani  na mama yake Christina  alijeruhiwa maeneo ya begani na hali zao siyo nzuri na wamelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Huku Christina akijeruhiwa mkononi na mguuni ambapo alitibiwa katika Hospitali ya Amana na Kuruhusiwa kurudi nyumbani huku mdogo wa Christina, Alfa Alfred akifariki kabla ya kufikishwa Hospitali.
Marehemu Alfa Alfred Newa pia alikuwa wa benki ya Barclays  ya jijini Dar es Salaam. Shumira ni baharia kitaaluma na inaelezwa kuwa ni raia wa Kenya.

Father Kidevu

Coastal yamsubiri Chippo kusajili dirisha dogo

Yusuph Chippo
MABINGWA wa zamani wa kandanda nchini, Coastal Union ya Tanga imesema haitakurupuka kufanya usajili katika dirisha dogo mpaka ipate maelekezo kutoka kwa kocha wao mpya, Mkenya Yusuf Chippo.
Aidha klabu hiyo imesema mpaka sasa haijapata taarifa zozote toka Simba juu ya kumrejesha kiungo wao, Uhuru Suleiman aliyekuwa akiichezea Coastal kwa mkopo katika duru la kwanza la Ligi Kuu Tanzania Bara.
Afisa Habari wa Coastal Union, Hafidh Kido, aliiambia MICHARAZO kuwa, ili kuepuka kufanya majukumu yasiyo yao, wameamua kumsubiri kocha wao mpya kuamua kwenye dirisha dogo kama atataka mchezaji mpya au la badala ya uongozi kukurupuka kulifanya zoezi hilo.
Kido alisema Chippo ambaye alikuwepo kushuhudia pambano la kufungia dimba la duru la kwanza kati ya Coastal na JKT Ruvu, ndiye mwenyewe jukumu la kuuelekeza uongozi kipi kifanyike katika dirisha dogo.
Alisema kwa vile hajapata muda wa kukaa na kuwafahamu wachezaji, viongozi wameamua kuiita mapema timu hiyo kambi ya mazoezi Desemba 2 ili kumpa wasaa kocha wao kujipanga upya kuanza kuinoa timu.
"Kambi ya mazoezi ya Coastal itaanza Desemba 2, lengo ni kutaka kumpa muda mzuri kocha wetu kuwasoma wachezaji na kama atabaini mapungufu katika idara za kikosi chake ndipo atapendekeza na sisi tutamsaidia kumtafutia mchezaji anayemtaka kwa nafasi anayotaka irekebishwe," alisema Kido.
Aliongeza baada ya kocha huyo kupata muda wa kukiangalia kikosi chake watamtafutia mechi za kirafiki za kujipima nguvu zitakazochezwa ndani na nje ya nchi kabla ya kuikabili Ligi Kuu duru la pili litakaloanza Januria 25.
Aidha klabu hiyo imesema haijapata  taarifa rasmi juu ya kurejea katika klabu ya Simba kiungo Uhuru Suleiman aliyekuwa akiichezea timu hiyo kwa mkopo, ingawa imesema haiwezi kumng'ang'ania mchezaji huyo.
Uhuru alinukuliwa kuwa ameamua kurejea Simba kumaliza mkataba wake na uongozi wa Simba kuthibitisha hilo, lakini Coastal wanasema haijapatiwa taarifa rasmi.
Coastal iliyomaliza duru la kwanza katika nafasi ya saba, iliachana na aliyekuwa kocha wake, Hemed Morocco aliyemaliza mkataba na kuamua kumnyakua Chippo aliyewahi kuzinoa Bandari-Mombasa, Nzoia, aliwahi  Mkurugenzi wa Ufundi (TD) wa Ulinzi na kuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa la Kenya, Harambee Stars.

Mbivu na mbichi CHADEMA kujulikana leo Kamati Kuu ikikutana

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), leo inaanza kikao chake cha siku mbili ikitarajiwa kujadili masuala mazito, hasa misukosuko iliyokikumba katika siku za karibuni.
Taarifa iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema, John Mnyika ilisema kikao hicho kitakachofanyika Dar es Salaam kitapokea, kujadili na kufanya uamuzi wa masuala mbalimbali ikiwamo hali ya siasa na ripoti ya fedha.
“Suala mojawapo litakuwa kujadili mihutasari ya mikutano iliyopita na yatokanayo na mikutano hiyo, taarifa ya hali ya siasa na ripoti ya fedha,” ilisema taarifa hiyo ya Mnyika, ambaye yuko ziara ya kikazi huko Uturuki.
Pia utajadili mchakato na maudhui ya mabadiliko ya katiba, taarifa ya utekelezaji wa Programu ya Chadema ni Msingi na shughuli za kanda na taarifa ya utekelezaji wa Mpango Mkakati kuhusu maboresho.

Chadema katika mawimbi makali
Miongoni mwa mambo ambayo yanatarajiwa kujadiliwa katika kikao hicho ni mustakabali wake katika kipindi hiki ambacho kinapita katika mawimbi makali kutokana na kuibuka kwa malumbano ya waziwazi baina ya viongozi wake waandamizi na pia kusimamishwa kwa baadhi ya viongozi wa mikoani.
Matukio ya karibuni yanajumuisha malumbano kati ya Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema kuhusiana na masuala ya posho, kusimamishwa kwa Mwenyekiti wa Chadema wa Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba, kuvunjwa kwa uongozi wa Mkoa wa Mara na pia kuondolewa kikaoni kwa Mbunge wa Maswa Magharibi, John Shibuda.
Wafuatiliaji wa mambo ya siasa watakuwa wanakitazama kikao hiki kama fursa ya kuweka sawa mambo ili kiendelee kutoa ushindani kwa chama tawala.
Alipoulizwa kama matukio ya hivi karibuni yatajadiliwa katika kikao hicho, Mnyika alikataa kuingia kwa undani na badala yake alisema taarifa zitatolewa baada ya kikao.
“Niko nje ya nchi, mengine utapewa majibu kesho (leo) kwa yale ambayo yatakuwepo katika taarifa zitakazowasilishwa. Yale ambayo hayatakuwepo utajulishwa pia iwapo hayatajadiliwa,” alisema Mnyika.

Zitto na Lema
Zitto na Lema waliingia katika vita ya maneno mwanzoni mwa Novemba kuhusiana na masuala ya posho ya vikao.
Vita hiyo ilianzishwa na Lema katika kikao cha wabunge wiki iliyopita aliposema kuwa Zitto anafanya unafiki kukataa posho.
Lema alimtuhumu Mbunge huyo wa Kigoma Kaskazini kwamba anakataa posho za vikao bungeni, lakini anapokea posho nyingi kutoka mashirika mbalimbali ya kijamii nchini.
Lema aliweka tuhuma hizo kwenye Mtandao wa Jamii Forum huku akisema suala hilo halihitaji vikao vya chama kulijadili isipokuwa vyombo vya habari na hususan, mitandao ya kijamii kwani hata Zitto hutumia mitandao hiyo.
Akijibu hoja hizo, Zitto alisema tangu siku nyingi alikwisha piga marufuku kwenye Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) kupokea posho kutoka taasisi au mashirika yanayosimamiwa na kamati hiyo.
Alisema tangu alipokuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma(POAC), alipiga marufuku posho na pia aliwahi kuwashtaki Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) wabunge wanaochukua posho kutoka taasisi za Serikali.

Ripoti kuhusu Zitto mtandaoni
Zitto pia alipata msukosuko mwingine baada ya kusambazwa ripoti inayoitwa ‘Taarifa ya Siri ya Chadema’ iliyomtuhumu kuwa alikuwa anashirikiana na CCM na viongozi wa Idara ya Usalama wa Taifa kuhujumu chama hicho.
Ripoti hiyo inayodaiwa kuwa iliandaliwa na Idara ya Upelelezi ya Chadema, ilieleza kuwa Zitto alikuwa akipokea fedha kutoka kwa maofisa wa usalama na kuzisambaza kwa makada wengine wa chama hicho ili wafanye kazi ya kukihujumu.
Hata hivyo, Chadema kupitia kwa Mnyika ilitoa taarifa kupinga vikali suala hilo.

CAG kukagua ruzuku
Pia, Zitto aliingia katika malumbano na chama chake baada ya kutuhumu vyama vya siasa kuwa hesabu zake hazikaguliwi na CAG.
Chadema ilipinga vikali madai hayo na kueleza kuwa imekuwa inatumia taasisi binafsi kufanya kazi hiyo.

Mwigamba, Shibuda na uongozi Mara
Suala jingine linalotazamiwa kujadiliwa katika kikao hicho ni kusimamishwa kwa Mwigamba na Baraza la Uongozi Kanda ya Kaskazini ambako kulizuka vurugu kiasi cha kunyang’anywa kompyuta mpakato (laptop) baada ya kudaiwa alikuwa anasambaza taarifa za kuhujumu chama hicho.
Suala lake linasubiri uamuzi wa kikao cha Kamati Kuu kama lile la kuvunjwa kwa uongozi wa Chadema wa Mara.
Pia kitendo cha Baraza la Kanda ya Ziwa Mashariki kumtimua Shibuda kwa madai kwamba halina imani naye nacho kina uwezekano mkubwa wa kujadiliwa.

Mapinduzi Simba! Rage, Kibadeni, Julio wafurushwa Msimbazi

Mwenyekiti wa Simba aliyetimuliwa Ismail Rage

King Kibadeni
 * Mcroatia wa Gor Mahia, Matola waula

KAMATI ya Utendaji ya Klabu ya Simba imefanya mapinduzi yenye utata baada jana kutangaza kumsimamisha kwa muda usiojulikana Mwenyekiti wao, Ismail Aden Rage, lakini uamuzi huo ukionekana kwenda kinyume na Kununi za Shirikisho la Soka nchini, TFF.
Kamati hiyo pia imeamua kuwatimua Kocha Mkuu, Abdallah Kibaden "King" na msaidizi wake Jamhuri Kihwelu 'Julio' na kumtangaza Kocha mpya kwamba atakuwa ni raia wa Croatia, Zdravok Logarusic ambaye atasaidiwa na nahodha wa zamani wa timu hiyo ambaye kwa sasa anainoa Simba B, Selemani Matola.

Katiba ya TFF
Hata hivyo, Katiba ya TFF ambayo ndiyo Katiba mama inayopaswa kufuatwa na vyama vya soka na klabu zote zilizo chini ya shirikisho hilo lenye mamlaka ya juu kisoka nchini, hairuhusu mapinduzi na wajumbe wote wa kamati za utendaji wa kuchaguliwa wanatakiwa wakae madarakani kwa muda wa miaka minne.
Ibara ya 31 (6) cha Katiba hiyo kinaeleza kwa tafsiri isiyo rasmi; "Mjumbe wa kamati ya utendaji anaweza kuondolewa baada ya yeye mwenyewe kuandika barua ya kujiondoa, kutohudhuria vikao vinne mfululizo vya kamati ya utendaji, kushindwa kufanya kazi za kamati ya utendaji kutokana na kuugua hadi kufikia hatua ya mgonjwa mahututi ndani ya kipindi cha miezi 12 na kupatikana na hatia ya kutenda kosa la jinai au kufungwa pasi na dhamana."
Kusimamishwa kwa Rage kumetokea ikiwa ni siku mbili tu baada ya kiongozi huyo kukamilisha usajili wa wachezaji wawili wapya, kiungo Awadh Juma kutoka kwa mabingwa wa Tanzania Bara 1999 na 2000, Klabu ya Mtibwa ya Morogoro na mshambuliaji Ally Badru akitokea Klabu ya Canal Suez ya Ligi Kuu ya Misri.
Akizungumza jana kwenye makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mtaa wa Msimbazi, Kariakoo jijini Dar es Salaam, aliyekuwa Kaimu Makamu Mwenyekiti, Joseph Itang'are 'Kinesi', alisema kamati ya utendaji imemteua yeye kukaimu nafasi ya mwenyekiti.
Itang'are alisema kikao cha kamati hiyo kilichokutana juzi usiku kilifikia uamuzi huo kutokana na kutokuwa na imani na Rage na kueleza kwamba amekuwa akifanya maamuzi mbalimbali binafsi bila ya kushirikisha kamati.
Alisema maamuzi waliyofanya ni kwa mujibu wa ibara ya 30 (m) ya Katiba ya Simba na yametokana na sababu mbili, mojawapo ikiwa ni kitendo cha Rage kutangaza kuahirisha mkutano wa marekebisho ya katiba ya klabu hiyo kama walivyowaeleza wanachama kwenye mkutano mkuu uliopita.
"Mwenyekiti amekiuka masuala mbalimbali na maamuzi tuliyofanya ni sahihi kwa sababu tunataka Simba iende mbele, isirudi nyuma...ni kwa nia nzuri yenye lengo la kuboresha na siyo kumkomoa tu, wajumbe wote wa kuchaguliwa tulihudhuria akiwamo Hanspope (Zacharia) ambaye ni mjumbe wa kuteuliwa," alisema Itang'are.
Alieleza kuwa, kocha huyo mpya anatarajiwa kuwasili hapa nchini Desemba Mosi, mwaka huu na siku inayofuata ataanza kazi rasmi kwa ajili ya kuiandaa timu na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara utakaoanza Januari 25 mwakani.
Aliongeza kuwa, kamati hiyo itaitisha mkutano mkuu wa marekebisho ya katiba ifikapo Desemba Mosi ambao pia utajadili hatma ya mwenyekiti huyo waliyemsimamisha.
Akitangaza uamuzi huo, Itang'are alifuatana na wajumbe wenzake wa kamati ya utendaji ambao ni pamoja na Swedy Mkwabi, Ibrahim Masoud 'Maestro', Francis Waya, Saleh Pamba, Daniel Manembe, na Katibu Mkuu, Evodius Mtawala.
Rage hakupatikana katika simu yake ya mkononi kueleza maamuzi hayo ya kamati ya utendaji ambayo ilikutana siku moja baada ya yeye kusafiri.

TFF: Tunasubiri barua Rage kusimamishwa

TFF imesema itatoa ufafanuzi kuhusu kusimamishwa kwa Rage baada ya kupata barua rasmi kutoka kwa uongozi wa klabu hiyo kongwe nchini.
Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Boniface Wambura alisema bado hawajapata barua kutoka kwa uongozi wa Simba kuhusu kusimamishwa kwa kiongozi huyo.
"Kwa sasa hatuwezi kuzungumzia suala hilo kwa sababu bado hatujapata barua rasmi kutoka kwa uongozi wa Simba juu ya kumsimamisha mwenyekiti wao (Rage). Tutatoa ufafanuzi baada ya kupata taarifa rasmi," alisema Wambura.

Kumbuka
Ikumbukwe kuwa Kinesi alichaguliwa kama mjumbe tu wa kamati ya utendaji na makamu mwenyekiti ni nafasi ambayo anakaimu baada ya kujiuzulu kwa Geoffrey Nyange ‘Kaburu’.
Kwa mantiki hiyo, Simba kwa sasa inaongozwa bila kuwapo kwa kiongozi mkuu wa kuchaguliwa kwani tayari aliyekuwa Makamu Mwenyekiti, ‘Kaburu’ naye alijiuzulu na nafasi yake inashikiliwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji, Kinesi ambaye kwa sasa anaishikilia tena hiyo ya mwenyekiti.

Kibadeni alonga
Alipotafutwa na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana mchana, Kibadeni alisema hana pingamizi na uamuzi uliyofanywa na uongozi wa Simba dhidi yake na kwamba anasubiri barua rasmi juu ya kutimuliwa kwake.
"Mpaka sasa (saa 6:47 mchana) bado sijapata barua ya kusimamishwa kwangu kuifundisha Simba, lakini sina pingamizi lolote na uamuzi huo. Naamini nitalipwa haki yangu kulingana na makubalino yetu yaliyomo kwenye mkataba wangu na klabu," alisema Kibadeni.
"Nitaeleza zaidi kuhusu suala hili baada ya kupata barua rasmi ya kusitishwa kwa mkataba wangu na Simba," alifafanua zaidi Kibadeni, ambaye alianza kukinoa kikosi cha Simba msimu huu akitokea Klabu ya Kagera Sugar, akichukua mikoba ya Mfaransa Patrick Liewig, ambaye pia uongozi wa Simba ulisitisha mkataba naye baada ya timu yao kumaliza nafasi ya tatu katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita.
Julio hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo. Klabu ya Simba imekuwa na utaratibu wa kutimua makocha kila msimu, na wakati mwingine katikati ya msimu. Kutimuliwa kwa Kibadeni kunaifanya klabu hiyo kufikisha idadi ya makocha wakuu watatu waliotimuliwa ndani ya misimu miwili wakianza na Mserbia Milovan Cirkovic kabla ya Mfaransa Liewig.


NIPASHE

Mapenzi yasababisha maafa Dar, njemba yaua shemeji na kujilipua mwenyewe


Polisi wakikagua gari walilokuwa wakisafiria watu wanne kabla ya kushambuliwa kwa risasi na mtu alitajwa kuwa jina la Gabriel Munisi aliyedaiwa kuua watu wawili na yeye kujiua baada ya kujeruhi wengine jana asubuhi jirani na Club ya Wazee, Ilala, jijini Dar es Salaam. Picha na Silvan Kiwale 

DAR ES SALAAM. 

MFANYABIASHARA wa magari, Gabriel Munisi (35), jana alijiua baada ya kumuua mtu mmoja na kujeruhi wengine watatu jijini Dar es Salaam katika tukio linalohusishwa na wivu wa mapenzi.



Munisi, ambaye alikuwa mkazi wa Mwanza, aliwapiga risasi watu watatu akiwamo mchumba wake, Christina Alfred katika Mtaa wa Bungoni Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.

Baada ya kumpiga risasi mchumba wake huyo na kudhania kwamba amemuua, inadaiwa kwamba Munisi aliendelea kuwamiminia risasi watu wengine na kumuua mdogo wake Christina, Alpha (22).

Katika tukio hilo, Christina na mtu anayedaiwa kuwa mchumba wake mpya, Francis Shumila wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kujeruhiwa. Mama yake Christina, Helen Alfred amelazwa katika Hospitali ya Amana baada ya kujeruhiwa pia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marieta Minangi alisema Munisi alikutwa na bastola moja, magazini mbili na yalikutwa maganda 14 ya risasi zilizotumika na risasi mbili ambazo zilikuwa hazijatumika.

Tukio hili limetokea mwezi mmoja baada ya mwandishi wa habari wa ITV, Ufoo Saro kujeruhiwa kwa risasi na mzazi mwenzake, Anthery Mushi.

Katika tukio hilo, Mushi alijiua baada ya kumuua mama mzazi wa Ufoo na inaaminika pia tukio hilo lilisababishwa na masuala ya mapenzi.


Lilivyotokea

Mashuhuda waliokuwapo katika tukio hilo walisema mauaji hayo yalitokea saa 1.15 asubuhi baada ya Munisi kufika Ilala Bungoni na kwenda katika Klabu ya Wazee iliyo jirani na eneo yalipotokea mauaji na kunywa supu kabla ya kusogea karibu na lango la nyumba anakoishi mchumba wake.

Mmoja wa majirani, Noel Gerald alisema alimuona Munisi akiwa amesimama karibu na lango la nyumbani kwa kina Christina.

Alisema baadaye waliona gari aina ya Toyota Hilux, Surf, likitoka katika lango la nyumba hiyo na mara walimuona Munisi akimwamuru dereva ashushe kioo lakini alikataa na kudai kwamba ndipo alipoamua kuwapiga risasi waliokuwamo kwenye gari hilo. 
 
MWANANCHI

Ufaransa, Ugiriki, Croatia nao hizooo Brazili 2014

Benzema na wenzake wakishingilia bao alililofunga katika mechi yao ya usiku wa jana
MABINGWA wa Dunia wa mwaka 1998, Ufaransa jana walifanikiwa kufuzu kimiujiza mbele ya Ukraine kwenda kwenye Fainali za mwakani za Kombe la Dunia baada ya kupata ushindi mnono nyumbani wa mabao 3-0.
Ufaransa walionyukwa mabao 2-00 na wapinzani wao ugenini wiki iliyopita ilipata ushindi huo usiku wa jana na kufuzu kwa jumla ya mabao 3-2.
Mabao ya Mamadou Sakho, Karim Benzema na lile la kujifunga la Oleh Husyev iliisaidia Ufaransa kuungana na timu za Ureno, Ugiriki na Croatia kupenya katika kapu kushiriki fainali hizo za Dunia zitakazoifanyika nchini Ufaransa.
Kipigo cha awali cha mabao 2-0 kilikuwa kikiitisha Ufaransa kuzikosa fainali hizo, lakini Sakho aliianza kupunguza magoli kwa kufunga bao la kwanza dakika ya 22 kabla ya Benzema kuongeza jingine dakika ya 34. 
Kipindi cha pili mchezaji wa Ukraine katika harakati za kuokoa bao alijikuta akiiusindikiza wavuni katika dakika ya 72 na kupa tiketi Ufaransa bila kutegemewa na wengi.

Ronaldo aipeleka Ureno Kombe la Dunia, amzima Ibrahimovic

Kaka kubali yaishe mi zaidi yako: Ni kama Ronaldo anamwambia Ibrahimovic timu zao zilipokutana jana
MSHAMBULIAJI nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo usiku wa kuamkia leo aliifungia timu yake mabao matatu na kuivusha kwenda kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014, huku akimfunika kabisa mpinzani wake Zlatan Ibrahimovic.
 
Ureno ilikuwa ikirudiana na Sweden huku wachezaji hao wawili wakiwekwa kwenye mchuano usio rasmi wa nani zaidi kati yao wote wakiwa manahodha wa mataifa yao na Ronaldo kuonyesha ni zaidi kwa Mswidish huyo aliyeifungia timu yake mabao mawili.

Ushindi huo wa jana wa mabao 3-2 umeifanya Ureno isonge mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2 baada ya mchezo wao wa awali kushinda 1-0 nyumbani kwa bao la nyota wake huyo anayewania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia 2013.

Mkali huyo aliifungia timu yake mabao hayo yanayozidi kumsogeza kwenye tuzo hiyo ya FIFA katika dakika za 50, 77 na 79, wakati  Ibrahimovic alifunga dakika ya 68 na 72.
 
Kufuzu kwa Ureno kwa msaada mkubwa wa Ronaldo kumehitimisha 'ligi' baina ya mashabiki wa Ronaldo na Ibrahimovic waliokuwa wakiwapambanisha na sasa Ronaldo ataenda kuchuana na mpinzani wake wa La Liga Leonel Messi na Neymar.

Ghana, Algeria kafuzu Fainali za Kombe la Dunia 2014

Algeria na Burkina Faso zilipokuwa zikiumana
TIMU za taifa ya Ghana na Algeria zimekata tiketi za kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 zitakazofanyika nchini Brazil baada ya kupata matokeo tofauti katika mechi zao za mkondo wa pili za hatua ya mtoano.
Algeria ikiwa nyumbani ikiisimamisha Burkina Faso kwa kuilaza bao 1-0 lililokuwa likihitajika, huku Ghana wakichezeea kipigo cha mabao 2-1, lakini ikifuzu kutokana na ushindi mnono wa mabao 6-1 iliyopata katika mechi ya mkondo wa kwanza dhidi ya Misri.
Waalgeria walipata bao hilo mapema kipindi cha pili, kupitia kwa Madjid Bougherra na kufanya matokeo ya jumla yawe 3-3, baada ya awali Burkina Faso kushinda mabao 3-2.
Ghana wakiwa na hazina kubwa ya ushindi ilipigana kiume mbele ya wenyeji wao Misri walipata mabao mawili ya kila kipindi kutoka kwa Amri Zakhy na Gedo kabla ya Kelvin Prince Boateng kufunga bao la kufutia machozi dakika za 'jioni' akitokea benchi.
Algeria na Ghana sasa zinaungana na Cameroon, Ivory Coast, na Nigeria kukamilisha idadi ya timu tano za Afrika kwenda Brazil mwakani.