STRIKA

STRIKA

USILIKOSE

USILIKOSE

Wednesday, June 22, 2016

Hapana chezea Isha Mashauzi

Zaidi ya watu 30 wauwawa Libya

http://3.bp.blogspot.com/-zlLTmY7LcdM/TqbS4f7JW-I/AAAAAAAAIlg/H1jAnpeAzeo/s1600/Wapiganaji%2Bwa%2BNTC%2Bmjini%2BSirte.jpg
Picha haihusiani na taarifa hii
SIMANZI. Zaidi ya watu 30 wamepotea maisha katika mapigano baina ya Jeshi la Libya na wapiganaji wa kikundi cha IS.
Inaelezwa mapigano hato yamesananisha vifo hivyo, huku mamia wakiachwa majeruhi, kipindi hiki ambacho waumini wa Kiislam wapo kwenye Mfungo wa Ramadhani.
Kwa mujibu wa BBC Swahili, Msemaji wa hospitali moja alisema kuwa wapiganaji 36 wameuawa huku wengine karibu 140 wakijeruhiwa katika mji wa Sirte ambao ni ngome ya Islamic state.
Wakati huo huo taarifa zinasema kuwa idadi ya watu waliouawa wakati mlipuko ulitokea katika ghala la silaha kwenye mji ulio magharibi wa Garabulli imeongezeka hadi watu 29.
Ghala hilo liliripotiwa kuwa ndani ya kambi inayotumiwa na wapiganaji kwenye mji wa Misrata pwani ya nchi.

TFF mnatania au mnawataka ubaya Wekundu wa Msimbazi?!

http://www.timesfm.co.tz/wp-content/uploads/2016/04/Alfred-Lucas.png
Afisa Habari wa TFF, Alfred Lucas
http://3.bp.blogspot.com/-fwITBV-i6O4/UxIL74ckclI/AAAAAAAFQd8/1eC1K_-kKew/s1600/MMG25686.jpg
Mashabiki wa Al Ahly wakipewa sapoti na mashabiki wa Simba wakati wa mechi baina ya Wamisri hao na Yanga lililochezwa Uwanja wa Taifa hivi karibuni
BILA shaka Simba watakuwa wanacheka huko walipo, baada ya kulisikia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likiwaangukia na kuwataka wawe na uzalendo kwa kuishangilia Yanga itakapokuwa ikiumana na TP Mazembe Jumatano ijayo.
Simba na Yanga kwa miaka mingi zimekuwa zikishindwa kupigana tafu kwenye mechi zao za kimataifa, kwa tabia yao ya kushangilia wageni na kufikia hatua ya kuvaa jezi ya timu pinzani inayocheza na mmoja wao, lakini TFF kupitia Afisa Habari wake, Alfred Lucas imewaomba mashabiki kuwa wazalendo kuisapoti Yanga.
Lucas alisema TFF inawaomba mashabiki waje kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kushangilia kwani wanaamini mashabiki ni mchezaji wa 12 na uwepo wao utaongeza ari ya ushindi.
"Tunafahamu mchezo wa Yanga utakuwa na changamoto zake kwa vile  wameanza kwa kufungwa na TP Mazembe wanaongoza kundi lakini tunaamini watafanya vizuri kwani inachezwa kwa mtindo wa ligi hivyo mashabiki waje kushangilia timu zetu.", alisema Lucas.
Yanga itacheza na Mazembe Juni 29 kwenye mchezo wa Kundi A ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika na kusisitiza kuwa mafanikio ya Yanga ni faida kwa soka la Tanzania na kuomba mashabiki kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono kama ambavyo anataka wajitokeze Jumapili kuishangilia Serengeti Boys itakayocheza na  Shelisheli mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Vijana U17 Afrika.

Tayari mashabiki wa Simba wameshaanza kununua jezi za Mazembe ili kuwaunga mkono katika mechi hiyo na iwapo watasikia ombi hilo la TFF lazima wataumia mbavu kwa kucheka kwani ni jambo lisilowezekana kwao kama ambavyo kigogo wa klabu hiyo, Zakaria Hanspoppe aliwahi kukaririwa akisema huwa anahisi kichefuchefu akitajiwa jina la Yanga.

Jose Mourinho kumvuta Matic Man United

Matic na Mourinho walipokuwa Chelsea
KOCHA Mpya wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho anatarajiwa kumchukua nyota wake wa zamani aliyemnoa akiwa Chelsea kwa kubadilishana na Mchezaji wake mmoja kwa mujibu wa duru za kispoti za England.
Imeripotiwa kuwa wakati dirisha la usajili likitarajkiwa kufunguliwa Julai Mosi, Kocha Mourinho anatarajiwa kuitumia shauku ya Meneja mpya wa Chelsea kutoka Italy, Antonio Conte ya kumhusudu beki toka Italia, Matteo Darmian kwa kumtoa kama Ofa ya kumchukua kiungo wa Chelsea Nemanja Matic.
Tayari Mourinho ameshaanza kuisuka upya Man United kwa kumnunua beki wa kati kutoka Villareal, Eric Bailly na anatarajiwa kuongeza wapya wengine.
Matic, Mchezaji wa Kimataifa wa Serbia, alikuwa nyota wa kwanza kwa Mourinho kumnunua aliporudi Chelsea kwa mara ya pili kwa kumsaini mwaka 2014 kutoka Benfica na sasa inaelekea Mourinho anataka kuungana tena na Matic.
Chini ya Mourinho, Matic alikuwa na msimu mzuri wa kwanza huko Stamford Bridge na kuweza kutwaa Ubingwa wa England, lakini Msimu uliopita, hasa Mourinho alipotimuliwa Desemba mwaka jana, Matic hakuwa na namba mara kwa mara kikosini.
Haijulikani kama Matic atakuwa vipi chini ya Kocha Conte ambae bado hajatua rasmi huko Chelsea kwani yupo bado yupo na kikosi cha timu ya taifa ya Italia katika fainali za Euro 2016 zinazoendelea Ufaransa.
Magazeti huko England yamedai Darmian yupo kwenye uhusiano mzuri na Conte katika timu ya Italia, kwani panga pangua hakosi namba na hilo limeleta imani kuwa anamtaka wawe wote Chelsea.
Darmian amekuwa na msimu mchanganyiko Man United ambako alitua mwaka jana kutoka Torino ya Italia na hilo, pengine ndio linamfanya Mourinho amtoe kafara ili amnase Matic ambae hucheza kwa kutumia nguvu katikati ili kuimarisha safu yake mpya.

Yanga yaamua kuwachezesha Mazembe usiku

Kikosi cha Yanga

Mashabiki watakaoishangilia timu yao usiku Uwanja wa Taifa
Baadhi ya nyota wa Yanga akiwamo Nahodha Nadir Haroub Cannavaro atakayekuwepo kuivaa Mazembe
IMEFAHAMIKA kuwa, pambano la Yanga dhidi ya TP Mazembe la Kundi A michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika litapigwa usiku wa Jumatano na sio Jumanne kama ilivyotangazwa awali.
Kwa mujibu kutoka kwa Msemaji wa klabu hiyo, Jerry Muro, mechi yao itapigwa majira ya saa 1:30 usiku kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Muro alisema wameamua kulipeleka pambano lao Jumatano usiku ili kutoa fursa ya mashabiki wengi kuhudhuria baada ya kutoka kazini na wakishakula futari ikizingatiwa kwa sasa waumini wa Kiislam wapo kwenye mfungo wa Ramadhani.
Msemaji huyo alisema maandalizi yao kuelekea kwenye mchezo huo yapo shwari na kwamba wana uhakika wa kuwatumia baadhi ya nyota wao wapya ambao wamewasajili hivi karibuni akiwamo Mzambia, Obrey Chirwa, licha ya kwamba kuna nyota wao wengine watawakosa kwa kasi za njano walizopewa Bejaia Algeria.
Yanga ilipoteza mchezo wao wa kwanza wa kundi hilo dhidi ya MO Bejaia kwa kulala bao 1-0, wakati Mazembe watakaotua nchini Jumapili hii wakitokea kwao Lubumbashi waliitambia Medeama ya Ghana kwa mabao 3-1 na kuongoza msimamo.

Real Madrid yathibitisha kumrudisha Morata Santiago Bernabeu

http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2015/09/15/21/2C5ADD7700000578-3235796-image-a-30_1442348975933.jpgWAMEPANIA si mchezo. Mabingwa wa soka Ulaya, Real Madrid wamethibitisha kuwa Alvaro Morata atarejea Santiago Bernabeu kipindi hiki cha kiangazi. Taarifa z klabu hiyo zinasema kuwa, hakuna kizuia kwa mkali huyo kurudia nyumbani.
Awali taarifa za mapema kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Juventus Beppe Marotta zilibainisha kuwa Morata anategemewa kurejea Madrid.
Madrid walikuwa na nafasi ya upendeleo ya kumnunua tena Morata mwenye umri wa miaka 23, ikiwa ni sehemu ya mkataba uliopelekea nyota huyo wa kimataifa wa Hispania kujiunga na Juventus miaka miwili iliyopita na sasa wamethibitisha kufanya hivyo.
Katika taarifa yao iliyotumwa katika mtandao, klabu ya Madrid walithibitisha taarifa hiyo na kudai kuwa Morata atajiunga na mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya wa La Liga chini ya Kocha Zinedine Zidane.
Hata hivyo, taarifa hizo zinadai kuwa Madrid wanaweza kumuuza Morata kwa klabu nyingine ili wapate faida zaidi.

Shelisheli lazima wapigwe Taifa, kama unabisha subiri J'Pili


Wachezaji wa Serengeti Boys wakijifua mazoezi kujiandaa na mechi yao dhidi ya Shelisheli
LAZIMA wapigwe! Kocha wa timu ya taifa ya Vijana ya Tanzania U17 ‘Serengeti Boys’, Bakari Shime, amejigamba kuondoka na ushindi dhidi ya Shelisheli katika mchezo wao utakaochezwa Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam Jumapili hii.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Kocha Shime alisema timu yake ameiandaa vya kutosha ikiwa imepata mechi kadhaa za kimataifa za kirafiki hali iliyomwezesha kukisuka vema kikosi hicho.
“Naamini kwa maandalizi haya tutasonga mbele kwenye hatua inayofuata na vijana wana ari ya kwenda Madgascar 2017 kwenye fainali za mashindano haya”, alisema Shime.
Mchezo huo wa kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa kwa Vijana U17 utachezeshwa na waamuzi toka Ethiopia ambao ni Belay Asserese ambaye ni mwamuzi wa kati na wasaidizi wake ni Tigle Belachew na Kinfe Yilma Kinfe huku mwamuzi wa akiba akiwa  ni Lemma Nigussie na Kamishna wa mchezo huo atakuwa ni Bester Kalombo.
Serengeti Boys iliyoingia kambini  Juni 14, 2016 itarudiana na wapinzani wao  Julai 2, 2016, endapo itafuzu hatua hii itakutana na timu ya Vijana ya Afrika Kusini.
Naye nahodha wa timu hiyo, Issa Makamba amesema wapo tayari kupambana na anaamini ushindi ni wao huku akiwataka mashabiki kuja kuwashangilia.

Man City yakaribia kunasa kifaa kingine kipya

http://estaticos.marca.com/imagenes/2015/09/24/en/football/spanish_football/1443048045_extras_noticia_foton_7_0.jpgWANAMCHUKUA. Klabu ya Manchester City, ipo hatua ya mwisho kumnasa straika wa kimataifa wa Hispania, Nolito kutoka Celta Vigo.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 29 amethaminishwa kwa kiasi cha Euro Milioni 18 katika mkataba wake na Rais wa Celta Vigo, Carlos Mourino tayari ameshadokeza anategemea ataondoka dirisha hili la usajili.
Taarifa zilizotolewa na gazeti la Guardian la Uingereza zimedai kuwa, Man City ina uhakika wa kukamilisha dili hilo na kuongeza kuwa Nolito tayari ameshakubali mambo binafsi katika mkataba wa miaka mitatu atakaopewa wenye thamani ya Euro Milioni 4 kila msimu.
Straika huyo wa zamani wa Barcelona, aliyeichezea timu yake ya taifa ya Hispania katika mechi zote tatu za makundi ya michauno ya Euro 201, awali alikuwa akitajwa kuwindwa na timu yake ya zamani ya Barcelona iliyotaka kumrejesha kikosini.
Nyota huyo mwenye bao moja kwenye michuano hiyo ya Euro inayoendelea nchini Ufaransa, aliondoka Nou Camp mwaka 2011 kwenda Ureno kujiunga na Benfica  kabla ya baadaye kutua Celta Vigo.