STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, November 20, 2013

Ronaldo aipeleka Ureno Kombe la Dunia, amzima Ibrahimovic

Kaka kubali yaishe mi zaidi yako: Ni kama Ronaldo anamwambia Ibrahimovic timu zao zilipokutana jana
MSHAMBULIAJI nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo usiku wa kuamkia leo aliifungia timu yake mabao matatu na kuivusha kwenda kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014, huku akimfunika kabisa mpinzani wake Zlatan Ibrahimovic.
 
Ureno ilikuwa ikirudiana na Sweden huku wachezaji hao wawili wakiwekwa kwenye mchuano usio rasmi wa nani zaidi kati yao wote wakiwa manahodha wa mataifa yao na Ronaldo kuonyesha ni zaidi kwa Mswidish huyo aliyeifungia timu yake mabao mawili.

Ushindi huo wa jana wa mabao 3-2 umeifanya Ureno isonge mbele kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2 baada ya mchezo wao wa awali kushinda 1-0 nyumbani kwa bao la nyota wake huyo anayewania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia 2013.

Mkali huyo aliifungia timu yake mabao hayo yanayozidi kumsogeza kwenye tuzo hiyo ya FIFA katika dakika za 50, 77 na 79, wakati  Ibrahimovic alifunga dakika ya 68 na 72.
 
Kufuzu kwa Ureno kwa msaada mkubwa wa Ronaldo kumehitimisha 'ligi' baina ya mashabiki wa Ronaldo na Ibrahimovic waliokuwa wakiwapambanisha na sasa Ronaldo ataenda kuchuana na mpinzani wake wa La Liga Leonel Messi na Neymar.

No comments:

Post a Comment